VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034
EPISODE 14
(Mara ya kwana kupost hii Episodes kwenye group whatsapp baadhi walidhani kuna sehemu nimeruka au nimekosea.. Mzigo haujarukwa wala kukosewa.. endelea kusoma na kufuatilia utaelewa)
GEREZA KUU LA MOROGORO
SIKU YA PILI
Kengere ya kuashiria muda wa chakula cha mchana Ilikuwa imepigwa tayari na wafungwa na mahabusu walikuwa wanaondoka yard kuelekea upande wa gereza wenye jiko.
Wakati wenzetu wanaelekea jikoni kuchukua chakula mimi na Godi tulibakia yard namba mbili.
Tukasubiri kama dakika tano tukiwa peke yetu kabisa yard yote, kisha ndio tukamuona Obama, yule askari magereza mstaarabu akija pale tuliposimama.
"I really hope unajua unachokifanya la sivyo wote tutaongia kwenye matatizo" Obama akaongea huku ananikabidhu funguo.
"Usijali mkuu, kila kitu kitaenda sawa!" Nikamjibu huku napokea funguo kwa kuificha kiganjani na kuiweka mfukoni. "Msauzi umempanga lindo pale nilipokueleza?" Nikamuuliza.
Obama akaitikia kwa kichwa kisha akageuka haraka na kuondoka.
"Ray, ungenidokeza japo kidogo huu mpango wako labda inaweza kusaidia! Usisahaunkuwa nina uzoefu mkubwa wa jela kuliko wew" Godi akaniuliza kwa shauku huku tunatembea kuelekea yard namba moja.
"Tatizo ni kwamba nikikwambia hauwezi kukubaliana nao" nikamjibu huku natembea kwa haraka.
"Unasemaje????" Godi akahamaki. "Kama una uhakika siwezi kukubaliana nao maana yake huo mpango wa wa hovyo"
"Ni kweli ni mpango wa hovyo lakini Nina hakika utafanikiwa, na bora kuwa na mpango wa hovyo kuliko kutokuwa na mpango wowote" nikamjibu.
"Na Obama umefanikiwaje kumshawishi hicho ulichoenda kumshawishi mpaka amekubali kukuletea funguo!!"
"Nitakuambia usijali" nikamjibu kwa mkato huku bado tunatembea kwa haraka na tahadhari kuelekea yard namba moja.
"Unaonaje ukiniambia sasa?" Akaniukiza huku ananishika bega nipunguze mwendo.
"Shiiiittt!! Una mpango mwingine wowote wa namna gani tunaweza kumfanya Kaburu asitishe kwenda ofisini kwa mkuu wa gereza???" Nikamuuliza kwa kufoka huku namtazama usoni. Godi hakujibu chochote. Nikaendlea kuongea, "sasa kama huna plani yoyote, unaonaje ukiacha kubwabwaja na kuniuliza maswali na badala yake ufanye kile ninachokueleza?" Nikaongea kwa kufoka.
"Ok! Poa.." Akajibu kwa kifupi.
Tulikuwa tumeshafika yard namba moja, ambapo napo yard yote tulikuwa peke yetu, wafungwa wote na mahabusu wameenda kula.
"Ok! Selo ya Blaki iko wapi?" Nikamuuliza Godi.
"Selo namba 46, ile kule mwishoni" akanijibu huku tunatembea kuifuata selo ilipo.
"Una uhakika bangianazowauzia wafungwa anaziweka humu ndani??" Nikamuuliza tukiwa tayari tumefika nje ya selo namba 46.
"Nisingekuwa na uhakika nisinge kwambia! Blaki ni kama kiwanda humu ndani unaweza kukuta ana kete hata mia tano humo ndani" Godi akaongea.
"Ok!!" Nikajibu kwa kifupi huku nafungua kufuli kubwa la Chuma lilikuwa linaning'inia selo namba 46.
Nikalifungua haraka haraka kisha tukaingia wote wawili. Ndani ya selo kulikuwa na magoro matatu yamepangwa pembeni na upande mwingine kulikuwa na mabegi ya mgongoni kama matatu hivi na yote kwa muonekano wa haraka haraka yalionekana yalikuwa na nguo ndani.
Nikang'amua kwamba begi mojawapo kati ya hayo atakuwa ameficha misokoto yake ya bangi anayouza humu jela ila amechanganya na Nguo ili isionekane kwa urahisi. Hatukuwa na muda wa kusachi kwa hiyo tukayabeba mabegi yote matatu na kuondoka nayo.
Tukatoka nje na kuanza kuondoka.
"Umesahau kufunga mlango!" Godi akageuka na kunionyesha mlango ambao niliuacha wazi.
"Sijasahau! Nataka ubaki hivyo" nikaongea huku natembea kwa haraka.
Tukarudi tena yard namba mbili na mabegi yetu.
"Ok! Selo ya Bokela iko wapi?" Nikamuuliza huku napepesa macho huku na huku.
"Ile kule nayo iko mwoshoni namba 75" akanijibu kwa haraka na tukaanza kutembea haraka haraka kuifuata.
"Kwa hiyo hawa ndio madoni wa kuuza bangi humu jela" nikamuiliza tukiwa tunaikaribia selo namba 75.
"Ndio hawa! Wote ndio madoni wa bangi humu lakini Blaki ndio nyoko zaidi, ana wapambe karibia ishirini humu ambao ni kama misukule yake akiwaambia chochote wanatekeleza bila kuuliza! Bokela yeye kwa hesabu ya haraka haraka wapambe wake hawavuki kumi" Godi akaongea tukiwa tumefika nje ya sell namba 75.
"Ok naomba kibiriti!" nikaongea huku naweka mabegi chini nje ya selo namba 75.
"Nimepata kibiriti ila ujue kwamba kibiriti ni bidhaa adimu humu, so nilicbofanikiwa kupata ni hiki" Godi akaongwa huku ananikabidhi njiti moja ya kibiriti na kipande cha karatasi cha kibiriti ile sehemu ya kahawia ya kuwashia.
"Itatosha! Good job" nikavipokea
Tukaangaza macho huku na kule pale yard kuhakikisha hakuna aliyerudi kuona na kutubamba tukifanya hiki tunachokifanya.
Nikaanza kuiwasha ile njiti kwa umakini sana huku Godi amezungusha mikono kuzuia upepo usiizime pindi ikiwaka.
Hatimaye ikawaka na nikachukua karatasi kidogo pembeni na kuiwasha pia ili kupata moto mkubwa kisha nikaanza kuyaunguza yale mabegi kwa chini moja baada ya jingine.
Tulipoona mabegi yameanza kushika moto, tukainuka kwa haraka na kuondoka yard na kuyaacha mabegi pale pale nje selo namba 75.
Tukaelekea upande wa mbele wa gereza kule jikoni na kupanga foleni ya chakula.
Kwakuwa tulikuwa tumechelewa kuja huku kwahiyo tukajikuta tuko mwisho kabisa foleni. Lakini kitu kilichomshangaza Godi ni kwamba tuliyemkuta nyuma kabisa ya mstati kabla yetu alikuwa ni Sinyorita.
Godi akageuka kwa mshangao na kuninong'oneza.
"We mseng* umepanga nini kitokee?? Na huyu choko uliongea naye nini jana nilipokuitia?" Akauniliza kwa kuninong'oneza ili Sinyorita asisikie.
"Utaona ndani ya dakika chache! Relax" nikaongea huku natabasamu kwa wasi wasi.
Magereza mengi ya Tanzania hayana 'mesi' ya kulia chakula. Hivyo gereza hili la Morogoro walikuwa na utaratibu kwamba ukishachukua chakula unasubiri mpaka watu waishe kwenye foleni au kubakia kidogo kisha mnaeuhusiwa mrudi yard na vyakula vyenu mkale.
Wakati tunafika kwenye foleni kulikuwa na kama watu thelathini hivi, lakini sasa tulikuwa tumebaki kama kumi hivi.
Afande Msauzi akafungua geti na kuruhusu watu waanze kurudi yard wakalw chakula.
Dakika kama tatu baadae baada ya watu kuruhusiwa kurudi yard ambapo kwenye foleni tulikuwa tumebaki kama watu watano hivi, ghafla tukaanza kusikia kelele kubwa za kishindo zinasikika kutoka yard.
Zilikuwa kelele kubwa hasa kama vile watu wanashangilia au kama wako kwenye uwanja wa vita wanapambana. Kelele zilizidi kila sekunde zilivhokuwa zinasonga,n ghafla tukasikia askari magereza aliyepo yard anapiga filimbi ya kuashiria hatari. Kadiri filimbi ilivyokuwa inapigwa na kelele zilizidi kuwa kubwa zaidi.
Wale wenzetu tuliokuwa nao kwenye foleni wakasahau ghafla hata swala la chakula wakakimbilia yard kwenda kushuhudia kinachoendelea.
Kwahiyo kwenye eneo hili tulibaki mimi, Godi, Sinyorita, Msauzi na wapishi jikoni.
Filimbi ya hatari ilipulizwa kwa nguvu zaidi na kishindo cha kelele kilizidi kuwa kikubwa.
Ghafla akatokea askari magereza kutoka kwenye ule mlango wa kwenda maofisini alikuwa anakimbia huku amebeba bunduki begani anaelekea yard.
Alipopita tu pale mlangoni kunakoelekea yard, Msauzi akaniangalia. Nikampa ishara kwa kumuitikia kwa kichwa. Akafunga geti kisha na yeye akakimbia kwenda yard.
Kwa hiyo katika eneo hili kwa sasa tulibaki mimi, Godi, Sinyorita na wapishi wa jikoni.
Kama sekunde kumi baada ya yule askari mwenye bunduki kupita na Msauzi kumfuata, tukasikia mlio mkali wa risasi. Mlio huo mkali ulisikika kwa kishindo mara tatu. Risasi tatu zilikuwa zimepigwa hewani. Wote kwa haraka tukajirusha na kulala chini mikono kichwani.
Hiyo ndiyo ilikuwa protokali ya magereza Tanzania. Kukitokea hatari askari anaoiga filimbi ili mlale chini, kama msipotii basi zinapigwa risasi hewani.
Baada ya hapo askari anaruhusiwa kumpiga risasi mgungwa yeyote ambaye atakuwa bado amesimama.
Kwahiyo kwa haraka sana tukalala chini, mpaka wapishi kule jikoni nikawaona nao wamejirusha kulala sakafuni.
Nikaangaliana na Sinyorita na kumpa ishara kwa kichwa.
Sinyorita akainuka kwa haraka na kukimbia kwa kunyata kuelekea kule kwenye mlango wa kuingia kwenye maofisi ya magereza. Akapita mlangoni ambao ulikuwa umeachwa wazi na yule askari mwenye bunduki na akatokomea huko ndani kwenye maofisi.
Tukiwa tumelala chini pale pale Godi akanigeukia na kuniangalia kwa mshangao.
"Kumanina zako! Nishaelewa ulichokilenga" akaongea na kutabasamu.
Kama dakika tatu baadae Msauzi akarejea kwenye eneo hili lenye jiko na akaongea kwa mamlaka na kwa kufoka.
"Wafungwa, mahabusu wote kwenda yard namba moja!! Wote yard namba moja" akaongea huku anatembea.
Wote tuliokuwa hapa, mimi, Godi na wapishi tukainuka na kuanza kukimbia kuelekea Yard namba moja.
Zaidi ya mimi na Godi, hakuna mwingine aliyekuwa anajua kuwa Sinyorita ameingia kule kwenye maofisi.
Tulipofika yard namba moja tukawakuta wafungwa wote na mahabusu wamejaza kwenye eneo hili.
Kwa kawaida wafungwa wakiwa wametapakaa yard ya kwanza na ya pili unaweza kuhisi gereza lina watu wachache sana. Lakini tulipokuwa tumekusanywa hapa na kujazana ndio nikapata picha halisi jinsi tulivyo kuwa wengi.
Watu wote walikuwa wamekalishwa chini kitako.
Mbele kabisa ya yard walisimama maaskari kama watano hivi na yule mmoja mwenye silaha. Pembeni yao kulikuwa na watu kama kumi na tano wamepigishwa magoti na karibia wanane kati yao walikuwa wanavuja damu kutokana na majeraha kichwani. Hawa walikuwa ni Blaki, Kobelo na wapambe wao.
"It's namba kuanzia mwisho huko" askari mmoja akafoka.
Wafungwa wakaanza kuhesabu namba kwa kutamka kwa sauti.
Ilichukua karibia dakika kumi nzima zoezi hili la kuhesabu namba kukamilika.
Baada ya kukamilika yule askari akafoka tena.
"Haya anzia hapa mbele kwenda nyuma"
Tukaanza tena kuhesabu namba safari hii kuanzia sisi tuliokaa mbele na kushia kwa wale waliokaa nyuma.
Mara zote mbili hesabu iliyopatikana ilikuwa ni 314.
"Bado wafungwa wawili hawapo" afande mwingine aliyekuwa ameshika daftari na kalamu akaongea.
"Umejumlisha vizuri walioko nje shambani"
"Nimefanya hivyo mkuu, walioko shamba ni 22 nikiwajumlisha hapa bado watu wawili hawapo hapa" akaongea yule mwenye peni na karatasi.
"Nani hayupo hapa" yule askari mwingine akajliza kitemi kwa sauti ya juu.
Watu wakaanza kugeuka geuka kuangaliana usoni.
"Kaburu hayupo!!" Kuna mfungwa akaongea kwa sauti..
"Yes mjumlishe na Kaburu yuko ofisini" yule askari akaongea akiwa kama amekumbuka kitu cha wazi kabis walichokisahau Kumjumlisha Kaburu aliyeko ofisini.
"Nani mwingine" akauliza tena.
Watu wakaanza kugeukiana na kuaangaliana.
"Daudi hayupo" kuna mfungwa akapayuka.
"Daudi yupi?" Yule askari akauliza kwa shauku.
"Sinyorita" Yule mfungwa akapayuka tena.
Wale maaskari wakashtuka kidogo na kuangaliana.
"Kwahiyo Kaburu na Sinyorita hawapo hapa" yule askari akaongea kwa hasira.
Wakaangaliana tena na maaskari wenzake. Kisha maaskari wawili wakaondoka kutoka pale yard na kuelekea kule eneo la jiko.
Yard ilikuwa kimya kabisa. Godi alikuwa anageuka na kuniangalia kisha anatabasamu kichini chini.
Tulikaa tukiwa tumetulia vile karibia robo saa nzima.
Mara tukaona watu kadhaa wameongozana wanaingia Yard.
Mbele alikuwa ametangulia mkuu wa gereza na pembeni yake kulikwa na maaskari wawili. Nyuma yao walikuwa ni Kaburu na Sinyorita ambao nyuma yao nao kulikuwa na maaskari wengine wawili.
Walipoingia pale yard wafungwa wote na mahabusu tukashikwa na mshangao mkubwa hatukuamini tulichokuwa tunakiona.
Au niseme wengine wote isipokuwa mimi walishikwa na mshangao.
Sinyorita alikuwa ameletwa yuko uchi wa mnyama ameshikilia nguo mkononi.
Walipofika pale mbele maaskari wote wakapiga saluti, kisha wakasogea pembeni kumpa nafasi mkuu wa gereza azungumze.
Kaburu na Sinyorita wakapiga magoti baada ya kukuta wenzao wengine akina Blaki waliokuwa pale mbele wamepiga magoti.
"Simameni hivyo hivyo msipige magoti nataka wenzenu wote wawaone mashetani nyinyi" Mkuu wa gereza akaongea kwa hasira.
"Naona mmeanza kutupanda kichwani sasa!" Akaongea mkuu wa gereza huku anatuangalia wafungwa wote na mahabusu.
"Yani mnaingiza taharuki kwenye gereza langu kwa kugombea misokoto ya bangi??" Akaongea kwa hasira na kutoa macho.
"Naona mmejisahau kuwa mko gerezani labda tumewapa Uhuru sana ndio maana. Sasa kesho asubuhi hakutakuwa na mazoezi badala yake tutafanya msako wa selo kwa sell, ole wako tukukuta na bangi, ole wako tukukute na sigara, ole wako tukukute na ugoro, ole wako tukukute na kisu, ole wako tukukute na begi limejaa Nguo!! Nasema ole wako tukukute na kitu chochote tulichokikataza." Mkuu wa gereza akahutubia kwa hasira.
"Na wewe Blaki umeshakuwa kero humu gerezani, kuanzia kesho akuweka solo mpaka utakapobadilika" akaongea huku anamuangalia Blaki na wapambe wake.
Baadae nilikuja kuelewa kuwa aliposema anamuweka 'Solo' alimaanisha kuwa atamuweka kwenye "solitary confinement". Ni ile sehemu yenye selo zilizojitenga ambazo Godi alinieleza kuwa huwa wanawekwa mahabusu na wafungwa 'maalum'.
"Sasa kwa kuwa nyinyi mnajifanya vidume, mimi nitawaonyesha ni kidume zaidi yenu wapumbavu nyinyi" akaongea huku anatuangalia wafungwa wote na mahabusu.
"Kaburu nilikupa heshima sana ndio maana nikakupangia kazi ofisini mwangu! Lakini unathubutu kuingiza mashetank wenzako ofisini kwangu ili mfirane!! Ofisi yangu mimi, ofisi yangu mnatumia kufirana, ofisi yangu mimi.!!" Mkuu wa gereza akaongea kwa hasira na hisia huku anapiga piga kifua.
"Afande nataka hawa mashetani wote! Kuanzia hawa waliokuwa wanafirana, na hawa waliokuwa wanagombea bangi.. Nataka muwapeleke ofisini kule mpige virungu mpaka wajute kuzaliwa! Mkimaliza hawa mbwa Blaki na wenzake wafungieni 'solo' kule na huyu firauni Kaburu nataka kuanzia jumatatu aanze kwenda shamba simuhitaji tena ofisini kwangu" akaendelea kuongea kwa hasira.
Nikajikuta natabasamu niliposikia maneno "simuhitaji tena ofisini kwangu"!! Nikajipongeza, 'goal achieved' nikajisemea kimoyo moyo.
"Saa ngapi hapo" akamuuliza askari wa pembeni yake.
"Saa nane na robo Mzee" askari akajibu kwa heshima.
"Sasa nadhani mlikuwa mnakula, lakini kutokana na ujinga huu mlio ufanya nahairisha kila mlichokuwa mnakifanya na mtafungiwa selo sasa hivi saa nane mlale badala ya saa kumi" akaongea kwa hasira kubwa na kumalizia, "vijana msitake kunijaribu, mimi sijaribiwi! Mtaiona jela chungu"
Akamaliza na kuanza kuondoka.
"Kaba seloooo" askari mmoja akapayuka kitemi.
Wote tukaanza kuinuka kwa unyonge tumelowa kama tumemwagiwa maji ya barafu.
Tukaongozana na Godi kuelekea selo yetu namba mbili kubwa.
"Kumamae wewe msenge ni kichwa!! Saluti" akaninongoneza kwa kufurahi.
"Kwahiyo nini kifuatacho ITV??" Akaniliza kwa shauku.
"Well, tumeshafanikiwa kumuondoa ofisini kwa mkuu wa gereza! Lakini umesikia pale ameamuru kuwa jumatatu aanze kupelekwa shamba. Maana yake ni kwamba tuna siku ya kesho ijumaa, jumamosi na jumapili!! Tuna siku tatu tu kuhakikisha tumeongea nae na ametupatia taarifa tunayohitaji" nikaongea kwa sauti ya chini huku tunatembea kuelekea selo.
"Woooww!! Daaahh nilikuwa nakuchukulia poa sana.. Kumbeee daaahh! Sakuti aisee!" Akaongea kwa utani huku ananipigia saluti.
Nikatabasamu tu. Sikusema chochote.
Siku hii ya pili imeisha kwa mafanikio. Nina siku tatu mbele yangu kuhakikisha nakamilisha 'mission' iliyonileta humu.
Nikajipa moyo. 'Inyeshe mvua, au liwake jua' lazima kieleweke.
TUKUTANE IJUMAA KWENYE EPISODE 15..
The Bold