VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034
EPISODE 27
Zilikuwa zimepita siku mbili toka nilipie kodi katika jengo ambalo ndilo nilikua nimedhamiria kukifanya kuwa ofisi ili kufanikisha mpango wa kuzipata files kutoka katika strong room ya Makao makuu ya benki.
Ofisi ilikuwa na vyumba vitatu.
Chumba cha mbele kabisa tulipanga kitumike kama mapokezi, chumba kingine tutakitumia kama chumba cha mikutano na chumba kinachobakia kitatumiaka kama ofisi yenyewe.
Katika hiki chumba cha ofisi nilijitahidk walau kiwe na mzingira fulani ya kuonekana kwamba ni ofisi halisi.
Kwahiyo nilikweka kabati zuri la "kichina" na kuweka files, meza nzuri ya kichina pia, pamoja na kiti kizuri cha "executive".!
Wote watatu tulikuwa hapa 'ofisini'. Yaani mimi, kaburu na Cheupe.
"Mnaonaje tangazo limekaa poa?" Nikawauliza, mimi nilikiwa nimekaa kwenhe kiti, kaburu alikuwa mkono wangu wa kushoto na Cheupe mkono wa kulia wote wameniinamia wakiasoma nilichokuwa nimekiandika kwenye laptop.
"Imekaa poa nadhani, I hope it's going this is going to work.. La sivyo tutaozea jela TISS wakitukama huu mchezo tunaoufanya" Kaburu akaongea huku kama kawaida hake akiweka tahadhari.
Katika laptop, hilo "tangazo" lenyewe nilikua nimeliandika kama ifuatavyo:
"Exciting opportunity... Kama unataka kufanya kitu cha tofauti na kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.. Si kwa faida ya kiuchumi pekee bali pia kubadili ulimwengu
Tunaitwa UNIMAX MARKETING, Tunatafuta vijana 12 wenye good Marketing Skills
Tupigie: 0718 096 811"
"Looks good.!" Cheupe naye akakubali kuwa tangazo limekaa poa.
"OK.! Napost sasa.!"
Nikaanza kupost tangazo kwenye miamtandao mbali mbali. Lakini hasa hasa nililenga mtandao wa Jamii Forums na mtandao wa Zoom.
Nikafungua anuani ya zoom na baada ya kujisajili.. Nikapost tangazo.
Baada ya hapo nikafungua anuani ya tovuti ya Jamii Forums, kisha nikatumia kama dakika tatu au nne kujisajili kama mwanachama kisha nako nikapost tangazo.
"Tayari..!" Nikaongea huku nainuka kwenye kiti na kujinyoosha.
"Kwahiyo kifuatacho itv??" Cheupe akauliza.
"Tunasubiri response ya watu watakaotutafuta"
Nikaongea huku naangalia simu mezani.
Nilikua nimechukua simu moja kati ya zile nilizonunua Dodoma na kuweka 'line' yenye namba 0718 096 811 kama Namba ya mawasiliano ya "kampuni" ya Unimax Marketing.
"Ray hii idea yako itatufitinisha na TISS, I can feel it" Kaburu akaongea huku anatembea tembea mule ndani ofisini.
"Usijali kuhusu TISS, wanachotaka ni file za The Board haijalishi tunazipataje" nikamjibu huku nakaa tena kwenye kiti.
"Yeah! Lakini sio muda wote ambapo 'the end ina justify the means'" Kaburu akaongea tena akinipa tahadhali.
"Man, if you have a better idea let’s hear it... Sioni njia nyingine aisee" nikamjibu.
"It's genius though.!" Kaburu akaongea kwa kuniinjoi.
"Hahaha.!" Nikacheka kwa kumuinjoi pia.
Tukaendelea na maongezi kwa takribani dakika kumi nyingine. Mara ghafla simu pale mezani ikaanza kuita.
"Here we go!" Nikainua simu na kuipokea kwa shauki kubwa.
***************
October, 1974: Dar es Salaam
Charles Kajuna alikuwa na heka heka za kiofisi kwa muda wa takribani miezi sita yote hii.
Rais alikuwa amemchagua kuwa Katibu Mkuu wa Hazina, ingawa nafasi hii alikuwa amepewa kama 'cover' kwa ajili ya shughuli maalumu aliyokuwa amempa.
Charles alipewa jukumu kuu la kusimamia uanzishwaji wa benki kuu ya Tanzania.
Kwa miezi sita yote hii alikuwa anasafiri kila kona ya dunia ili kufanikisha suala hili.
Rais alikuwa anataka mpaka kufikia mwezi January 1975 nchi tayari iwe na benki kuu.
Charles ndio alikuwa amerejea kama wiki moja iliyopita akitokea Makao makuu ya IMF ambao walikuwa wanasaidia kuandaa muswada wa kuwasilisha bungeni ili kuanzishwa kwa benki kuu (Central Bank Legislation).
Baada ya kurejea, Charles alikuwa anaendelea na mchakato wa kutengeneza timu ya wataalamu watakaokuwa kama wafanyakazi wa mwanzo kabisa wa Benki kuu na watakaosaidia kuanza kwa shughuli za benki kuu.
Hii ilimlazimu kuchukua mpaka wataalamu wengine kutoka nje ya nchi, kwa mfano alimchagua Mr. Cleoford Truman kutoka Benki kuu ya Uingereza kuwa Meneja wa kitengo cha Currency an Domestic Banking Operations.
Vivyo hivyo kulikuwa na wataalamu kutoka nchi nyingine kadhaa.
Mwishoni mwa mwezi huo wa Octeber ndipo akataarifiwa kuwa kampuni ya ya Messrs Thomas de la Rue kutoka uingereza ambao walipewa tenda ya Sarafu na noti walikuwa tayari kuleta mzigo wa kwanza wa sarafu ndani mwezi mmoja ujao.
Kwa kuwa benki kuu ndio kwanza ilikuwa inaannza, hivyo haikiwa na Strong Room kwa ajili ha kuhifadhi kiwango kikubwa hicho cha Sarafu.
Ndipo hapa intupeleka kwenye kikao cha siri kubwa ambacho waziri wa fedha Ndugu, Abdul Aziz na mzew tajiri Chifu Sekioni ambao wote ni mwanachama wa kikundi cha siri cha The Board, walimuita Charles ili waweze kumpa maelezo ha kumshawishi Rais juu ha namna ha kuifadhi huo mzigo wa Sarafu utakao wasili.
Kipindi haya yote yanatokea, Charles alikuwa anamalizia ujenzi wa nyumba yake maeneo ya Upanga.
Kipindi kile April, alipoitwa na Rais akitokea Nairobi na baadae kukabidhiwa nyumba ya serikali maeneo ya Mikocheni A, mkewake akiwa bado mjamzito alikiwa anachefukwa sana na harufu kutoka baharini.
Hii ilimfanya katika wiki zile zile za kwanza kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga nyumba.
Akafanikiwa kupata plot maeneo ya Upanga mtaa wa Kilombero na mara moja akamlipa mkandarasi shilingi laki moja na nusu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
Hadi kufikia muda huu octoba, mkewe alikiwa ameshajifungua tayari mtoto wa kike aliyempa jina la mama yake, Dorothea!
Nyumba yao ya Upanga ilikuwa imeisha na ilikuwa inafanyiwa 'finishing' ndogo ndogo.
Sasa, katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwezi oktoba ndipo alipoitwa katika kikao cha siri na Waziri wa fedha Ndugu, Abdul Aziz na Chifu Sekioni.
Kikao hiki kilifanyika usiku Nyumbani kwa chifu Sekioni maeneo ya Oysterbay.
Walikuwa peke yao watu watatu tu katika sebule kubwa ya nyumba hiyo.
Baada ya maongezi ya hapa na pale, hatimaye ukawadia wasaa wa kujadili lililowakutanisha hapo.
"Kajuna, nadhani wote hapa tunafahamu kuwa mwezi ujao tunapokea shehena GA kwanza ya Sarafu" akaongea Waziri Abdul Aziz.
"Ni sawa kabisa ndugu Waziri" Kajuna akaitikia.
"Nadhani unafahamu kuwa ni kwa kiasi gani tunahangaika kupata sehemu yenye kutosha na usalama ya kuhifadhi kiasi kikubwa hicho cha Sarafu" akaendelea kueleza Waziri Abdul Aziz.
"Ni kweli lakini nadhank juzi tulishauriana mimi, wewe na waziri wa mipango kuwa shehena ya Sarafu ihifadhiwe kwenye majengo ya Makao makuu ya jeshi pale mgogoni" Charles akafafanua, akieleza kuhusu makubaliano hayo ya kuhifadhi Shehena ya sarafu kwenye makao makuu ya jeshi ambapo kipindi hicho yalikuwa yapo magogoni.
"Hiyo ndiyo sababu ya kukuita hapa Charles" akadakia Chifu Sekioni.
"Ndio Chifu!" Charles akaongea akimsikiliza Chifu Sekioni.
"Siku chache zijazo wewe na Waziri hapa mtaenda kumbrief Rais kuhusu uamuzi mlioufikia kuhusu sehemu ya kuhifadhi Sarafu.. Sasa waziri kuna jambo atalendekeza tunataka uliunge mkono kwani unafahamu katika hii ishu ya Uanzishwaji wa benki kuu hakuna mtu ambaye Rais ana muamini zaidi yako" Chifu Sekioni akafafanha kwa kirefu.
"Charles.." Akaanza kuongea, "tukienda kumbrief Rais kuhusu hifadhi ya shehena ya Sarafu nitapendekeza kuwa tusihifadhi shehena yote TPDF.. Kiasi kidogo walau hata robo ya shehena nzima tihifadhi sehemu nyingine"
"Na kwanini tihifadhi sehemu nyingine?" Charles akauliza.
"Nitampa sababu yoyote ile, mfano labda pale TPDF hapatoshi kuhifadhi sarafu zote.. Au si shahihi kimkakati kuweka shehena yote sehemu moja na kadhalika na kadhalika.. Nitatafuta sababu yenye kufaa kumpa" waziri Abdul Aziz akaeleza.
"Na ulikuwa unapendekeza hiyo robo ya shehena ikahifadhiwe wapi?" Charles akauliza kwa shauku.
"Nadhani kuna nyumba unaijenga pale upanga na bado haujahamia kwa hiyo....."
Kabla Waziri hajamaliza, Charles akamkatisha.
"No no no!! Huo utakuwa uhuni uliopitiliza.. Hatuwezi kuhifadhi Sarafu za serikali ya Jamuhuri kwenye personal property!! Siwezi kukubali hilo" Charles akaongea kwa kupaniki mpaka akainuka kutoka kwenye kiti pale sebuleni
"Sikiliza Charles.. Kama waziri nitasimamia mchakato kuhakikisha tunakodi jengo lako kwahiyo wewe hautaishi pale.. Pia milango itaboreshwa kuwekwa milango mingine na maafisa wa TPDF watakiwa wanalinda masaa 24 kwahiyo hakutakuwa na upotevu wowote qa Mali ya umma" akaongea waziri kumpooza Charles ambaye alikuwa amekwishaanza kupaniki.
"Kwahiyo sababu hasa ya kutaka kuhifadhi sarafu kwenye private propeprty ni nini?" Akauliza Charles akiwa amepoa kidogo na kukaa chini kwenye kiti.
"Tunaamini kuwa ukisha teuliwa kuwa gavana walau utakuwa na 'access' ya urahisi kwenye strong room ktakayokuwa upanga kuliko strong room ya magoglni ambako kuna ofisi ya CDF." Waziri Abdul Aziz akafafanua.
"Na sababu ya kunitaka niwe na access ya ufahisi kwenye strong room ni ipi?" Charles akahoji.
"Kuna nyaraka Chairman anataka kukupa na anahitaji zihifadhiwe sehemu salama salama haswa! Ni nyaraka nyeti mno" akaongea waziri.
"Chairman, chairman, Chairman!! Huu mwezi wa sita sasa nimekuwa mwanachama wenu lakini simjui hata kwa sura huyu Chairman zaidi ya kusikia tu kila siku.. Chairman, Chairman!!" Charles akaongea akiwa na hasira kidogo.
"Utaonana naye ndani ha wiki mbili zijazo! Anahitaji kuonana na wewe kwa sababj maalumu" akadakia Chifu Sekioni.
"Sababu gani?" Charles akaongea kwa mshangao na shauku kubwa.
"Amekuchagua kuwa 'The Book Keeper'" akamalizia Chifu Sekioni.
Itaendelea Jumatatu…