Mdomo bakuli
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 3,442
- 7,020
Big up mkuu, Nifah anajua kuchagua
jnne ndio ataweka kuwa mvumilivuJamani ya 13 baado tu
Kaka kwema uko kuna wengine tupo njee ya nchi bongo hatuna watu tufanyie hisani niunge kwenye group niwe napata vipepeo weusi nikija mwenzi 7 ntakupa mihela yko nomb yngu +27784696692VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034
EPISODE 12
Nikatembea mpaka kufika pale alipokuwa amekaa Kaburu lakini nikasimama nyuma yake. Nilikuwa na uhakika kabisa kuwa alikuwa anajua kuwa kuna mtu amesimama nyuma yake lakini hakugeuka aliendelea tu kunywa uji.
"Sijawahi kuona mtu mpumbavu kama wewe!" Kaburu akaongea huku ana simama na kunigeukia.
"Toka kuzaliwa kwangu, nimeona watu wajinga na wapumbavu! Lakini hao wote hawafikii upumbavu wako kijana" akaongea huku akiwa amesimama na kuniangalia usoni.
"Shikamoo mkuu" nikamuamkia.
"Sikudhani kama utarudi tena toka nikupe lile onyo siku ile kwamba unahatarisha usalama wako na usalama wangu kwa kuja kuongea na mimi! Lakini kudhihirisha ulivyo mpumbavu umejileta jela makusudi uendelee kunifuata fuata" akaongea kwa hasira bado akiwa ananiangalia usoni.
"Sikuwa na jinsi.! Sina chaguo lingine zaidi ya kufahamu ukweli kuhusu The Board" nikaongea kwa kujitutumua na kujiamini.
"Na kinachokufanya uhisi kuwa nitakwambia hicho unachokitaka ni mini?" Akaniuliza huku anatabasamu kwa dharau.
"Trust me! Utanieleza ninachokitaka utake usitake" nikaongea kwa kujiamini kabisa. Nimeishi uswahilini maisha yangu yote utotoni. Na moja ya vitu muhimu nilivyojifunza uswahilini ni kutokumuonyesha adui hofu yako na kujua namna ya kupiga mikwara.
Nikamuona kaburu alivyoduwaa ghafla baada ya kuona kujiamini kwangu.
"Ok! Tuseme kwa mazingaombwe yako ukawa na njia ya kunifanya nikupe hiyo taarifa! Nakuhakikishia kuwa utakuwa ushafukiwa kaburini siku nyingi kabla ya kuifanyia Nazi" akaongea akiwa na uhakika usoni wa anachokisema.
"Unadhani unavyoua watu ndio suluhisho la wewe kuwa Salama?" Nikamuuliza kwa hasira.
"Sio mimi nitakaye kuua kijana! Humu ndani kuna watu wa hao unaowasema,The Board na nina hakika kuna watu wa Usalama wa Taifa. Hao ndio watakaoshughulika na wewe" akaongea huku anageuka mkono wake wa kushoto kuna mahabusu akawa anawaangalia.
Nikageuka kuangalia kule mkono wa kushoto. Kulikuwa na mahabusu watatu wamesimama wanatufuatilia maongezo yetu.
Nikagundua kuwa wawili kati yao walikuwa ni moja katika wale mahabusu kadhaa jana waliokuwa wamekaa nyuma kabisa ya yard 'wakituchora' mimi na Godi jana wakati ambapo Godi alikuwa ananionyesha mazingira ya humu ndani.
Hawa wajamaa walikuwa na miili iliyojengeka kiasi na mmoja wao alikuwa amevaa nguo za kifungwa za rangi ya chngwa na mwingine alivaa nguo za kawaida ikimaanisha alikuwa mahabusu kama mimi.
Nikageuka kumuangalia tena Kaburu. Alikuwa ananiangalia huku anatabasamu kisha akaanza kutikisa kichwa kama ananisikitikia.
"Umebakisha siku chache sana za kuishi mdogo wangu" akaongea huku anaanza kuondoka pale yard.
Nikageuka tena kuwaangalia wale mahabusu waliokuwa wanafuatilia maongezi yetu muda wote. Bado walikuwa wamesimama wananiangalia huku usoni wakiwa wako serious haswa.
Kaburu alikuwa ameshaondoka kutoka yard hivyo na mimi nikageuka na kuondoka kwenda yard namba mbili.
Nilipofika yard nikaangaza macho huku na huko lakini sikumuona Godi.
Nikasogea na kwenda kukaa chini karibu na muembe nikiwaza mambo kadhaa.
Kitu cha kwanza nilichokuwa nakifikiria sana ilikuwa ni taarifa niliyoambiwa na Godi na baadae Kaburu mwenyewe kuithibitisha kwamba watu wengi walioingia humu jela na kuanza kumfuata fuata wamekuwa wakiuwawa.
Moja kwa moja nikaamini kuwa lazima The Board watakuwa wanahusika na mauaji hayo, yani kwamba wamepandikiza watu humu gerezani kufuatilia nyendo za Kaburu na wakiona kuna mtu anakuwa naye na ukaribu sana basi wanammaliza haraka.
Hii ilinifanya nielewe kwamba kuna taarifa ambazo Kaburu alikuwa nazo na The Board walikuwa wanahofia mtu mwingine yeyeote asizifahamu.
Lakini swali kubwa zaidi nililokuwa najiuliza kichwani ni kwanini The Board wasimmalize Kaburu mwenyewe ili kuondoa kabisa hofu yao ya taarifa kuvuja?? Kwanini walimuacha aishi kama wanahofia kuvujisha taarifa zao?
Moja kwa moja nikaanza kuhisi kwamba labda pengine kuna taarifa nyeti sana za The Board na mtu pekee ambaye anazo hizo taarifa ni Kaburu ndio maana wanahofia kumuua. Nilikuwa na hakika kabisa lazima kutakuwa na siri nzito kuhusu The Board ambayo Kaburu alikuwa anaitumia kama 'insurance' kumuwezesha kuepuka kumalizwa na The Board.
Kitu kingine nilichojiuliza na ambacho nilikuwa natakiwa kukifahamu haraka sana ni kuhusu anakoshinda Kaburu humu gerezani. Nikikumbuka kauli ya Godi alinieleza kwamba muda pekee ninaoweza kumuona Kaburu ulikuwa ni muda wa kunywa uji na baada ya hapo sitoweza kumuona mpaka muda wa 'kaba selo'.
Niko humu gerezani ili niweze kumshawishi Kaburu anipe taarifa kuhusu The Board, na ili niweze kumshawishi ninatakiwa niwe na muda wa kutosha wa kuongea naye. Kwahiyo yanipasa kufahamu anakoshinda mida wa mchana na nione ni namna gani nitaweza kwenda hapo alipo na kuongea naye.
Nikiwa bado nimekaa pale chini ya mwembe nikiwaza na kutafakari, nikamuona mahabusu ambaye hapo baadae nilikuja kufahamu jina lake la utani humu gerezani wanamuita Sinyorita, alikuwa anatembea kuja pale nilipokuwa nimekaa.
Huyu kijana alikuwa na umri wa kama miaia 24 hivi na alikuwa na 'swaga' Fulani hivi kama mwanamke.
Kwanza kabisa alikuwa na umbo fulani hivi namba 8 ambalo mtoto wa kiume hapaswi kuwa nalo na kwa jinsi alivyokuwa mshenzi alikuwa anavaa vibukta vifupi vinavyombana.
Pia alikuwa 'amejaaliwa' rangi nyeupe pee kabisa mpaka kwenye visigino.
Siku za huko mbeleni nilikuja kufahamu kuwa Sinyorita alikuwa moja ya 'makaka poa' wa 'hadhi ya juu' humu gerezani. Yani kwamba humu gerezani kulikuwa na mahanisi wengi tu ambao kila mmoja wao alikuwa na hadhi yake. Kuna wale ambao walikuwa na hadhi ya kufanana na malaya wa uwanja wa fisi. Kulikuwa na wengine wenye hadhi ya kama machangu wanajiuza barabarani sinza. Kukikuwa na wengine wenye hadhi ya kufanana na wale machangu huku mtaani wa "laki moja kwa goli"!
Alafu kulikuwa na mahanisi first class wenye hadhi kama ya wale wanajiuza Serena Hotel kwa mfano. Na Sinyorita humu gerezani alikuwa na hadhi hiyo. Alikuwa ni pumziko la 'madoni' wa gereza.
Moja ya vitu nilivyokuja kuvigundua humu gerezani tofauti na stori za mitaani ni kwamba watu wanaofirw* humu, wengi wao wanafanya hivyo kwa hiari yao kabisa. Yani kiasi fulani ni kama ilivyo mtaani, kuna watu humu gerezani wana hela kweli kweli na wanatumia hizo hela kushawishi wafungwa wenzao au mahabusu na kuwageuza wake zao.
Japokuwa kulikuwa na matukio machache ya watu kubakwa au kufirw* kwa lazima, lakini hiyo ilikuwa ni moja kati ya makosa ambayo ukiyatenda humu jela na likifika kwa Askari magereza, basi wewe mbakaji utatamani ardhi ipasuke ukimbilie jehanum.
Wenyewe maaskari magereza walikuwa na msemo wao kuwa "jela ikitulia, ikiwa na amani na sisi kazi yetu inakuwa rahisi na tunafurahi kuifanya."
Hivyo ishu ya kubaka ilikuwa moja ya vitu vinavyokemewa vikali humu ndani, lakini hawakuwa na time wala kujali wale wanaofiran* kwa hiari yao.
Kwahiyo, japokuwa bado gerezani ni sehemu ya hatari, iliyojaa uonevu na ukatili ila ikitokea mtu ameenda jela na ukasikia wenzake wamemgeuza mke wao, ujue kuna asilimia kubwa alifirw* kwa hiari yake kutokana na tamaa ya kutaka kuishi jela kama yuko uraiani kwa kula vizuri na kulala vizuri.
Sinyorita alitembea mpaka pale nilipokuwa nimekaa, alafu akasimama mbele yangu. Nikainua shingo na kumuangalia.
"Mambo!" Akanisalimia kwa sauti kama anabana pua.
Sikuitikia, nikaendelea tu kumwangalia.
"Naweza kukaa hapa?" Akaniuliza tena bado akiongea kikike kike.
Sikumjibu kitu, lakini akakaa pale pale nilipokaa mimi akiwa amenisogelea kabisa.
"Mambo vipi?" Akarudia tena kunisalimia kikike kike baada ya kukaa.
Kuna mda huwa mtu anafanya kitu cha Ainu kiasi kwamba wewe wa pembeni yake unajisikia aibu kuhusu anachokifanya kuliko hata yeye mwenyewe. Hivyo ndivyo nilivyokuwa najisikia muda huu.
"Unataka nini?" Nikamjibu kwa ukali na kukereka.
"Ai jamani kwani ugomvi" akaendelea kuongea kwa deko.
"Nimekuuliza unataka nini?" Safari hii nikamjibu huku nimekunja uso namtazama usoni mwake.
"Heee! Basi bwana yaishe, nimetumwa na blaki anakuita"
"Blaki ndio nani?"
"Yule pale!"
Akanionyesha kule nyuma ya yard mahali ambapo kuna ule uchochoro wa kutokea yard namba moja.
Alikuwa ni mmoja wa wale wajamaa walikuwa watuangalia mimi na Kaburu tulipokuwa tunaongea. Moyo wangu ukapasuka kwa hofu.
"Mwambie niko bize siwezi kwenda" nikamjibu kwa mkato.
"Nyoko zako uko bize na nini wakati uko jela humu! Hebu waulize mbwa wenzako nini kitakukuta Blaki akikuita na ukikataa kwenda" Sinyorita akaongea kama vile wanawake wanasutana.
"Anataka nini?" Nikauliza tena kwa kifupi.
"Hebu nenda bwana utajua huko huko anachokuitia msyuuuuuuu" akaongea na kumalizia na kusonya.
Baada ya hapo akainuka na kuanza kuondoka huku anatembea kwa madaha kama kawaida yake.
Nikatazama kule nyuma ya yard kwenye uwazi wa uchochoro, Blaki alikuwa amesimama ananiangalia.
Kiasi fulani nilishikwa na hofu lakininkwa upande mwingine nilishikwa na moyo wa ushujaa. Kwamba tayari nimeshaingia jela, sipaswi kuogopa chochote humu ndani. Maji nimeshayavulia nguo, sharti niyaoge.
Nikainuka na kuanza kueleke kule alipo Blaki. Nilipofika pale akasogea kidogo kama ananipisha nipite. Nikapita.
Baada ya kuingia pale uchochoroni nikakuta kuwa wako watu watatu. Blaki, yule mwenzake anayevaa nguo za kifungwa na mahabusu mwingine.
Nipoingia tu kwenye uchochoro, mwenzake mmoja akakaa kwenye uwazi wa kutokea uchochoroni mkono wa kulia mwingine akakaa mkono wa kishoto na Blaki mwenuewe akasimaa mbele yangu kama hatua tatu hivi kutoka pale nilipo.
Tukabaki tunaangaliana tumekaziana macho kwa takribani dakika nzima. Nikaanza kukumbuka stori za Godi aliponileta hapa asubuhi kuhusu watu waliouwawa hapa, pia nikakumbuka kauli ya Kaburu aliposema "umebakiza siku chache sana za kuishi". Nikahisi hiki ndicho nilichoitiwa hapa.
Jambo la ajabu ni kwamba, japokuwa presha ilikuwa imenipanda na jasho lilianza kunitoka lakini sikuwa na hofu kabisa moyoni mwangu badala yake nilijisikia hasira ya kiwango cha juu.
"Dogo una dakika moja kunieleza ni nini ulichofiata huku jela" Blaki akaongea huku amefura.
"Kabla sijajieleza chochote kwanza nadhani ujieleze wewe kwanza, wewe nani na unataka nini?" Na mimi 'nikamdindia' huku nimefura.
"Narudia tena una dakika moja kujieleza ulichofuata huku jela" Blaki akaongea huku
Nikaona ngoja nimjaribu.
"Niko jela kwasababu kuna mtu nimemuibia na nimekosa dhamana, unaweza kunieleza unataka nini kuniuliza maswali ya ajabu ajabu?"
Ghafla nikamuona Blaki amefura zaidi kwa hasira. Akaingiza mkono mfukoni. Akatoa kisu. Nikasikia roho imepasuka kwa hofu, pwaaaaaaaa. Jasho likaanza kunitirika.
Gerezani hawaruhusu wafungwa kuwa na visu, kwahiyo wanachokifanya wanachukua kijiko na kukichonga kwa kukisugua sana mpaka kinatengeneza ncha kali kama kisu na upande mwingine wanafunga na mpira wa kuvutika ili kutengeneza kama mpini hivi.
Hicho ndio aina ya kisu ambacho Blaki alikuwa amekitoa kutoka mfukoni.
Akakishikilia kisu mkononi na kuanza kunisogelea taratibu. Mapigo yangu ya moyo yakaongezeka kwa kasi ambayo nikahisi moyo unataka kuchomoka.
"Wewe fala nakuuliza mara ya mwisho! Umefata nini jela??" Blaki akafoka kwa hasira mpaka jasho lilianza kumtoka. Pepo la uuaji lilikuwa limeshampanda kichwani.
Nikaanza kurudi nyuma taratibu.
"Fikiria kwa makini hicho kitu unachotaka kufanya, mimi sio huyo mtu mnayemfikiria" nikajitetea huku narudi nyuma mpaka nikafika ukutani. Blaki tayari alikuwa mbele yangu na "hasira" ilikuwa imempanda mpaka jasho linamtoka.
Ghafla nikakumbuka ile karatasi niliyopewa na Baba bite kuwa itanisaidia kusurvive humu gerezani. Jana usiku niliisoma lakini sikuielewa kwa asilimia zote lakini nakumbuka kabisa jina la "Blaki" limetajwa mara kadhaa mle ndani kwenye maelezo ya Baba Bite.
Kila nilipojitahidi kukumbuka haraka haraka kujua ni nini kilichoongelewa kuhusu Blaki, kumbukumbu ilikuwa haiji. Nadhani ni kutokana na kuwa katika paniki mda huu na pia kwakuwa sikuyaelewa Yale maelezo toka jana wakati nayasoma.
Nikanyoosha mkono wangu mpaka kwenye mifuko ya suruali ili nitoe hicho kikaratasi ili nikisome au walau nimuonyeshe Blaki. Sidhani kama nimewahi kuwa 'desperate' kiasi hiki kwenye maisha yangu kama jinsi ambavyo nilikuwa najisikia muda huu.
Nikanyoosha mkono na kupapasa mifuko ya suruali, lakini jambo la ajabu ni kuwa ile karatasi haikuwepo. 'What the ****??', nikajikuta najiuliza kichwani. Karatasi imeenda wapi wakati nakumbuka kabisa baada ya kuisoma niliiweka mfukoni na hata asubuhi milipoamka bado nilikuwa nayo mfukoni.
Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. Huu msemo haukuwa tu msemo, bali kwa wakati huu ndio ulikuwa uhalisia uliopo mbele yangu.
Nikajiuliza labda nipigane nao? Lakini nikaona uhalisia kabisa, kisu kilichopo mkononi mwa Blaki kitakuwa kimeshafika tumboni mwangu kabla hata sijarusha ngumi ya kwanza.
Macho yangu yakaanza kuangalia pale juu kwenye damu iliyovilia ambayo alinionyesha Godi asubuhi, kisha macho yakahamia kuangalia pale chini kwenye kona kwenye michirizi ya damu iliyovilia ambayo pia Godi alinionyesha asubuhi. Nikahisi kama moyo wangu umeacha kudunda.
Nikamuona Blaki anageuza kisu mkononi na kukishikilia vizuri na kwa nguvu zake zote! Alikuwa amefura kwa hasira. Jasho linamtiririka, pepo wa kuua amempanda.!!
Nikajua kinachofuata! Nikafumba macho kwa hasira, uchungu na hofu.!!
Itaendelea Jumanne.. Episode 13
Join my exclusive whattsapp group kusoma makala na simulizi kila siku.. 0718 096 811 (kuna subscription fee)
The Bold

FUNGUA KWA KUANGALIA NAMBA ZA POST HUSIKAJamani Msaada Tutani nilisoma nikaishia Episode ya 9 tu zingine hazifunguki
Huruma yenu kwangu
Jamani Msaada Tutani nilisoma nikaishia Episode ya 9 tu zingine hazifunguki
Huruma yenu kwangu
Pamoja sana comrade..Daah mwana umetia sana alafu ni tamu balaaa
Asante sana kiongozi
Kesho mkuu..Sehemu ya 13.. Nataka kujua alitokaje man kwa black... Mkuu weka hiyo 13 bac
Hahahah! Shukrani mkuu..Big up mkuu, Nifah anajua kuchagua
Tazama whatsapp mkuu.. Tayari nimekuunganisha kwenye groupKaka kwema uko kuna wengine tupo njee ya nchi bongo hatuna watu tufanyie hisani niunge kwenye group niwe napata vipepeo weusi nikija mwenzi 7 ntakupa mihela yko nomb yngu +27784696692
EPISODE 9 IPO KWENYE POST YA 3116
EPISODE 10 IPO KWENYE POST YA 3176
EPISODE 11 IPO KWENYE POST YA 3212
EPISODE 12 IPO KWENYE POST YA 3262
Sawa mkuu.. Usijali baadae usiku nikikaa chini nikitulia nitafanya mambo link ziwepo pale juuMkuu Ombi kwako niwekee Link mkuu natumia sim
Maelekezo ya Awali yamegoma Mkuu
Tusaidiane ktk hili walau nami niipate Dozi hio maana ni hoi na Maradhi ya Vipepeo weusi
Sawa mkuu.. Usijali baadae usiku nikikaa chini nikitulia nitafanya mambo link ziwepo pale juu