Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

The bold naona wanalekebisha blog yao ili tuwe tunaingia kwa password na user name ...but now najaribu kujisajili inagoma
Najua yupo burn akirundi atatuelekeza vema
 
The bold Ndio nimeanza kuisoma hii hadithi. Nimeipenda kweli kweli. Lakini sasa hizo hashtag za kurasa zenye hadithi zimeishia 14 naipataje ya 15 na kuendelea??msaada mkuu Maana hii hadithi imenilaza saa 7 jana
 
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034



EPISODE 31



Nilikuwa natembea taratibu kana kwamba nanyatia kitu fulani. Kuna upende fulani wa moyo wangu ulikuwa hautamani nifike kule kwenye chumba cha ofisi ya Chifu, nilitamani niaifahamu kilichotokea, sikutamani kusikia ananiambia "tumezikosa files".

Nikapiga hatua za taratibu mpaka kwenye kile chumba anachokiita ofisi na kuingia.
Chifu mweneze alikuwa ameketi chini kwenye zuria la manyoya kama kawaida. Mbele yake kulikuwa na kifungu cha majani kama mchicha ambayo nilipoangalia vizuri ninagundua kuwa ilikuwa ni mirungi. Kwa kiasi fulani nilimuona kuwa alikuwa na wasiwasi japokuwa alikuwa anajifahidi aonekane yuko kawaida.

" Nini kimetokea Chifu?" Nikauliza nikiwa bado nimesimama mara baada ya kuingia.

"Kaa chini kijana!" Akanijibu bila kuniangalia.

Sikutaka kuwa mbishi, nikaa chini na kusubiri jibu lake.

"Wale watu ni kina nani hasa maana siku ile umekuja hapa na Eric mlinieleza juu juu tu.!" Akanijibu huku anaongea mdomoni amejaza fundo la mirungi shavu moja limetuna kama vile anaumwa jino.

"Chifu hayo sio maswali ya kuulizana sasa hivi.. Kama ulikuwa na maswali kama haya ungeniuliza toka juzi! Tafadhali nieleze ni nini kimetokea??" Nikamjibu huku nahema juu juu.

"Sijawahi kuona nyumba binafsi ina vault ndani, vault ambayo hata matawi ya kawaida ya benki hawana.. Na hizo files unazozitaka wanazilinda kuliko hata uhai wao.!" Akaongea bila kuniangalia, huku anachambua vijiti vya mirungi kwa mdomo utadahi mbuzi anatafuna mchicha.

"So what happened??" Nikamuuliza kana kwamba sikusikia alichokuwa anaongea.

"Aisee! Ilibakia kidogo tuwamiminie risasi kwa kujihami.. Ubaya tu nina Sheria moja katika kazi zangu.. Ni marufuku kuua mtu" akaongea huku anaendelea kuchambua mirungi kwa mdomo.

"Na files zimekuwaje?" Nikauliza safari hii kwa hasira.

"Tumezipata!" Akanijibu na kuniangalia usoni.

Nikahisi kama moyo umesimama ghafla. Badala ya kuruka kwa furaha, jasho likaanza kunitoka na presha kupanda tena. Sikutegemea hili jibu.!

"Whaaaat??" Nikauliza kwa mshangao nikihema.

"Ndio kijana.. Tumezipata file zako.!!"

"Ziko wapi?" Nikauliza kwa papara.

"Taratibu kijana.. Utafahamu! Nimekuita huku ofisini ili tuongee kwanza kabla ya kukukabidhi."

"Mambo gani?" Nikaanza kupandwa na hasira kwa mbali. Nikahisi kama huyu Mzee anataka kunizunguka.

"Una uhakika kuhusu ulichoniahidi.. Maana nadhani jinsi hili suala lako lilivyonigharimu.. Kijana wangu mmoja amepigwa risasi, nategemea atapona lakini itanigharimu fedha nyingi sana kumtibia na itachukua miezi mingi kabla hajarudi tena kazini.. Ndio maana nakuuliza una uhakika kuhusu ulichoniahidi?" Chifu akaniuliza huku amenikazia macho.

"Chifu nisikilize, nimekwambia nitakukabidhi kampuni ya ulinzi pamoja na tenda za kuanzia kazi moja kwa moja na namaanisha hilo.. Liko ndani ya uwezo wangu.!" Nikaongea kwa kujiamini ili kumpa Chifu uhakika wa ninachokisema.

"OK! Nataka iwe milioni 150.!"

"Milioni 150 zimefanyaje?"

"Huo mkataba wa kwanza wa tenda nitakaopewa, nataka thamani yake isipungue milioni 150"

"Its done! Nitahakikisha hilo linafanyika.." Nikamjibu tena kwa kujiamini.

"OK! Inabidi uondoke usiku huu na mzigo wako.." Akaongea huku anaanza kuinuka.

"Alafu sijaona kama mna huo mzigo kwa kadiri ninavyoufahamu 'mzigo'?"

"Kijana huwezi kufanya tukio na kwenda kulala chumba kimoja na ulichokiiba.. Ikitokea umekamtwa unakuwa umerahisisha kabisa kupatikana ushahidi... Kwahiyo tumeuhifadhi mahala Salama.. Ukishanieleza wapi unaelekea basi tutaangalia tuupitie vipi mzigo nikiwa nakusindikiza.."

"Nashukuru sana chief, asante sana kwa msaada wako… nakuahidi sito kuangusha kwa hili nililokuahidi!"

"Na jitahidi usiniangushe kijana.. Maana mimi sio serikali, nitakutafuta na tutamalizana kwa mtindo kama huu huu niliokusaidia.!"

Nikamuelewa. Hiyo "mtindo kama huu huu niliokusaidia" alikuwa anamaniisha risasi na umafia ulitumika kupata files.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza chief kunipiga mkwara tangu nimefahamiana naye, na nilijua fika kuwa alikuwa anamaanisha alichokisema.

"Kijana usidhani nawafukuza… mngeqwza kulala hapa muondoke kesho lakink kutokana na uzito wa hili suala sitaki wahusika wote tuwe sehemu moja ikitokea siri imevuja.. Kwahiyo hii ni tahadhari kwa usalama wetu sote… pamoja na hilo wale watu kule upanga kuna wawili tumewapiga risasi mguuni na mmoja ubavuni.. Sitaki waendelee kuvuja damu vile wasijekupoteza maisha yakazuka mengine.. Kwahiyo muda si mrefu tuna itaratibu wetu wa kuwataarifu polisi wafike pale" akaongea huku anabofya bofya simu na kuiweka sikioni.

"Usijali Chief! Naelewa vizuri tu!"

"Juma, lete gari nyumbani!" Akaongea na simu yake, kisha akakata.

"Kwa hiyo niwapeleke wapi?"

"Aaahh tupeleke tu magomeni.. Magomeni mapipa!" Nikawaza haraka haraka na kumjibu.

Tukatoka kule ofisini na kurejea sebuleni.

"Vipi huyo hali yake?" Chief akamuuliza moja ya mabinti wale wawili ambaye alikuwa anapita pita kila mara pale sebuleni.

"Imetengamaa kiasi!" Yule binti akajibu huku akielekea kule jikoni aliko kijana wa Chief aliyepigwa risasi.

Nikaenda mpaka alipo Cheupe na kuanzia kumsaidia kubeba mabegi yetu ya nguo na kumuashiria kwamba "safari imeiva".

" how is it?" Cheupe akaninongoneza.

"So far, so good" nikamjibu kwa sauti ya chini.

Tukatoka ndani pale wote wa Tatu mpaka nje kwenye geti. Hapo tukakuta kuna taxi imepaki, nikahisi huyu ndio Juma aliyepigiwa simu na chief kwamba alete gari.

"Kakabidhi hesabu kwa mama ndani mimi nina safari kidogo" Chief akamueleza Juma huku tukiwa tunapanda kwenye ile Taxi.

Chief akakaa kwenye usukani na mimi na Cheupe tukakaa siti ya nyuma. Safari ikaanza.
Tulipotokea tu barabara kubwa ya kizuiani, chief akatoa tena simu akabofya bofya kisha akaweka sikioni.

"Kilwa road, Mtoni kwa Azizi Ally! Niko na taxi yangu" akaongea na simu kwa kifupi tu kisha akakata simu.

Akaendesha gari huku wote tukiwa kimya bila kuongeleshana chochote mpaka tulipofika mtoni kwa azizi ally. Akapaki gari pembeni karibu na kona ya barabara inayochepuka kwenda Chang'ombe.

Tukasubiri hapo kama dakika tano hivi, mara ikaja gari 'Rav 4' nyeusi ikapaki karibu yetu.
Akashuka jamaa mwenye mwili uliojengeka hivi amevalia tisheti nyeupe na jinzi bluu.
Mikononi alikuwa amebeba "mikoba miwili myeusi ya kiofisi".! Roho yangu ikapasuka, paaaaaaaaaa.!!

Akaja mpaka kwenye dirisha la upande aliokaa chief, Chief akashusha kioo.
Hawakusemeshana chochote, yule jamaa akamkabidhi Chief mabegi kisha akarudi kwenye gari yake na kuondoka kwa mwendo wa kasi.
Chief akafunga kioo kisha akageuka na kunikabidhi "mzigo" wangu. Nikapokea huku mikono inatetemeka. Kwa kiasi fulani nilishindwa hata kushangilia maana nilijihisi kama vile naota. Finally, files ziko mikononi mwangu.!! Nilihisi hii ni ndoto hakika, labda nisubiri mpaka nikipata wasaa wa kuzipekua na kuhakiki ndio zenyewe ndipo nitang'amua huu ni uhalisia na si ndoto..!!

Cheupe akanikumbatia kwa nguvu na kunibusu shavuni, "You did it!"

Nikashindwa hata kujibu, nikabaki nakodolea macho tu ile mikoba niliyopewa.

Chief akawasha gari na tukaifuata tena kilwa road, kisha akaanza kuifuata Mandela Road.

"Mbona unapita huku, nimekueleza tunaenda magomeni mapipa!" Nikamueleza huku nimekumbatia "mzigo" wangu utadhani katoto kachanga.

"Tumepita hiyo njia wakati tunatoka upanga.. Sitaki kupita tena.. So tutapita ubungo, then tutarudi mpaka magomeni"

"Ooh OK!" Nikamjibu huku natazama ile mikoba yenye files.

"Unafahamu kilichomo kwenye hii mikoba? Umeangalia" nikamuuliza Chief.

"Hapana, sifahamu na sijaangalia.!" Chief akanijibu huku amekaza macho kwenye barabara.

"Hujapata hamu hata ya kuangalia ukizingatia jinsi tulivyosumbuka namna hii ili kuipata?" Nikamuuliza tena.

"Ray, kazi yangu ilikuwa kufanya ambush na kuchukua hiyo mikoba.. Kuhusu kilichomo ndani sihitaji kufahamu.. Hivyo ndivyo ninavyofanya kazi yangu.. Natimiza wajibu wangu tu! Mengine namuachia client mwenyewe.."

"OK! I like that, very professional.. Lakini mimi ningekuwa wewe ningechungulia walau mijue nilichomo ndani.!"

"Hahah! Ukizingatia kwamba watu tulioenda kuzipokonya walikuwa tayari kufa lakini sio kutuacha tuchukue hiyo mikoba.. Hiyo ina maana kuwa kuna siri nzito sana humo.."

"Kwahiyo hutaki kujua siri nzito?"

"Ray, kwa umri wangu huu na shughuli ninazozifanya nimejifunza mambo mengi sana.. Moja wapo ni 'mind your own business'.. Kutojiingiza kwenye mambo ambayo hayanihusu.. Na kuhusu kujua siri nzito, nimejifunza kwamba sio kila siri ina faida ukiijua.. Kuna siri nyingine ukishazijua zinakuondolea kabisa amani yako kwenye maisha.. Kwahiyo ni bora kutokujua muda mwingine"

Chifu akaongea huku macho ameyakaza barabarani. Maneno yake haya yalinichoma mno. Yalifanana kabisa na kile alichonihusia Kaburu kuwa nisiangalie hizi file nikipata, nisitake kujua kilichopo ndani.
Sikumjibu Chifu kitu chochote, nikakaa kimya tu.

Tulipofika Ubungo kwenye mataa tukapinda kulia kuifuata Morogoro Road na kama dakika 15 baadae tulikuwa tumefika Magomeni Mapipa.
Tukashusha mabegi yetu, Cheupe akiwa amebeba mabegi ga nguo na mimi nimeshikilia ile mikoba miwili myeusi.
Baada ya hapo, tukaagana na Chief na akaondoka na kutiacha hapo.
Ilikuwa tayari inakaribia mishale ya saa Tatu usiku hivi.

"Why tumekuja mapipa?" Cheupe akauliza mara tu baada ya Chifu kuondoka.

"Tunaelekea Ubungo Ila sikutaka afahamu tunakoenda.. Nadhani hata yeye amejua hilo.!"

Nikamjibu Cheupe huku naita taxi.
Baada ya taxi kuja tukapanda na akatupeleka moja kwa moja Ubungo. Tuliposhuka hapo ikabidi niongee na wale 'wapiga debe' wa magari ya mkoani kuwa tuna haraka tinaenda Iringa atuelekeza kama tunaweza kupata usafiri wa gari 'private' linaloelekea huko muda huu.

"Kuna jamaa ana Harrier anenda Mbeya, anataka abiria watano tu twendeni huku."

Tukaongozana naye mpaka karibu na Ubungo Maji.
Hapo tukakutana na hiyo gari na huyo muhusika. Alikuwa bado hajapata 'abiria' hata mmoja kwahiyo mimi na Cheupe ndio tulikuwa abiria qa kwanza. Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa elfu tano nikampa yule mpiga debe aliyetuleta ili aondoke tuongee na huyu jamaa.

"Mwana, sisi tunataka utuache Kibaha Maili moja tu hapo.." Nikamueleza baada ya yule mpiga debe kuondoka.

"Aaaaahh sasa maili moja si mpande Kosta au Noah, kuna gari kibao mnapata.." Jamaa akanijibu huku amekereka haswa.

"Tuna haraka sana ndio maana"

"Dah mi nataka abiria wa Iringa au Mbeya, angalau hata ungekuwa unaenda Morogoro ningekupakia"

"Skia mwana, nakulipa elfu hamsini… unatuacha Maili moja hapo unaendelea na safari zako naamini huwezi kukosa kichwa Chalinze au Morogoro"

"Uko serious??" Jamaa akaniuliza kwa mshangao.

Sikutaka maneno mengi, nikazama mfukoni na kutoa noti tano za elfu kumi kumi na kumkabidhi.
Tukapanda kwenye gari na kuondoka.

Uzuri ilikuwa ni Usiku kwa hiyo hakukuwa na foleni kubwa, mpaka kufikia saa Tatu na nusu tulikuw a tumefika Kibaha, Maili Moja.
Tukashuka kwenye gari na jamaa akendelea na safari yake ya Iringa.

Baada ya kushuka, tukavuka barabara mpaka upande wa pili na kuelekea Njuweni Hotel ambapo tukachukua chumba namba 1023 ili tupumzike kwa usiku wa Leo na kupanga mkakati wa hatua inayofuata kumaliza suala hili.

"Opppppppppsss…!!" Cheupe alijirusha kitandani baada ya kuingia chumbani.

"Pole mama, I can imagine kiasi gani umechoka.. It has been a long day.." Nikampa pole huku naweka mezani ile mikoba myeusi.

"Aiseee…" Cheupe akajibu huku anainuka kutoka kitandani na kuja karibu na meza niliposimama.
"Hongera sana kichwa.. You did it.!!" Akanipongeza na kunibush midomoni.

"No.. We didi.. Nisingefanikiwa hili bila wewe.. Thank you honey.." Nikamjibu huku namrudishia mabusu mdomoni.

"Sasa inabidi tujadili 'kifuatacho ITV' nikitoka tu chooni" akaongea huku anaelekea bafuni.

"Sawa mama!" Nikamjibu nikimuangalia akiingia bafuni na kufunga mlango.

Nikakaa kwenye kitandani na kuanzia kuvua viatu. Macho yangu yalikuwa yameganda kwenye ile mikoba myeusi yenye files za The Board. Kila nilivyojitahidi nisifikirie, nijifanye kama vile hazipo pale, lakini akili ilikuwa inakataa. Niliendelea tu kuikodolea macho.

Nikaanza kukumbuka maneno ya Chief, kwamba kuna baadhi ya siri ukizijua unaweza kujikuta unakosa amani maisha yako yote.

Kisha maneno ya Kaburu yakaanza kupita kichwani, kwamba nisifungue na kuangalia hizo files. Si lazima kujua kila siri. Kina siri ukizijua unaweza kujuta na kutamani usingeli zijua. Kwamba muda mwingine, 'ignorance is a blessing'.
Namna ambavyo Kaburu alinambia maneno yale ilikuwa kana kwamba kuna kitu Fulani hivi anakijua na kwa utashi wake alikuwa hatamani mimi nikifahamu kwa faida yangu.
Kadiri nilivyofikiria hivi ndivyo ambavyo moyo wangu ulizidi kutamani kujua kilichomo, japokuwa roho yangu ilikuwa inaniambia nisifungue hizo files lakini moyo ulikataa, ulitamani kujua kuna nini.

"Honeeeyy.. Mi naoga kabisa.!" Cheupe aliota kutoka bafuni.

"Okey honey!" Nikamjibu kwa kifupi.

Nikasimama na kuanza kusogolea tafatibu meza zenye ile mikoba kama vile nanyata.
Nilipofika mezani nikaushika mikoba mmoja na kuanza kuufungua. Mikono ilikuwa inatetemeka.

Ndani yake kulikuwa na mafaili makubwa manne. Kwa haraka haraka kila file ilikuwa na karatasi kwa makadirio zisizopungua mia moja.
File zile kwa juu ziliandikwa. TBS I, TBS II, TBS III na TBS IV.

Nikatafsiri hii 'TBS' kama 'The Board Strategy' hivyo nikaelewa kwamba mafaili haya ndio yalikuwa yanamikakati ya The Board, kuanzia mkamati wa kwanza mpaka huu wa sasa wa 34.

Nikaweka mkoba huu pembeni. Nitapitia hiyo mikakati mmoja mmoja baadae.

Nikafungua mkoba wa pili. Huu nao ulikuwa na mafile makubwa maane yenye karatasi nyingi kila file kama mkoba ule wa kwanza. Tofauti ni kwamba file hizi ziliandikwa tofauti.

File ya kwanza ilianzikwa; Brothers
Baada ya kupitia haraka haraka karatasi zake nikaelewa kuwa file hii ilikuwa na majina ya wanachama wa The Board tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa.

File ya pile iliandikwa; Friends
Nayo nilipopitia haraka haraka nikaelewa kuwa ilikuwa na majina ya vibaraka wa The Board serikalini na sekta binafsi na maelezo yao kuhusu maisha yao, familia zao, historia zao na kadhalika.

File ya tatu iliandikwa; Books
Nayo baada ya kuipitia haraka haraka nikaelewa kuwa ilikuwa na orodha za akaunti za siri za The Board, nyumba za siri, magari, kampuni na mali nyingine wanazozimiliki kwa usiri mkubwa.

File ya nne ilikuwa tofauti na nyingine zote. Kwanza ilikuwa juu imeandikwa Chairmen Memos.
Nikaelewa kuwa file hii ilikuwa imebeba moja ya siri kubwa zaidi ndani ya The Board.. Chairman!
Ndani yake ilikuwa na vi-file vingine vidogo vitatu.

Ki-file cha kwanza kiliandikwa SIR. NIXON MURPHY (1951 - 1968). Kilikuwa na kama karatasi ishirini hivi au thelathini.

Ki-file cha pili kiliandikwa CHANDE R. CHANDE (1968 - 1984). Hiki kilikuwa na kama karatasi hamsini hivi.
Nikapigwa na butwaa na bumbuwazi. Chande Ramadhani Chande, Waziri Mkuu kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi kumbe alikuwa ni mwanachama wa The Board. Na sio mwanachama tu bali pia alikuwa Chairman. Aisee..

Nikafungua ki-file cha tatu.

Ki-file hili kilikuwa tofauti kabisa na file zote. Kwanza kilikuwa na karatasi nyingi zaidi, kama karatasi mia hamsini au mia mbili hivi.

Nilipoangalia juu kilivyoandikwaanzoni nikahisi nimesoma vibaya. Baada ya kusoma tena mara ya pili nikahisi labda macho yangu yana tongo tongo hayaoni vizuri. Nikayafikicha kwa nguvu na kusoma tena.
Sikukosea, wala sikuwa naota, nilichokiona ndicho kilikuwa sahihi. Nilisikia kama moyo unataka kupasua kifua na kutoka kwa jinsi ulivyodunda kwa nguvu.

Nikahisi pumzi zimekata. Mwili mzima ilikuwa ganzi sikuweza hata kutikisika. Ndani ya sekunde kumi tu shati lilikuwa limelowa jasho kama nakimbia marathoni.
Nisikia kichwa kinakuwa chepesi, nilisikia kama nataka kufa. Nilijihisi kama ufahamu unapotea.

Ile file ndogo ya tatu ilikuwa imeandikwa.


CHARLES B. KAJUNA (PRESENT)



"Ray… Ray! Ray.. Raaayyyyy!! Rayyyy.!!

Sijui ni kwa muda gani Cheupe alikuwa amesimama pale chumbani na kuanza kuniita baada ya kutoka bafuni. Inawezekana hata ni dakika kumi nzima, lakini sikusikia mpaka sasa hivi. Akili haikuwepo kabisa, na hata mimi mwenyewe nilihisi sikuwepo.

"Ray.. What's wrong!" Cheupe akaniuliza huku amekodoa macho kwa woga kuniona katika hali ile.

Nikageuka kama roboti kumuangalia nikiwa bado kamkama sijitambui, na neno pekee nililoweza kulitamka ni,


"Cheupe... we are in big trouble.!"




NB: Nadhani nilishatoa ufafanuzi kwanini The BOld hayuko hewani.. i hope diferences zake na JF watazimaliza soon na kurejea.. shykrani sana kwa kujali uwepo wake humu.. pia kumradhi kwa website kutokuwa hewani leo.. nadhani mnajua tena jambo jipya changamoto hzikosekani.. kuna marekebisho machache yanafanyika.. Tuko pamoja wakuu.. we miss you alot..



Itaendelea kesho…
 
EPISODE 31, POST # 4251



Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove
 
Website haifunguki

194ef34e77b5532b1e358778e4b4b8cb.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom