Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)




=========

Muhimu: Simulizi hii inaakisi namna ambavyo kila mmoja wetu anaguswa na mambo ya siri yanayofanywa na watu wenye nguvu na ushawishi. Pia simulizi hii inajitahidi kugusia ulimwengu wa hatari wa "conspiracies" na Ujasusi. Pia msimuliaji anaonyesha namna ambavyo nguvu ya mapenzi inaweza kuokoa nafsi ya mtu na kumfanya kuwa bora kwa wanomzunguka na nchi yake.

Kumbuka simulizi hii ni ya kutunga. Wahusika, matukio na visa vyote vinavyosimuliwa ni vya kufikirika, hivyo mfanano wowote na mtu katika maisha halisi ni bahati mbaya.

Tafadhali si ruhusa kutumia andishi hili mahali popote pasipo ruhusa ya muandishi.

VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034
"Nipe mahali pa kusimama na ndoano mkononi mwangu, naweza nikainua dunia." - The Bold


EPISODE 1

MIAKA 3 ILIYOPITA, Dar es Salaam.
Nimezaliwa miaka 29, miezi minne, wiki mbili, siku tano, masaa 18, na dakika 40 zilizopita. Jina langu naitwa Rweyemamu Charles Kajuna, lakini marafiki na wanafamilia hupendelea kuniita kwa kifupi, Ray.

Nakumbuka miaka mitatu iliyopita. Siku ya kwanza waliponifuata. Siku ya kwanza nilipo fahamu kuwa wanataka niwe mmoja wao au angalau yafaa kusema niwe kibaraka wao.

Ilikuwa siku alhamisi, jioni yapata majira ya saa kumi na mbili kasoro, walifika wakiwa ndani ya gari nyeusi aina ya Land Ceuiser V8. Nilikuwa nimelala kitandani lakini niliamka baada ya kumsikia Shangazi akiongea nao nje.

Nyumba yetu ilikuwa pembezoni mwa barabara ya mtaa katika maeneo ya Mwembe Chai, na nyumba yetu haikuwa na uzio. Hivyo nilivyo amka kutoka kitandani na kuchungulia dirishani niliweza kuwaona wageni waliokuwa wanaongea na Shangazi.

Walikuwa wamepaki gari yao nyeusi ng'ambo ya barabara. Watu wawili walishuka kutoka kwenye gari na kuja mpaka mlangoni mwa nyumba yetu. Wakagonga mlango na shangazi akatoka kuwasikiliza.

Haya yote nilikuwa nayaona kupitia dirishani. Kitu cha kwanza kilichoisumbua roho yangu baada ya kuwaona watu hawa ilikuwa ni gari waliyokuja nayo. Kichwani mwangu nilishawishika kabisa gari hii naifahamu na nimewahi kuiona lakini kumbukumbu ilikuwa haiji ni wapi niliiona au naifahamu vipi.

Nikahisi labda kuna mahusiano na bahasha niliyoipokea wiki mbili zilizopita, nikiwa ofisini Morogoro ililetwa na mtoto anayeuza machungwa akidai kuwa amepewa na mtu nje ya jengo letu la ofisi na akaambiwa aje amkabidhi mtu anayeitwa Ray.

Ndani ya bahasha hii nilikuta simu na kikaratasi kimeandikwa "speed dial 1", ikimaanisha nibonyeze kwa muda kitufe namba moja cha simu ili simu ipige. Suala hili nilikuwa sijalifanya mpaka leo hii na sikuwa na mpango wa kulifanya kwani ni uchizi kutii maagizo ambayo hata haufahamu yaliko toka.

Hisia zangu zikaendelea kufikiri labda watu hawa wana uhusiano na bahasha ile. Lakini pia roho yangu ilizidi kusumbuka kila nilipoiangalia ile gari waliyokuja nayo. Kadiri nilovyoiangalia ndivyo nilivyozidi kushawishika kuwa naifahamu, lakini bahati mbaya sikuweza kukumbuka niliiona wapi.

Nikiwa bado niko dirishani nachungulia kuangalia kinachoendelea mara shangazi akaniita kutokea nje, "Ray.!!"
"Naaaam.!" Nikamuitikia huku nikisogea kwenye dirisha sikuataka wajue kuwa nilikuwa nawachungulia mda wote huu.
"Kuna wageni wako nje hapa"
"Nakuja" nikajibu huku navaa pensi mda wote huu nilikuwa nimevaa bukta ya kulalia na singlendi.

Kabla sijatoka chumbani kwangu, nikachukua begi la mgongoni ambalo lilikuwa pembeni ya kitanda na kufungua zipu kisha nikatoa bahasha pamoja na simu nilivyovipokea wiki mbili zilizopita. Nikaiweka simu ndani ya bahasha na kuikunja ili niweze kuishika mkononi.

Baada ya kufungua mlango na kutoka nikiwa sebuleni shangazi naye alikuwa ndio anaingia kutoka nje. Nikamuuliza "kwanini hujawakaribisha ndani wageni".

"Wamesema hawakai wana haraka" akanijibu kwa ufupi huku akielekea chumbani kwake. Nikafungua mlango nikatoka nje. Wageni wangu walikuwa ni watu wawili, mmoja alikuwa ni muhindi, mtu mzima kiasi mwenye umri kati ta miaka 40 hadi 42 na mwenzake alikuwa ni mswahili na kijana zaidi kwa makadirio ya umri kuanzia miaka 34 hadi 36.

Yule muhindi alikuwa amevalia shati, suruali ya jinzi na viatu vyeusi, na yule mwenzake mswahili alikuwa amevalia suti ya kaunda. Jamaa huyu mswahili alikuwa na mwili uliojengeka kimazoezi kiasi kwamba hata suti ilikuwa imemkaa sawia. Kwa mtazamo wa haraka nikahisi kwamba jamaa huyu mswahili alikuwa ni mlinzi binafsi wa huyu muhindi.

"Hujambo Ray?" Yule muhindi alisalimia huku anatabasamu mara tu nilipofika walipokuwa wamesimama.
Sikutaka kuitikia salamu yao, nikaenda moja kwa moja kwenye hisia zangu "mmefuata mzigo wenu?" Nikawauliza huku nawaonyesha bahasha niliyotoka nayo ndani.

Yule muhindi akatoa tabasamu kubwa na kuniuliza "nini kinachokufanya uhisi huo ni mzigo wetu na ndicho kilichotuleta?".
"Kama sio mzigo wenu niambieni niurudishe ndani alafu nije niwasikilize hicho kilicho waleta?" Nikaongea kwa kujiamini huku nimemkazia macho yule muhindi.

Akaichukua bahasha kutoka mkononi mwangu kisha akampa yule mswahili aishike, kisha akaniuliza kwa kifupi tu "kwa nini haukupiga simu?".
"Mimi sio mpumbavu nifuate maelekezo nipige simu wakati hata sijui hiyo bahasha ilikotoka!" Nikamjibu haraka huku nikijitahidi kuonyesha kujiamini. Yule muhindi akatabasamu tena huku akitingisha kichwa "ndio maana tumeamua tuje ili tuongee kwa mdomo, relax" akaongea yule muhindi.

"Siwezi kurelax wakati siwafahamu hata nyinyi ni kina nani, mnatokea wapi na mnataka nini." Nikajitutumua zaidi. Rohoni nilijisikia raha kwasababu nilijihisi kama nimeshika usukani wa haya maongezi.
"ooohh usijali, mimi naitwa Sultan na mwenzangu anaitwa Kevin"

Nikamkazia macho yule muhindi huku, na yeye akinikodolea macho kana kwamba anajaribu kusoma ninachofikiria.
"Mmejitambulisha wawili tu, kwanini hamjamtambukisha mtu wa tatu mliyekuja naye?" Nikamuuliza huku nimemkazia macho kwa kujiamini.
Yule muhindi Sultan akageuka wakatazamana na yule mswahili Kevin kisha akanitizama mimi, "Ray mtu gani wa tatu unamuongelea"

Sikupepesa macho wala kutazama pembeni, nikaendelea kumkazia macho na nikasogea hatua moja mbele kuelekea aliposimama Sultan. Kisha nikamuangalia moja kwa moja machoni kwa kujiamini na kumueleza, "nimewaona tangu mnakuja, mlipofika hapa na gari lenu wewe ulishuka kwenye gari kwa mlango wa kushoto wa mbele, na huyu mwenzio alishuka kutoka mlango wa nyuma, kwahiyo nina hakika kuna aliyekaa upande wa kulia mbele ambaye ndiye anayeendesha gari na hajashuka!"

Nilipowaambia maneno hayo wote macho yetu kwa pamoja yakaelekea kwenye gari lililokuwa wamepaki ng'ambo ya barabara. Gari ilikuwa na vioo vyeusi visivyoonyesha ndani. Kutokana na pale tulipokuwa tumesimama nikafanikiwa kuona namba za gari, T 228 CNL. Namba hizi zikazidi kuniaminisha hisia zangu kuwa gari hii naifahamu lakini bado kumbukumbu zangu haziji kuelewa gari ile niliwahi kuiona wapi.

Sultan akaangaliana na mwenzake Kevin kisha Kevin akatingisha kichwa kumpa kama ishara ya kukubali. Kisha akaniangalia mimi, "ok Ray, twende tukamsalimu".

Tukavuka barabara mpaka mahali walipopaki gari. Tulipofika Kevin akagonga kwa kidole kioo cha gari. Kioo kikafunguliwa taratibu na kilipofunguka chote mpaka chini, ndipo hapa nikaelewa kwanini kumbukumbu zangu ziliniambia kuwa nalifahamu hili gari.

Ndani ya gari kwenye siti ya dereva alikuwa ameketi Dr. Boniface Shirima.
Dr. Shirima ni mwalimu wangu wa Uchumi, au yafaa kusema alikuwa mwalimu wangu wa uchumi Chuo Kikuu cha Mzumbe kabla sijahairisha masomo miezi minne iliyopita ili niweze kujizatiti katika shughuli zangu za taasisi niliyoianzisha.

Nilimuangalia kwa mshangao kwa dakika kadhaa bila kuongea chochote.
Bumbuwazi langu lilikatishwa na Dr. Shirima ambaye alitabasamu na kunisalimu "hujambo Rweyemamu?"
"Shikamoo dokta, tafadhali nieleze kinachoendelea hapa sielewi" nikamjibu haraka haraka ndani ya nafsi yangu nikihisi kuwa labda walau sasa kuna mtu ninaye mfahamu anaweza kunieleza mini kinaendelea.

"Usijali Ray, kwanini haukupiga simu wiki mbili zote hizi" Dr. Shirima alikwepa swali langu na kuniuliza swali lingine.
"Dokta nimeshawaeleza hawa wenzako nimeletewa bahasha katika mazingira ya kutatanisha na ndani nakuta simu yenye kikaratsi chenye maelezo kwamba nipige simu!

Mimi sio mpuuzi kiasi hicho kufuata maelezo nisiyoyajua yalikotoka" nikamjibu Dr. Shirima, kwa mbali hasira zilinza kunishika kwenye nafsi. Nilianza kuchoshwa na hiki kilichokuwa kinachoendelea.

Kana kwamba Dr. Shirima alisoma akili yangu kwa haraka akendeleza maongezi, "Ray, hauna haja ya kuogopa wala kuwa na wasiwasi. Inawezekana haujafikiria hili lakini nchi hii inahitaji vijana wenye maono kama yako. Sisi ni marafiki, pia tuna pambana usiku na mchana kuhakikisha nchi inasonga mbele"

Kwa muda wa sekunde chache nikajaribu kutafsiri maneno yake kichwani ili niweze kuelewa kile ambacho labda alimaanisha na alikuwa hakitamki. Nikatafakari maneno kadhaa 'nchi inahitaji vijana wenye kama yako', 'tunapambana usiku na mchana kuhakikisha nchi inasonga mbele'!

Kiasi nikahisi kama nimemuelewa anachojaribu kukisema, hivyo nikataka nipate uhakika nikamuuliza, "Dokta kama mko na Idara ya Usalama wa Taifa, sidhani kama huu ndio utaratibu wa kurecruit watu ku…."
"No no no no hatuko na Usalama wa Taifa" Dr. Shirima alinikatsha kabla sijamalza nilichotaka kusema.
"Kama sio Usalama wa Taifa, nyinyi ni akina nani?" Nikamuuliza nikionyesha wazi mshangao wangu.

Dr. Shirima hakunijibu moja kwa moja akaingiza mkono kwenye begi dogo lilikuwa pembeni yake na kutoa simu inayofanana kabisa na ile niliyoletewa wiki mbili zilizopita niliyo wakabidhi Sultan na Kevin. Akanikabidhi simu na kunambia, "ni rahisi sana kukujibu sisi ni akina nani na kwanini tunakuhitaji, unachotakiwa kufanya, leo ikifika saa nne usiku bonyeza 'speed dial' namba 1"

Nikaipokea simu, nikaiangalia na kuigeuza geuza, nikijiuliza kichwani nimrudishie au nifanyeje?
"Na kama sitopiga simu hiyo saa nne?" Nikamuuliza.

Dr. Shirima akainamisha kichwa chini kama anafikiria kitu hivi kisha akaniangalia usoni, "kama hutopiga simu basi tutaachana nawe, lakini kabla haujafanya uamuzi huo kumbula kitu kimoja, nafahamu ni kiasi gani unapata tabu kutafuta funds za kuendesha program yako ya 'Sote Hub'! Tuna uwezo wa kukusaidia kwenye hilo, we can point you to the right direction upate hizo funds" Dr. Shirima alinieleza huku amenikazia macho, alijua wazi kabisa ni kiasi gani maneno haya yatakuwa yamenigusa moyoni.

Moyo wangu ulilipuka niliposikia anataja kuhusu 'kuniwezesha kupata funds kwa ajili ya 'Sote Hub'. Nikamuangalia usoni, Dr. Shirima akatabasamu, nilikuwa na uhakika kuwa amefahamu ni kiasi gani maneno aliyoyasema yamenigusa.

Akatabasamu, "Ray, fikiria kwa makini uamuzi ni wako, leo saa nne usiku fanya uamuzi sahihi." Akanieleza kwa kifupi huku akiwapa ishara wenzake Sultan na Kevin ambao mda wote walikuwa wamesimama kando yangu wakifuatilia mazungumzo yetu mimi ma Dr. Shayo. Wakapanda kwenye gari na mimi nikaanza kuondoka.

"Hey Ray.." Dokta aliniita, nilikuwa nataka kuvuka barabara na wao walikuwa wameshawasha gari. Nikageuka.
"Yes.." Nikamuitikia
"Msalimie cheupe!" Dr. Shirima akaniambia kwa utani huku anatabasamu. Na mimi nikashindwa kuzuia tabasamu usoni, nikamuitikia tu kwa kutingisha kichwa. Kichwani mwangu nikawaza "hawa washenzi wanafahamu vitu vingapi kuhusu mimi?". Nikatabasamu.
Wakawasha gari na kuondoka na mimi nikavuka barabara na kurejea nyumbani.

Nilipoingia ndani nikamkuta shngazi sebuleni na aliponiona tu akaanza kuniangalia kwa macho ya udadisi.
"Uko sawa?" Akaniukiza huku bado ananitazama kwa kijicho cha udadisi.
"Yeah shangazi, niko poa tu" nikamjibu kwa mkato huku nikielekea chumbani, sikutaka kubaki sebuleni hata dakika moja maana namfahamu shangazi yangu, ungeanza mfululizo wa maswali ambayo nilikuwa sitaki kuyajibu mda huu. Lazima angeanza kuniuliza Wale kina nani, wamesemaje, wanataka nini, unafahamiana nao vipi??
No, sikutaka kujibu maswali haya sasa, nikapitiliza mpaka chumbani kwangu na kufunga mlango.

Nilipofika chumbani nikajitupa kitandani kifudifudi, "aaaaaaarrrrggghh". Nikajiungurumia mwenyewe. Kichwa kilikuwa kinauzunguka nikitafakari mambo kadhaa kwa wakati mmoja.

Kitu kikubwa zaidi nilichokuwa nakiwaza na kikijirudia tena na tena akilini mwangu ilikuwa ni kauli ya D. Shirima, "tunaweza kukusaidia kupata funds kwaajili ya 'Sote Hub'". Nilitabasamu kila nilipofikiria kauli hii. Nikajiuliza ni kama ni kweli wana uwezo wa kufanya hivyo au ilikuwa ni mbinu ya kunipata na kuniingiza katika mipango yao waliyo nayo ambayo bado sikuijua mpaka muda huu.

Lakini jambo moja lilikuwa bayana, kwamba ndani ya mwezi mmoja ujao kama sitoweza kupata funds kwa ajili ya program ya Sote Hub sitakuwa na chaguo lingine zaidi ya kutii amri ya serikali ya kufunga ofisi.
Kila nilipofikiria dhana ya kufunga ofisi moyo wangu uliniuma na kulipuka. Nikikumbuka jinsi nilivyo vuja jasho na 'damu' mpaka kuanzisha Sote Hub, hakika kufunga ofisi itakuwa moja ya mapigo yatakayo niuma zaidi kwa maisha yangu yote.

Nikikumbuka jinsi safari ya kuanzisha Sote Hub ilivyo moyo wangu uliuma.
Safari hii ilianza mwaka mkoja uliopita nikiwa kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Mzumbe nikichukua shahada ya 'Economics and Project Planning'.

Nilipata wazo la kusaidia wanafunzi wenye talanta ya ujasiriamali. Nikaanzisha shindano la michanganuo ya biashara. Shindano hili nililiita 'Anzisha Business Competition'. Nikapata ufadhili kutoka kampuni ya Coca Cola.

Wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali Tanzania walituma michanganuo yao ya mawazo ya biashara. Kisha mimi pamoja na panel yangu akiwemo Dr. Shirima ambaye alikuwa ni mwalimu wangu wa uchumi na moja ya watu ninaowahusudu sana kitaaluma kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuona mambo kwa mtazamo mpana zaidi, tulichagua wanafunzi thelathini wenye mawazo bora zaidi kisha tukawashindanisha na kuwachuja na kubaki na wanafunzi kumi pekee ambao waliingia raundi ya mwisho ya fainali.

Fainali za shindano hili la Anzisha Business Competition zilirushwa kwenye televisheni ambapo washiriki walijieleza juu ya idea zao hizo na namna gani zitakavyo tekelezeka na kuleta faida za kiuchumi kwao na kuajiri vijana wengine.
Mshindi wa kwanza alipewa shilingi milioni kumi kutoka kampuni ya Coca Cola na mshindi wa pili alipatiwa milioni tano na watatu milioni mbili.

Miezi mitatu baadae tulipotembelea washindi hawa kufanya tahimini ya shindano tukakuta wote biashara zao walizianzisha lakini zimekufa.

Ndipo hapo katika kikao chetu cha majumuisho, nakumbuka Dr. Shirima akaeleza kuwa kumpatia mtu fedha pekee haisaidii bali anahitaji pia apatiwe mafunzo afahamu ulimwengu wa ujasiriamali ukoje, afundishwe kuhusu kutambua masoko, branding ya bidhaa yake na hata apate 'mentor' wa kumjenga kisaikolojia kuhusu biashara.

Ndipo hapa nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa pili, nikachukua hatua ya kuanzisha kituo cha kukuza biashara za vijana wenye ideas za tofauti na zenye uwezo wa Kukuwa kuwa kampuni kubwa.

Nilidhamiria kituo hiki kichukue vijana wenye mawazo bora kabisa ya kibiashara, kisha wapewe mafunzo kuhusu masoko na 'branding', watafutiwe mentors na mwishoni wapemwe mtaji wa kuanzisha biashara zao (seed capital).
Sisi kama kampuni tunaowasimamia tutachukua asilimia ndogo za hisa katika kampuni zao watakazo zianzisha.

Nikasajili kituo/kampuni hii kama 'Sote Hub' (SOTE - startup operations and trainings in Entrepreneurship).

Nikavuja jasho kuhangaika usiku na mchana kutafuta wafadhili wa kusaidia kuanzisha program hii. Baada ya miezi kadhaa ndipo nikafanikisha kuingia mkataba na Vodacom kudhamini hii programu. Ambapo kwa mwaka wa kwanza watatoa kiasi cha shilingi milioni 120 ambazo zitatolewa kwa awamu tatu, milioni 40 kila baada ya miezi minne.

Kwakuwa nilikuwa bado mwanafunzi chuo kikuu mzumbe, hivyo kituo hiki nikakianzisha Morogoro mjini na ofisi zake zilikuwa katika ghorofa la Hajram Mtaa wa Boma Road.
Ofisi na programu yenyewe zikazinduliwa kwa sherehe kubwa ya kufana mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya Morogoro. Ikarushwa katika taarifa za habari za televisheni mbali mbali na kutokea kwenye magazeti.

Vodacom wakanipa awamu ya kwanza ya funding, shilingi milioni 40. Utekelezaji wa programu ukaanza. Vijana kutoka kila pembe ya nchi wakatuma michanganuo ya biashara. Tukatumia takribani miezi miwili kupitia michanganuo yote na hatimae kupata vijana watano ambao ndio watakuwa chini ya programu hii kwa awamu hii ya kwanza.

Tukafanya press conference kuwatangaza. Vijana wakasafiri kutoka walipo wakaja Morogoro. Lengo lilikuwa ni 'kuwapiga msasa' kuhusu masuala ya kibiashara kwa miezi mitatu kisha mwishoni wanapatiwa seed capital ya milioni 10 kila mmoja.
Kutokana na kuwa bize sana kusimamia shugjuli za programu ikanibidi nihairishe masomo chuoni.

Vijana wakapatiwa mafunzo kwa mwezi wa kwanza. Ilipofikia mwanzoni mwa mwezi wa pili wa Programu, kukatokea mabadiliko makubwa ya kisera na uongozi ndani ya Vodacom. Uongozi mpya ukasitisha mikataba mingi ya udhamini ukiwepo mkataba wao na Sote Hub.

Hapa ndipo mushkeli ulipoanza katika maisha yangu. Nikahangaika usiku na mchana kutafuta sponsor mwingine wa kusaidia kuifikisha mwisho programu tuliyoianza lakini hakukuwa na mafanikio yoyote.

Sasa leo hii napata wageni tata, ambao ni dhahiri wana agenda ya siri na mimi na wanaahidi "tunaweza kukusaidi upate funding kwaajili ya Sote Hub".
Nilibaki na alama ya kuuliza kichwani. Niliwaza na kuwazua kwa masaa kadhaa. Nikaangalia saa kwenye simu ilionyesha ni saa tatu na dakika tano.

Nikachukua simu nimpigie Hasnat. Yes, Hasnat. Roho ya roho yangu. Mtu pekee ambaye nikisikia sauti yake hata niwe nimepaniki kiasi gani kila kitu kinakuwa shwari. Hasnat, mwanamke wa maisha yangu. Mwanamke niliyempenda na tunapendana tokea utotoni, na mwanamke pekee ambaye nataka niendelee kumpenda kwa maisha yangu yote duniani. Hasnat, mwanamke anayenifahamu pengine kuliko hata mimi ninavyojifahamu.

Nikachukua simu na kumpigia.

"Nambie kichwa" Sauti ya Hasnat iliongea kutoka upande wa pili wa simu. Taratibu taharuki yangu ikaanza kuyeyuka.
"Fesh tu, uko poa cheupe"
"Niko poa baba, nimechoka choka tu nilikuwa discussion ndio naingia room sahizi hapa wakati unapiga"
"Ok, skia cheupe! I have some bad news and worse news, what do you want first?"

"Hahahaha no i want the good news"
"OK! Kuna watu wamekuja home leo wanataka kunisaidia nipate funding kwaajili ya Sote Hub, the problem is I don't trust tem.."
"Are you kidding me, that's really a good news, kwanini unasema ni habari mbaya and kwanini huwatrust?"

"Sijui nisemeje but nadhani its better nichukulie hii positively, unakumbuka ile stori nilikwambia kwenye nchi za Asia wanaamini ukitembea barabarani kipepeo akikugusa hiyo inaashiria baraka, labda ndio vipepeo wenyewe hawa hahaha."

"Yeah but sio kila kipepeo ana rangi za kupendeza, vipepeo wengine ni vipepeo weusi majanga tupu hahahaha kidding honey, I think you should take the deal"
"Yeah kesho nitaenda kuonana nao"
"That's ma boi, good luck honey mi wacha nilale nimechoka kinyama yani"
"Poa! Usiku mwema cheupe, nakupenda"
"love you more kichwa"

Hasnat alikuwa na miujiza ya aina yake au labda ni kutokana na kumpenda kupindukia, kwani kusikia sauti yake tu kulifanya taharuki yote iliyokuwepo ndani yangu kuyeyuka. Lakini kuna maneno aliyoyatamka yaliendelea kujirudia kichwani mwangu na kufanya kuanza kurudiwa na hofu. "Sio kila kipepeo ana rangi ya kupendeza, kuna Vipepeo weusi pia". Maneno haya yalijirudia tena na tena kichwani.

Nikaangalia tena saa kwenye simu, ilikuwa ni saa nne na dakika mbili. Nikajipa moyo, "fu*k it! Wawe na rangi ya kupendeza au nyeusi, kipepeo ni kipepeo tu"
Nikachukua simu niliyopewa na Dr. Shirima na kubonyeza speed dial namba moja na kuweka sikioni.

"Halo!" Nikasubiri kusikia sauti kutoka upande wa pili.
"Una peni na karatasi hapo" sauti nzito upande wa pili wa simu iliongea bila hata kuitikia salamu yangu wala yeye kunisalimia. Haraka haraka nikafungua zipu kwenye begi la mgongoni lililokuwa pembeni mwa kitanda na kutoa kalamu.

"Ndio ninavyo" nikamjibu haraka haraka.
"Kesho saa kumi na nusu, PPF House, ghorofa ya saba, Unimax Marketing, jina lako ni Ally Hassan" ikaongea sauti upande wa pili wa simu bila nukta, haraka haraka.
"What, jina langu ni Rweyem….." Kabla sijamaliza kuongea simu ilikuwa imekata.

Nikaangalia taarifa nilizokuwa nandika kwenye kikaratasi nilipokuwa natajiwa na ile sauti kwenye simu. 'Saa kumi na nusu. PPF House. Ghorofa ya Saba. Unimax Marketing. Ally Hassan.'
"What the fu*k is this?" Nikajisemea kimoyo moyo..
Nikakikunja kile kikaratasi nikakiweka kwenye begi la mgongoni pembeni ya kitanda, kisha nikajilaza nikitafakari hiki kinachoendelea. Na baada ya kama dakika ishirini usingizi ukanipitia.

* * * * *

Saa kwenye simu ilikuwa inanionyesha ni saa tisa na dakika arobaini. Nilikuwa nje nimesimama nasubiria taxi. Nilikuwa nimempigia simu Musa, dereva taxi maarufu maeneo ya mwembechai ninaye mfahamu toka niko nasoma sekondari.
Kama dakika tano baadae Musa aliwasili na bila kuchelewa kama ilivyo ada yetu waswahili nikafungua mlango wa mbele na kukaa pembeni ya dereva badala ya kukaa siti ya nyuma ambapo ndipo haswa anapotakiwa kukaa abiria.

"Niaje kichwa?" Musa akinisalimu kwa uchangamfu na tabasamu kama ilivyo kawaida yake.
"Poa tu, mishe vipi" nikamjibu na kumuuliza.
"Mishe mwanana tu mwanangu! Adimu sana kichwa vipi mtoto mzuri gani kakuficha mwanangu hahaha!" Kama kawaida Musa akaanza masikhara na kucheka kama kawaida yake.

Musa alikuwa na desturi ya kupenda masihara na mara zote yeye mwenyewe ndiye anakuwa wa kwanza kucheka kwa sauti kubwa hahahaha.
"Nifichwe wapi mwanangu! Kutafuta ugali tu." Nikamjibu.
"Nakuaminia sana baharia wangu! Alafu unajua j'mo tunawakalisha kama watoto"

Daah ndio akanikumbusha kuwa jumamosi kuna mechi kali ya Barcelena na Madrid. Mawazo niliyokuwa nayo yalinisahalisha kabisa kuwa kuna mambo mengine yanayoendelea duniani.
Musa alikuwa mnazi wa Barcelona na mimi nilikuwa mnazi wa Madrid.

"Mumkalishe nani wachumba nyinyi, subiri uone tunavyowapakata" nikamjibu nikijitahidi kuwa natural kuficha mawazo niliyo nayo kichwani.
"Tunaelekea wapi babu?" Hatimaye akaniuliza.
"Stesheni mwanangu, PPF House."
"Mia mia"

Safari ikaendelea pamoja na utani wa hapa na pale, na dakika ishirini baadae tukafika PPF.
Nikatoa noti mbili za elfu kumi nikampatia Musa. "Ya uchakavu hii mwanangu" nikampatia
"Shukrani" Musa akajibu huku anatoa shilingi efu tano anirudishie chenji.
"Zuia hiyo mwanangu usijali" nikamzuia asinipe chenji.
"Dah shukrani kichwa"
"Mia"

Tukaagana na kushuka kwenye gari nikaingia ndani ya jengo la PPF House.
Jengo hili nalifahamu vizuri sana, kuna shemeji yangu alikuwa anafanya kazi hapa miaka ya nyuma, nimewahi kufika hapa mara kadhaa lakini sikuwahi kusikia kampuni ya Unimax Marketing kuwa na ofisi katika jengo hili. Nilikuwa najua PPF wenyewe, Sumatra na kampuni nyingine kutumia jengo hili lakini sio Unimax Marketing. Na si hivyo tu bali pia hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuisikia kampuni ya Unimax Marketing.

Nikaenda mpaka kwenye meza ya kuandika majina ya wageni.
Mlinzi akaniuliza "Mfanyakazi au mgeni?"
"Mgeni" nikamjibu kwa mkato.
Akanisogozea kaunta book lililokuwa limefunguliwa liko juu ya meza.
Nikalivuta karibu na kabla sijaandika nikapitisha macho haraka haraka na niliangalia zaidi kwenye jedwali watu wanapoandika ofisi anayo kwenda. Nikaona majina tu ya PPF, Sumatta, BUMACO yakiwa yanajirudia rudia lakini sikuona Unimax Markering hata sehemu moja.

Nikaandika jina langu, kisha nikapita kwenye Mashine ya ukaguzi na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye lifti. Kwenye lifti nikabonyeza kitufe namba saba na ndani ya dakika moja mlango wa lifti ukafunguka nikiwa ghorofa namba saba.

Nilitoka na kusimama koridoni na mbele yangu kulikuwa na mlango wa kioo ulioandikwa Unimax Marketing. Nikaufungua na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye meza ya mapokezi.

"Habari yako dada" nikamsalimu mdada mrembo aliyekuwa mapokezi.
"Salama tu, nikusaida nini kaka" akaniuliza.
Nikashikwa na kigugumizi kwa sekunde kadhaa. Sikujua nimjibu nini. Anisaidie nini??.

"Aaaah natakiwa niwe hapa jina langu naitwa Ally Hassan" nikakumbuka jina nililotajiwa jana kwenye simu na nilijitahidi kujieleza kwa kumung'unya maneno.
"Subiri hapo kwenye kiti tafadhali"
Yule dada alinijibu haraka baada ya kumtajia jina la Ally hassan akionekana ameelewa ninachozungumza. Nikasogea pembeni na kukaa kwenye kiti cha wageni.

Dada akainua simu ya mezani na kumpigia mtu. "Amefika" alimwambia kwa kifupi huyo aliyekuwa anaongea nae. Baada ya hapo akawa bize anaendelea na shughuli zake. Dakika moja baadae akaja mdada mrefu, mrembo haswa amevalia sketi fupi nyeusi na shati jeupe.
"Habari, yako? Nifuate tafadhali"
Dada alinisalimu na kabla sijamjibu akanipa maelezo nimfuate.

Nikainuka na kumfuata. Kulikuwa na milango kadhaa ya ofisi yote ikiwa ya vioo, tukakata kushoto na kufuata korido iliyoenda moja kwa moja na mwishoni kulikuwa na mlango wa mbao. Yule dada akaufungua tukaingia. Ndani kulikuwa kama chumba cha daktari au theater. Nikaanza kushikwa na hofu kiasi.
Baada ya kuingia tu, akaingia mwanamama mwingine amevalia suti amebeba kibriefcace kidogo.

"Jina langu ni Zuhura na huyu mwenzangu anaitwa Jeniifer, atakufanyia utaratibu wa kawaida ili tuweze kuendelea na ratiba nyingine." Aliongea yule dada mrefu. Siku sema chochote nilibaki tu nawakodolea macho.

Yule mama aliyetambulishwa kama Jennifer akaweka kibriefcase chake juu ya meza na kukifungua. Akatoa gloves na kuzivaa mkononi. Mapigo ya moyo yakaanza kuniaenda mbio. Nikaanza kujutia kwanini hata nimekuja hapa.
Mara akatoa bomba la sindano na pamba. "Naomba mkono wako wa kushoto" yule mama akaongea.

"Hey wait!" Nikafoka huku namuangalia yule dada aliyejitambulisha kama Zuhura. "Unaweza kinambia nini kinaendelea hapa." Nikamuuliza huku natetemeka.
"Sikiliza Ray, tunaweza kuendelea na utaratibu au unaweza kufungua mlango na kuondoka" alinijibu huku amenikazia macho bila kuyapepesa.
Nikajishangaa mpaka mimi mwenyewe, Zuhura aliniruhusu kama sitaki kuendelea na 'utaratibu' wanaoufanya basi naweza kwenda,

lakini jambo la ajabu kuna sehemu kubwa ya nafsi yangu ilikuwa haitaki kuondoka, inataka kufika mwisho wa hili jambo. Ni kama unapotamani usinywe pombe lakini nafsi yako inashindwa kujizuia. Nikajifariji moyoni kuwa nimeshakula ng'ombe mzima wacha nimalizie mkia.

"Fu*k it!" nikajikuta nimetamka kwa nguvu na kumnyooshea mkono yule mama Jennifer. Atumia sindano kunitoa damu kiasi kwenye mkono wa kushoto na kisha sindano ile yenye damu akaihifadhi kwenye kifaa kama kimkebe na kurudisha kwenye briefcase yake. Kisha akatoa kifaa kama simu ya 'tablet' na kuanza kuniscan viganja vya mikono, akaanza na mkono wa kulia na kisha mkono wa kushoto. Nikaelewa alikuwa anachukua alama za vidole.
Akipomaliza akaweka vifaa vyake vyote kwenye briefcase na kuondoka.

"Tumemaliza tunaweza kuendelea sasa, nifuate" aliongea yule dada Zuhura huku akigeuka kuanza kuelekea kwenye mlango. Nikainuka na kumfuata. Tukapita tena koridoni kwenye milango ya vioo ya ofisi na kukata kushoto tukatokea mapokezi. Hapo tulimkuta jamaa ambaye jinsi alivyo vaa na umbo lake anafanana kabisa na Kevin ambaye alikuja Jana nyumbani.

Alikuwa na umbo la miraba minne na alikuwa amevalia Kaunda suti. Alipotuona akasimama. Tulipo mkaribia akafungua mlango na wote kwa pamoja mimi, Zuhura na huyo jamaa tukatoka nje kuelekea kwenye lifti.
Tukashuka chini na jamaa akatuongoza mpaka kwenye parking ya magari.

Tukapanda gari nyeusi inayofanana kabisa kabisa na waliyokuja nayo nyumbani Dr. Shirima na wenzake jana. Land cruiser V8 nyeusi.
Safari ikaanza tukaikamata Morogoro Road moja kwa moja mpaka Ubungo. Ubungo tukapinda kulia Kuifuata Barabara ya Sam Nujoma moja kwa Moja mpaka mwenge.

Kwenye makutano ya barabara tukanyoosha moja kwa moja na mbele kidogo tukakata kushoto kisha kulia. Nikaelewa kuwa tunaelekea Mikocheni B, kitu ambacho sikuwaelewa ni kwanini tumezunguka sana. Hii tayari ilikuwa imefika saa mbili usiku.

Mikocheni B tukapita Kanisa la Mlima wa Moto, tukaenda mbele kidogo mtaa wa nyuma yake. Tukaifikia nyumba moja iliyokuwa imejitenga kiasi na nyingine. Ilikuwa na uzio wa ukuta mrefu na juu una waya za umeme na geti kubwa.

Tulipofika nje ya geti hili bila kupiga honi geti likafunguliwa. Pembeni ya geti kwa ndani kulikuwa na watu wawili ambao walionekana walikuwa ni walinzi lakini walinzi hawa walikuwa na tofauti. Walikuwa wamevalia sawa kabisa na jamaa huyu tuliyeongozana nae kuja hapa na Kevin aliyekuja jana nyumbani. Wote wana miili ya mazoezi na walivalia Kaunda suti.

Nyumba hii ilikuwa na ghorofa moja na moja kwa moja jamaa akaenda kupaki gari ambapo hapa tulikuta karibia gari ishirini za aina tofauti. Range Rovers, V8, BMW, n.k. moja kwa moja nikajua gari hizi si za mtu mmoja bali kuna watu wamekuja nazo kama sisi. Hii ilimaanisha kulikuwa na kikao hapa. Na kwa muonekano wa gari hizi za gharama ni dhahiri kilikuwa ni kikao kizito.

Tukashuka kwenye gari, yule jamaa tuliyekuja naye akaelekea getini kwa 'wenzake' na Zuhura akaniongoza kuingia ndani ya Jumba hilo. Kadiri tulivyokuwa tuna pig a hatua kuingia ndani moyo wangi ulizidi kulipuka kwa hofu. Nilikuwa kwenye taharuki kubwa kiasi kwamba nilianza kutokwa jasho.
Baada ya kuingia ndani tukapandisha ngazi zilizokuwa zinaelekea juu ghorofani.

Tulivyofika juu, tukakutana na korido ndefu ambaye tuliifuata mpaka kufika katikati ilikuwa inaungana na korido nyingine ndogo mkono wa kushoto. Tukipokata kushoto kulikuwa na mlango mkubwa. Zuhura akaufungua na kunikaribisha ndani.

Kilikuwa ni chumba cha mikutano lakini hakikuwa na mtu. Kulikuwa na meza ndefu ya mikutano ya kiofisi na viti vinne kila upande.
Zuhura akaniashiria niketi.
"Subiri hapa" akanieleza kwa mkato tu kisha akatoka nje.
Ndani nikabaki peke yangu. Upande mmoja wa chumba hiki ulikuwa ni kioo tupu, hii iliniwezesha nione kwa urahisi kinachoendelea nje.

Baada ya kama dakika kumi hivi, nikaona nje geti linafunguliwa na gari tatu aina ya Range Rover ziliingia zikiwa zimeongozana. Baada ya kuingia hazikwenda kupark bali zilienda mpaka mlango wa mbele wa kuingia ndani ya nyumba. Magari mawili kati ya yale matatu, milango ilifunguliwa na watu wakashuka lakini gari la katikati milango haikufunguliwa kwa muda wa takribani dakika moja.

Wale walioshuka ambao wote wamevalia suti, waliangaza macho kila upande. Kisha wakafungua mlango wa nyuma wa gari ile ya kati kati na kuna mtu akashuka na wakaanza kuingia ndani ya jengo. Walitembea katika mtindo ambao yule mtu alikuwa katikati mbele yake kulikuwa na watu wawili, nyuma watu wawili na kulia na kushoto watu wawili wawili. Wakaingia ndani ya jengo. Nilijitahidi kadiri niwezavyo nione sura yake lakini sikufanikiwa kutokana na Giza na jinsi alivyozungukwa na walinzi.

Nikabaki nikitafakari sehemu hii nilipo. Nini kinaendelea, na kwenye hiki kitu nilichojiingiza. Nikajiuliza tena na tena, hawa watu ni akina nani, malengo yao ni nini na wanataka nini kutoka kwangu.
Niliwaza na kuwazua, nikasimama na kuanza kutembea kutoka upande mmoja wa chumba mpaka upande mwingine, tena na tena.

Baada ya kama dakika 45 msafara wa yule mtu mwenye walinzi ulitoka na moja kwa moja wakapanda kwenye gari zao na kuondoka. Kama dakika kumi baadae nikaona watu wengine karibia kumi na tano wanatoka na kwenda kupanda kwenye zile gari tulizozikuta wakati tunafika. Wote walikuwa wamevalia suti nadhifu na zote zilikuwa rangi nyeusi.
Nikajaribu kuwatazama kwa umakini niweze kung'amua walau watu wachache.

Nilipata mshtuko nilipoweza kuwang'amua watu wawili.
Wa kwanza alikuwa ni mfanyabiashara maarufu nchini na mmliki wa vyombo vya habari. Mzee Bernard Shayo
Wa pili alikuwa ni mbunge kijana na mwanasiasa mashuhuri nchini, Zephania Zuberi.

Presha ilinipanda na mshtuko nilioupata nikaanza kutokwa jasho mpaka shati nililolivaa kikaanza kulowa.
Nikakaa chini kwenye kiti. Nikitafakari, na kuwaza lakini akili ilikuwa haifanyi kazi kabisa kutokana na mshangao niliokuwa nao.

Mara mlango ukafunguliwa. Nilipigwa na butwa nilipomuona aliyeingia. Alikuwa ni Dr. Shirima akiwa amevalia suti nadhifu ya rangi nyeusi kama wale wengine niliowaona. Pia katika ukosi wa koti la suti usawa wa mfuko alikuwa ameweka pini kama ile inayovaliwa na viongozi wa kiserikali ikiwa na bendera ya nchi. Lakini pini hii ilikuwa tofauti, ilikuwa na rangi nzuri ya zambarau na kwa ndani ilikuwa na mchoro kama wa kichwa cha simba ambao ulikuwa na rangi ya dhahabu.

"Hujambo Ray?" Alinisalimia Dr. Shirima kwa tabasamu, mkononi alikuwa ameshika bahasha.
"Hapana dokta siko ok, nimeenda kwenye ofisi ambayo sijawahi kuisikia, nimetolewa damu, nimechukuliwa alama za vidole alafu naletwa hapa jumba lenye mazingira ya kutatanisha, so yes am not ok dr. Labda unieleze kinachoendelea."

Kama kawaida yake, Dr. Shirima akatabasamu "Relax Ray." Akaongea huku ananipa bahasha aliyokuwa ameishika mkononi.
Nikaipokea na kuiweka juu ya meza.

"Naomba upitie hizo document zilizomo ndani, kuna mambo namalizia kidogo nitarudi baada ya nusu saa! Zisome na uzielewe." Dr. Shirima aliongea huku ananitazama usoni kwa udadisi. "Unaonekana kama una swali Ray, uliza."
"Who are you people?" Nikamuuliza huku nimemkazia macho, nikiwa namaanisha kweli kweli.

"The Board! Karibu sana Ray." Dr. Alinijibu kwa ufupi na kutoka nje.

Nilikuwa nimebaki tena peke yangu ndani ya chumba hiki ma nikiwa na nusu saa tu kupitia hizi document kabla Dr. Shirima hajarudi tujadiki hicho anachotaka tujadili. Nikaifungua ile bahasha. Ndani kulikuwa na karatsi zipatazo kumi na karatasi ya juu ilikuwa na kichwa cha habari T.B.F.Q Strategy # 0034.

Nikaketi kwa utulivu, nikavuta pumzi ndani na kuzishusha kwa taratibu. Akili ikakaa sawa. Nikaanza kuzisoma.

The Board ni watu gani? Malengo yao ni yapi? Wanataka nini kutoka kwa Ray? Mkakati # 0034 unahusu nini?

Join my exclusive whatsapp group kusoma simulizi na makala kila siku - 0718 096 811 (kuna "subscription fee")


The Bold.
Habari mkuu nilipoteza mawaauliano na wewe kule whatsap tafadhali naomba uniunganishe tena
Maana bado ni mwanachama hai
Na tanguliza shukrani
 
HATIMAYE JUMANNE IMEFIKA..

STAY TUNED!! LEO HII EPISODE 10 YA VIPEPEO WEUSI ITAKUWA HAPA..
Sijui ulishawahi kufikiri kama kuna watu hawana simu janja (smartphone) nikiwepo mimi wa kwanza, na hivyo hatuwezi kupata access ya kuji-whatsappisha kwa stori zako. Kwa nini usifungue say website na iwe na restrictions za registered members only ndiyo wasome post zako, na wakati huo huo, hao registered wanakuwa na fee kila mwezi au kwa mwaka. Naona hiyo itafanya hata sisi tusio na simu za kutuwezesha ku-access whatsapp, tutakuwa na sehemu ya kupata stori zako kwa wakati kulikoni hii ya kuleteana arosto zisizo na sababu. Ni maoni tu lakini. Na by the way, whatsapp ina restriction ya only 250 (kama bado iko vile niliacha), wakati website (blog) ina watu wengi zaidi ya hao. Na uzuri tayari una fan base ya kuanzia.
 
Ni shilingi elfu tano kwa mwezi..

Makala moja ya uchambuzi kila siku asubuhi..

Episode moja ya simulizi kila siku jioni..
Utaratibu ukoje wa kufanya malipo na kutambulika kama nimejiunga na huduma hiyo
 
Sijui ulishawahi kufikiri kama kuna watu hawana simu janja (smartphone) nikiwepo mimi wa kwanza, na hivyo hatuwezi kupata access ya kuji-whatsappisha kwa stori zako. Kwa nini usifungue say website na iwe na restrictions za registered members only ndiyo wasome post zako, na wakati huo huo, hao registered wanakuwa na fee kila mwezi au kwa mwaka. Naona hiyo itafanya hata sisi tusio na simu za kutuwezesha ku-access whatsapp, tutakuwa na sehemu ya kupata stori zako kwa wakati kulikoni hii ya kuleteana arosto zisizo na sababu. Ni maoni tu lakini. Na by the way, whatsapp ina restriction ya only 250 (kama bado iko vile niliacha), wakati website (blog) ina watu wengi zaidi ya hao. Na uzuri tayari una fan base ya kuanzia.
Kuwa na.whatsapp sio lazima smartphone hata pc inawezekana

Bluestack

Anyway
Nisiwe kimbelefront ngoja hakujibu muhusika wazo ni zuri mkuu
 
Sijui ulishawahi kufikiri kama kuna watu hawana simu janja (smartphone) nikiwepo mimi wa kwanza, na hivyo hatuwezi kupata access ya kuji-whatsappisha kwa stori zako. Kwa nini usifungue say website na iwe na restrictions za registered members only ndiyo wasome post zako, na wakati huo huo, hao registered wanakuwa na fee kila mwezi au kwa mwaka. Naona hiyo itafanya hata sisi tusio na simu za kutuwezesha ku-access whatsapp, tutakuwa na sehemu ya kupata stori zako kwa wakati kulikoni hii ya kuleteana arosto zisizo na sababu. Ni maoni tu lakini. Na by the way, whatsapp ina restriction ya only 250 (kama bado iko vile niliacha), wakati website (blog) ina watu wengi zaidi ya hao. Na uzuri tayari una fan base ya kuanzia.
Wazo zuri mkuu, shukrani..
Nitafnyia kazi!
 
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034









EPISODE 10




Nilikuwa katika kile kichumba ambacho wenyewe wanakiita tunduni, kichumba ambacho mahabusu wanawekwa wakiwa wanasubiria kupandishwa kizimbani.

Niliporudishwa na askari kutoka ofisini kwa hakimu niliwakuta mahabusu wengine watano humu ndani ya kichumba ambao wao walikuwa wameletwa kutoka gerezani kuja kusikiliza kesi zao.

Uzuri kesi zao zote zilikuwa zimekuja kutajwa tu siku ya leo. Kwahiyo walikuwa wanachukuliwa na kupandishwa kizimbani, kisha kesi inatajwa na kuhairishwa kisha wanarudishwa tena humu tunduni. Hii ili maanisha kuwa muda si mrefu zoezi la kutajwa kesi litaisha na tutapelekwa gerezani.

Nilikuwa nimesimama tu naangalia nje ya tunduni kupitia dirisha. Akilini mwangu mawazo kadhaa yalikuwa yanapita kichwani.

Cha kwanza niliwaza kuhusu The Board. Ni dhahiri kuwa walikuwa hawataki niende gerezani na hii nilihisi kuwa walikuwa wamefahamu au wamehisi mpango wangu kuwa nina lengo la kuonana na Eric Kaburu. Kwahiyo kichwani mwangu niliamini kuwa labda walikuwa na hofu ni kitu gani Kaburu atanieleza kama nikifanikiwa kumshawishi kuongea na mimi.

Ilikuwa ni ajabu kupata kikaratasi cha kunitaka tuonane kutoka kwa Dr. Shirima kwa muda mfupi hivi toka tuonane. Ni takribani wiki tatu pekee toka tuonane pale kwenye parking ya Nashera Hotel na kwa kawaida ingepita miezi mitatu au hata minne ndio niletewe kikaratasi kingine cha kunitaka tuonane. Hivyo ni dhahiri kuwa hii ilikuwa ni 'emergency'. Na nilitafsiri kuwa walikuwa wanahofia mimi kuonana na Kaburu.

Upande mwingine ni Idara ya Usalama wa Taifa. Kwanini nao hawataki niende gerezani? Je, wanahofia usalama wangu? Au labda wamehisi nina mpango gani na wanaona si mpango sahihi?
Sikupata jibu zaidi ya kujua tu kwamba nao hawataki niingie gerezani. Rohoni mwangu nikazidi kuamini kwamba ninachokifanya ni sahihi kabisa ndio maana The Board hawataki nikifanye, na ndio maana Usalama wa Taifa nao hawataki nikifanye.

Nikiwa bado nachungulia nje ya dirisha, nikamuona Baba Bite akiwa anaingia tena getini. Alikuwa amebeba briefcase na alipoingia akatembea kwa haraka sana kuja huku tunduni. Nikamfuatilia kwa macho na nikamuona ameenda mpaka nje ya hiki kichumba mahala ambapo maaskari wanaotulinda wamekaa.

Alipofika nikawaona kama wanasalimiana kisha akaingiza mkono mfukoni na kutoa kitu kama kitambulisho hivi mfukoni na kuwaonyesha. Ghafla wale maaskari wote nikawaona wamesimama kwa ukakamavu na kupiga saluti.

Kisha maaskari wawili, yule aliyenipeleka ofisini kwa hakimu kusomewa shtaka na mwingine mwenye silaha wakaongozana na Baba Bite mpaka mlangoni mwa hiki kichumba na kufungua.

"Haya tokeni nje" yule askari ambaye hakuwa na silaha akaamuru.

"Wewe baki ndani" akaninyooshea kidole mimi.

Wale wenzangu wote wakatoka nje nikabaki mimi peke yangu. Kisha nikamuona Baba Bite ameingia na briefcase yake na mlango ukafungwa.

"Ray, sijawahi kuona mtu mpuuzi kama wewe" Baba bite akaongea akiwa serious.

"Nilishawaambia nikijua chochote nitawasiliana na nyinyi, haya ni maisha yangu na nafanya kile ninachokiona sahihi" nikamjibu kwa kujiamini.

"Hivi unafahamu kuwa The Board hawawezi kuruhusu upate hizo taarifa unazozitaka? Na wanaweza hata kuua kabla haujazipata?" Akaniuliza huku anafungua briefcase yake.

Nikakaa kimya, sikujibu chochote.

Alipomaliza kufungua briefcase akatoa karatasi nyeupe ya A4 yenye maandishi yaliyo chapwa. Akanikabidhi mkononi.

"What is this?" Nikapokea karatasi na kumuuliza.

"Hicho kilichopo humo kitakusaidia labda kukuepusha na kifo ukiwa ndani gerezani" akanijibu
"Hakikisha unaificha isionekane ukiwa unaingia gerezani"

"Nitaifichaje wakati nasikia kabla hujaingia gerezani unasachiwa" nikamuuliza.

Baba bite akatabasamu. Tabasamu fulani hivi kama ananicheka .

"Well, wenzako wafungwa wazoefu huwa wanaficha vitu katikati ya makalio ila wanaingiza kwa ndani kidogo" akaongea huku anatabasamu zaidi kama ananicheka.

"***!!" Nikasikia kinyaa. "Na kwanini wewe na wenzako kwenye Idara mjisumbue kiasi hiki kutaka kulinda Usalama wangu gerezani, napata hisia kuwa kuna kitu haukisemi"

"Ray, bado kuna mambo mengi tunahitaji utusaidie… So wewe ni asset kwetu na kila binadamu ana haki ya kulinda asset yake" akatabasamu.

"Bullshit!" Nikamjibu kwa kukereka.

Baba bite akagonga mlango na askari aliyekuwepo nje akafungua.

"Hey, alafu mshtakiwa anataka kwenda kujisaidia.. Mpelekeni tafadhali kabla hajaenda ngomeni" Baba bite akaongea na kunikonyeza kwa kunicheka.

Nikajikuta nacheka kichini chini nikikumbuka ushauri alionipa jinsi ya kuficha ile karatasi.

"Sawa mkuu, twende mshtakiwa" yule askari akajibu.

Akanisindikiza mpaka chooni ambavyo vilikuwa karibu tu na tunduni. Akabaki nje ya mlango wa choo na mimi nikaingia ndani.
Nilichokifanya huko ndani kuficha ile karatasi siwezi kusimulia.

Nikatoka chooni baada ya kama dakika tano hivi. Wote walikuwa wananisubiri mimi. Tukapandishwa katika difenda ya polisi na safari ya kuelekea magereza ikaanza.

Gari ikanyoosha moja kwa moja mpaka 'round about' ya mnara wa mashujaa, tukapinda kulia barabara ya 'Old Daresalaam Road', tukaenda kidogo kama tunaelekea kilakala na dakika kama kumi hivi tulikuwa tumeshafika Gereza Kuu la mkoa wa Morogoro.

Kwa miaka mingi niliyokuwa naishi Morogoro nimekuwa nikipita njia hii na kuliona jengo hili lenye muonekano wa kuogofya.
Jengo hili la magereza kwa muonekano wa nje lilikuwa limejengwa kwa mawe yenye rangi kama nyeusi hivi iliyo changanyika na kijani lakini imepauka sana na lilikuwa na kuta ndefu sana zilizopanda juu sana na zimewekewa nyaya za miiba. Ukiwa nje unaona miembe miwili mikubwa imechomoza ikiwa ndani ya gereza.

Nimeliona jengo hili la kutisha kwa miaka mingi lakini leo linaenda kuwa makazi yangu.

Geti kubwa likafunguliwa. Tukaingia ndani wote sita.

Pale ndani kulikuwa na kama kibaraza hivi, na mkono wa kushoto kuna chumba kile ambacho watu wanaingia wakienda kuwaona wageni na mkono wa kulia kulikuwa na mlango ambao bado sikujua kazi yake lakini nitaijua mda mchache ujao.

Tulipoingia tu hapo kwenye kama hicho kibaraza. Wenzangu wote wakachuchumaa chini. Na mimi nikachuchumaa. Kisha mmoja wa yule askari tuliyekuja naye akamkabidhi makaratasi mmoja wa maaskari magereza tuliowakuta pale.

"Kuna fresh mmoja" yule askari akamueleza yule askari magereza. Kisha akapewa likitabu fulani hivi akaandika andika na mwishoni nikamuona anatia saini.

Baada ya kukamilisha hizo taratibu yule askari tuliyekuja naye na wenzake wakaondoka. Tukabakia na maaskari magereza watatu mbele yetu.

Akachukua zile karatasi na kuanza kuita majina. Alikuwa anaita katika mfumo ambao, anasoma jina lako la kwanza pekee alafu wewe unamalizia jina lako ka kati na la mwisho na unayatamka kwa kupayuka kwa nguvu kweli kweli kisha unasimama.

Akasoma majina ya wenzangu wote watano, na jina langu mimi lilikuwa la mwisho.

"Rweyemamu!" Akasoma

"Charles Kajunaaaaaaa" nikapayuka kama wenzangu walivyofanya na kusimama.

"Wewe ndio fresh?" Akaniuliza.

"Ndio" nikajibu

"Ingia huko"

Akanionyesha ule mlango wa mkono wa kulia.

Nikafungua na kuingia ndani. Ilikuwa ni ofisi na nilimkuta askari magereza kijana wa kama makamo yangu hivi ameketi.

"Karibu" yule askari akanikaribisha.

Huyu jamaa kwa kiasi fulani alikuwa tofauti na wale maaskari magereza wengine. Akikuwa ana mwonekano fulani hivi na 'swaga' ya kisomi somi flani hivi. And alikuwa na kiwango kikubwa sana cha ustaarabu pengine kuzidi hata jinsi askari magereza anavyotakiwa awe.

Akanikabidhi makaratasi ya kujaza. Nikajaza majina yangu kamili, namba yangu ya kesi, kesi yangu inahusu nini, ninakoishi, jina kamili la ndugu wa karibu, anuani yake na namba yake ya simu na mwishoni nikasaini.

Akaichukua ile karatasi, akaipitia kwa makini kisha akaniuliza.

"Hivi wewe si ndiye mwenye ile nini inaitwa… Aaahh Sote! Yeah sote hub? Si ni wewe?"

"Yeah ni mimi" nikamjibu kwa kiasi fulani huku najisikia aibu.

"Aisee, pole sana kiongozi yataisha haya! Ndio maisha"

"Nashukuru sana"

Akanionyesha nifungue mlango mwingine wa kutokea tofauti na ule niliotumia kuingilia. Nikafungua na kutokea kwenye chumba kingine na sekunde chache wale mahabusu wengine wakiwa na wale maaskari magerez nao wakaingia.

Hiki chumba kilijuwa kimeungana chumba kingine lakini hakukuwa na mlango kati kati.

Yaani kilijengwa katika mtindo ambao kulikuwa na vyumba viwili vinavyopakana lakini havikuwa na mlango wa kufungua, unapita tu na kuingia chumba kinachofuata.

Tukiwa pale kwenye kile chumba cha kwanza nikaona wenzangu wanaanza kuvua nguo. Na mimi nikafuatisha. Tukavua nguo zote na kubaki uchi kabisa.

Ingawa wote tulikuwa wanaume lakini hakuna kitu kinachokera kama kuwa kwenye kundi la wanaume wenzako mkiwa uchi. Inakera haswa.
Wengine sijui hawajanyoa wana miezi mingapi, wengine maumbile makubwa kama waigizaji wa filamu za ngono, wengine maumbile madogo yamesinyaa utadhani nyanya chungu za juzi. Ili mradi ni kero tu. Nilitamani kujifunika uume wangu kwa mikono kama mtoto.

Wenzangu walikuwa kawaida tu, inaonekana wamezoea hili zoezi.

"Haya twende" askari mmoja akaamuru.

Nikaona mahabusu mmoja ameingia kwenye kile chumba kinachofuata kisha baada ya muda sauti ya mlango huko kwenye chumba hicho unasikika unafunguliwa na huyo maabusu anaondoka. "Mwingine" anaita huyo mtu aliyeko kwenye chumba cha pili.

Wote wakafuata utaratibu huo na mimi nikawa wa mwisho.

Nikaingia uchi na nguo zangu nimeshikilia mkononi. Kwenye hicho kichumba kulikuwa na askari kijana tu ila ana sura chungu kweli kweli ya kibandidu amekaa kwenye kiti na kuna meza mbele yake. Chumba kizima hakukuwa na kabati la ofisi wala taka taka yoyote ile. Kulikuwa na kiti na meza ndogo tu na huyu askari aliyekaa. Nikafika nimesimama tu namwangalia.

"Unashangaa nini wewe msenge, lete nguo hizo" akafoka yule askari.

Nikaweka nguo zangu juu ya meza. Akaanza kuzikagua. Akasachi mifukoni, akakagua kwenye pindo za nguo, kisha akaikung'uta kung'uta mara kadhaa, alipomaliza akazitupa sakafuni.

"Geuka" akaniamuru.

Nikageuka.

"Inama" akaniamuru tena.

Nikasita. 'Huyu msenge ukaguzi gani huu'! Nikajisemea kimoyo moyo.

Sikutaka matatizo. Nikainama.

Alikuwa bado amekaa pale kwenye kiti nyuma ya meza. Nikamchungulia kwa chini nikiwa nimeinama. Nikamuona yuko makini sana "kunikagua".

"Panua matako" nikamsikia ananiamuru.

Nikajikuta ghafla nimeshikwa na hasira iliyochanganyika na hofu. Pia nikakumbuka huko ninakoambiwa nipanue nimeficha karatasi niliyopewa na Baba Bite. Nisipofanya kitu hapa nitaumbuka na kujiingiza kwenye matatizo mengine

Nikainuka kwa hasira.

"Huku sio kunisachi sasa, huu ni udhalilishaji!!" Nikaongea kwa hasira kwa sauti ya juu.

Yule askari akainuka haraka kutoka kwenye kiti akiwa amefura kwa hasiara.

"Unasemaje wewe msenge!!" Akafoka.

"Huu udhalilishaji, sio ukaguzi huu" nikavimba.

"Skia we msenge, hii jela! Unaskia, usiniletee usenge usenge wako wa haki za binadamu, hii jela!! Nikikwambia lala unalala, nikikwambia kaa chini, unakaa chini, nikikwambia simama unasimama, nikikwambia panua matako, una panua matako!!" Yule askari akafoka kwa hasira huku amefura ananisogelea pale niliposimama.

Moja wapo ya mbinu za kumkabili adui ni kamwe kutokumuonesha hofu yako. Kwa hiyo na mimi nikamvimbia. Sikusogea hata hatua moja nyuma. Nikamtazama usoni kwa hasira huku 'nimevimba'.

"Unaskia we msenge, nikikwambia panua matako unafanyaje?" Akaniuliza kwa kufoka.

"Ukinambia panua matako nakwambia panua wewe kwanza!!" Nikamjibu kwa hasira na kufoka kwa sauti ya juu.

Akanishtukiza kwa kofi zito shavuni. Lilikuwa kofi kali mpaka nikajiinamia kwa maumivu. Mara nikasikia 'kifuti' kikali amenipiga mbavuni. Nikadondoka chini kuugulia maumivu.

"Nitakuumiza wewe **** wewe! Nitakuumiza!!" Akafoka kwa hasira huku ananipiga mateke ya mbavuni pale chini nilipo lala.

Nikasikia maaskari wengine wanaingia.

"Hey, hey, hey, hebu muacheni" nikasikia askari mmoja ana waamuru.

"Mseng* huyu hataki kukaguliwa anatuletea ujuaji!!" Akafoka yule askari bandidu aliyenipiga.

"Ni mgeni hajui utaratibu! Hebu tokeni nitamkagua Mimi msije kuleta balaa hapa" yule askari mwingine akawamuru.

Nikamuangalia vizuri, alikuwa ni yule askari mwenye "swaga za kisomi" aliye niandikisha maelezo yangu kwenye chumba kingine kile.

Wale askari wengine wakaondoka kwa hasira. Nikajiinua na kukaa sakafuni. Bado niko uchi.

"Inuka uvae" yule askari akaniamuru.

Nikasimama huku naugulia maumivu na kuanza kuvaa.

"Dogo, hii sehemu hatari sana! Usijifanye mjuaji utaumia!!"

"Sorry! Nashukuru kwa kuniokoa kiongozi" nikamjibu kwa sauti ya maumivu huku navaa.

"Usijali! Unasaidia vijana wengi huko uraiani kwahiyo wewe ni asset na asset inapaswa kulindwa!"

Nilikuwa nafunga mkanda nikajikuta nimeganda kama sanamu. Hii ilikuwa ni bahati mbaya au ameongea sentesi hii kwa makusudi? "wewe ni asset na asset inapaswa kulindwa"!!
Nusu saa iliyopita Baba bite ametoka kunambia sentesi inayofanana kabisa na hii. Na huyu anakuja kuniokoa na kutamka sentesi kama hiyo! Ni bahati mbaya au amefanya kusudi?

Nikainua kichwa kumtazama. Tukakaziana macho kama sekunde thelathini hakuna aliye pepesa macho.

Kisha akatabasamu. Pembeni ya hiki chumba kulikuwa na mlango mkubwa kama geti. Akaenda mpaka hapo mlangoni na kunifungulia.

"Kilala kheri" akaongea akinionyesha ishara nitoke kwenye chumba na kuingia rasmi gerezani.

Sikujibu chochote. Nikamuitikia kwa kichwa tu. Nikapita mlangoni na kutokea upande wa pili. Gereni kwenyewe. Sasa nilikuwa nimekanyaga rasmi gerezani.

Watu wanaona jinsi gereza linavyoogopesha kwa nje ukilitizama, lakini kitu wasichofahamu ni kwamba hakuna kitu chenye kuogofya kama muonekank wa gereza kwa ndani.

Nikavuta pumzi kubwa ndani na kuitoa nje. Sasa umefika wakati wa kuikabili 'jehanum' iliyoko mbele yangu.

Nilibaki nimesimama pale nilipo kwa dakika kadhaa nikiangalia kilichopo mbele yangu.

Nilikuwa ndani ya gereza kwa mara yangu ya kwanza kwenye maisha. Nilihisi kama niko ndotoni.

Mbele yangu niliona vyumba vikubwa kama 'halls' vitatu. Moja kilikwa mkono wangu wa kushoto na vingine viwili mbele yangu. Kati kati kulikuwa na uwanja mkubwa. Pia mbele yangu kulia kidogo kulikuwa na chumba kingine kikubwa ambacho kutokana na moshi pamoja shughuli zilizokuwa zinaendelea nikaelewa kuwa lilikuwa ni jiko.

Nikajiuliza wafungwa na mahabusu wako wapi?

Maana mbele yangu pale katikati kwenye nafasi kubwa kama uwanja ambao chini imemwagwa sakafu ya zege kulikuwa na Nguo nyingi zimetandazwa chini zimeanikwa. Kulikuwa na sare za kifungwa na nyingine nguo za kiraia, lakini mbele yangu niliona kama wafungwa na mahabusu 15 pekee wote wakiwa bize kufanya shughuli hii ama ile pale jikoni.

Ila mkono wangu wa kulia kulikuwa na liukuta likubwa sana la mawe lenye mlango mdogo ambao ulikuwa wazi.

Nikarudisha tena macho yangu kwenye 'jiko'. Moshi mzito wa kuni ulikuwa unatoka na kutengeneza kama wingu zito na 'wapishi' wenyewe walikuwa hawajali, inaonekana wamezoea hali hii. Walikuwa wanakohoa na kuendelea na wanachokifanya.

Nikajiuliza tena. Wafungwa na mahabusu wako wapi.

"Hahahahahah siamini macho yangu"

Nikasikia mtu upande wangu wa Julia anacheka. Nikageuka kumuangalia.

Godi.

"Siamini macho yangu kama umekuja huku"

Godi akaongea na kunifuata mpaka pale nilipokuwa nimesimama.

"Nilikuwaa yard huko, niliposikia watu wamerudi kutoka mahakamani, nikasema ngoja nije nione kama kuna mgeni na kama yuko ninaye mfahamu, lakini sikutegemea uwe ni wewe aisee hahahah"

Godi akaongea na alikuwa ameshafika pale nilipokuwa nimesimama.

"Karibu sana gerezani, jisikie uko nyumbani!"

"Asante, ila nyumbani kwetu hakuna jiko la namna hii kama tuko karne ya 18" nikamjibu kwa utani huku namuonyesha kidole kule jikoni.

"Ooohh usijali kila mtu siku ya kwanza analionaga hilo jiko lina kera kama liko miaka 100 nyuma lakini baada ya wiki tu utaanza kuliona kama Sheraton" Godi akaongea huku anatabasamu.

"Wafungwa wako wapi? Mbona sioni mtu zaidi ya wale jikoni sijui ndio wapishi" Nikamuuliza.

"Ooh hili eneo haliruhusiwi kukaa mida hii. Wafungwa wote na mahabusu wako yard mda huu" akaongea akinionyesha kidole kile kimlango kidogo kwenye lile liukuta likubwa mkono wetu wa kulia.
"Ile pale unayoiona" akanyoosha kidole moja vyumba vikubwa vile kama 'hall' mkono wetu wa kushoto, "ile ni selo 'namba moja kubwa' au tunaiutaga reception. Humo wanalala wagonjwa wa akili lakini pia na wageni kama nyinyi mkija siku za kwanza kwanza. So nisipofanya miujiza yangu leo maana yake utapangiwa kulala mle."

Akaongea huku anatabasamu kwa kujidai.

"Ile pale ni 'selo namba mbili kubwa'" akaoonya kidole kwenye chumba kikubwa sana kati ya vile vitatu.
"Hii tunaiita 'selo ya waislamu'. Hii ndio moja ya selo za kistaarabu zaidi lakini wanaolala humo wengi ni waislamu so kila mda wa swala inabidi mjumuike kuswali"
Akanielezea huku tumeanza kutembea kuelekea kwenye kile kimlango kidogo kwenye liukuta likubwa.

"Ile pale ni 'selo namba tatu kubwa' au tunaiita selo ya walokole" akanionyesha chumba kikubwa cha Tatu ambacho kimepakana na jiko.
"Humo wanaolala wengi ni walokole, kwahiyo usiku mapambio kwa sana na kunena kwa lugha hahahah" akaongea huku anacheka. Tulikuwa tume karibia kabisa kile kimlango kwenye liukuta.

"Hizo selo nilizokuonyesha kila moja wanalala wafungwa kama 40 hivi, lakini pia huku yard tunakoenda kuna 'selo ndogo' kama 70 hivi na kila selo moja wanalala wafungwa watano"
Akanieleza na tulikuwa tumefika kwenye kile kimlango kwenye liukuta.

Tukaingia kwenye kile kimlango na kutokea upande wa pili.

Kulikuwa na kama uwanja mkubwa ambao chini pia ulikuwa na sakafu ya zege. Uwanja huu ulikuwa umezungukwa na vyumba vidogo vidogo vilivyo ungana na kutengeneza umbo la 'U'. Lakini kwa hesabu ya haraka haraka vile vyumba vilikuwa havifiki sabini kama Godi alivyonieleza.

"Hii ni yard ya kwanza! Ya pili iko nyuma huko" akaongea akinionyesha ishara kuwa nyuma ya msululu wa selo zilizo kuwa mbele yetu kuna yard nyingine.

Katikati ya huu uwanja uliozungukwa na selo, au yard kama wenyewe wanavyoita humu gerezani, kulikuwa na mwembe mkubwa katikati. Nikakumbuka huu ni moja ya miembe ambayo inaonekana ukiwa nje ya gereza.

Kuna watu kadhaa walikuwa wameketi kuzunguka huu mwembe. Kuna mzee mmoja wa makamo nilimuona yeye kuna vitu anashona shona na sindano ya mkono, siku za baadae nikaja kuelewa kuwa ndio alikuwa "fundi cherehani" wa gereza ingawa hakuwa na cherehani.

Pembeni yake walikuwa wameketi wafungwa kadhaa wanacheza drafti.

Sehemu ya mbele kabisa ya hii yard kulikuwa na televisheni imewekwa juu ya meza na kulikuwa na wafungwa wengi wamejikusanya wamekaa chini sakafuni wanaangalia.

Katika kila karibia mlango wa hizi selo ambazo zote niliona zilikuwa zimefungwa, kulikuwa na wafungwa wamekaa chini wanapiga stori.
Kitu kingine nilichokigundua kwa haraka kwenye hizi selo ni kwamba hazikuwa na madirisha.

Zilikuwa na milango ya Chuma iliyopakwa rangi ya kijani na katika hiyo milango ndio kulikuwa na vidirisha vidogo sana.

Nyuma kabisa ya hii yard kulikuwa na wafungwa na mahabusu ambao kwa muonekano walikuwa ni 'mabandidu' haswa wamekalia ndoo za maji wanapiga stori na baadhi yao 'wanatuchora' mimi na Godi anavyoniongoza kwenye hii 'tour'.

Tukaondoka kutoka kwenye hii yard na kwenda kuangalia yard nyingine ambayo iko kwa nyuma.

Tukaenda mpaka nyuma kabisa ya yard walipokaa wale 'mabandidu' kuna uchochoro mpana sana ambao pia unatumika kama 'bafu' tukapita hapo na kutokea yard ya pili iliyoko nyuma.

Hii ilikuwa inafanana kabisa na ile yard ya kwanza. Ilikuwa na uwanja mpana wenye sakafu ya zege, katikati kulikuwa na mwembe mkubwa. Pia, Selo za vyumba vidogo vidogo vilivyoungana kutengeneza umbo la herufi 'U'.

Lakini yard hii haikuwa na televisheni kule mbele. Badala yake pale mbele kulikuwa na ukuta wenye geti la kijani.

"Kule kuna nini?" Nikamuuliza Godi nikimuonyesha ule ukuta mbele ya yard wenye geti.

"Ooh kule ni kondemu (condemn)"
"Kama ikitokea mahabusu akihukumiwa kifungo cha maisha au kunyongwa, anatengwa na mahabusu na wafungwa wengine unao waona hapa. Anafungiwa kule ndani kwenye lile geti unaloliona, ndani yake kuna selo kama tano hivi. Kwahiyo anakuwa anahifadhiwa humo mpaka atakapokuja kuchukuliwa kupelekwa kwenye gereza lao maalumu liko dodoma linaitwa Isanga."
Godi akanieleza huku tuna tembea tembea pale kwenye yard.

"Kwahiyo ikitokea hakuna aliyehukumiwa kifungo cha maisha au kunyongwa, hizo selo zinakaa hivyo tu hata mwaka mzima?" Nikamuuliza.

"Hapana! Pia huwa wanawahifadhi mahabusu na wafungwa maalumu! Uliwahi kusikia wale watu waliokamatwa kilombero wakihusishwa na ugaidi kwamba wameweka kambi msituni wanajifunza ugaidi?" Akaniuliza.

"Yes! Nakumbuka nilisikiaga" nikamjibu.

"Sasa mahabusu maalumu kama hao ambao hawatakiwi wachanganyike na wengine wanawekwa kule kondemu. Pia kuna mahabusu kama hawa akina shehe Juma Kassim pia wanawekwaga huko"

Akanieleza akinipa mfano wa sheikh Juma Kasimu ambaye mihadhara yake imekuwa ikimfanya aingie kwenye mgogoro na serikali mara kwa mara na kumfanya awe na kesi mfululizo zisizoisha. Kiasi nikawa nimemuelewa Godi anachonieleza.

"Vipi umekujaje humu mwenzangu?" Godi akanieleza huku tunatembea tembea pale yard.

"Kujaje kivipi?" Nikamuuliza.

"Hujaficha hata hela kidogo kuingia nayo?"

Akaniuliza. Lakini alipotaja kuhusu kuficha hela nikakumbuka karatasi 'niliyoficha'.

"Hapana sijaficha hela yoyote! Kwani tunahitaji hela humu? Maana sijaona duka wala soko! Alafu tumbo silielewi elewi hebu nielekeze chooni" Nikamjibu huku nikidanganya kutaka kwenda kujisaidia ili nikatoe ile karatasi niliyoificha.

"Unahitaji hela humu kuliko unavyohitaji oksijeni! Na hiyo haja yako hebu ibane mpaka tukiingia selo kulala! Vyoo vya nje huku majanga tupu, kwanza vichafu alafu na hivi wanakujua mgeni wanaweza kukuweka mtu kati wakakufanyia kitu mbaya"
Godi akaongea huku anapepesa macho pale yard huku na huko kama kuna mtu anamtafuta.

"Mpaka mda wa kulala? Yani nikae na haja mpaka usiku mda wa kulala? Acha utani?" Nikamjibu kwa mshangao nikishangazwa na na pendekezo lake ati nisubiri mda wa kulala.

"Hahahaha! Humu kulala ni saa kumi kijana, na kwa makisio hii inakaribia kabisa saa tisa" akanijibu bila kuniangalia huku anaendelea kupepesa macho pale kwenye yard.

"Jesus Christ! Saa kumi? Hata usingizi unakuja kweli? Unatafuta nini alafu mbona unatazama tazama?"

"Nimekumbuka inabidi nifanye miujiza yangu tupate sehemu nzuri ya kulala. Hebu nisubiri hapa nakuja dakika sifuri!" Akaongea akinionyesha nikae chini kwenye mwembe kisha akaondoka kulekea yard ya kwanza kule tuliyotoka.

Nikakaa chini kwenye sakafu ya zege pale kwenye mwembe.

Nikatafakari mambo kadha wa kadha. Jambo moja ambalo lilikuwa linanitatiza kichwani ni kwamba tumetembea kwenye yard zote mbili lakini sikufanikiwa kumuona Eric Kaburu. Kwanini? Yuko wapi?
Kingine kilichonitatiza ni jinsi gani nitakavyoweza kumshawishi anipe siri nzito ambazo naamini kuwa anazo kuhusu The Board. Hivi nikionana naye nitamweleza kitu gani?
Nikawaza pia kama Isaack na Cheupe wataweza kupata kitu chochote kwenye uchunguzi wao wa Kaburu ambacho kitaweza kunisaidia kumshawishi aongee na mimi.
Pia nikawaza hiki kikaratasi nilichopewa na Baba bite kinahusu nini??

Nikawaza na kuwaza.

Nikaanza kumuwaza Cheupe wangu. Ni Mungu pekee ndiye anajua kiasi nilichommiss.. Nilitamani nimchukue twende tukaishi kwenye sayari nyingine kabisa kuepuka hizi heka heka, migogoro na mkanganyiko.
Dammmnn nimemiss Cheupe wangu.
Nikafumba macho kwa hisia kumuwaza cheupe.

"Oyo! Twende huku!" Godi alinishtua kutoka kwenye kutafakari kwangu.

Nikainuka na kumfuata. Tukaelekea mpaka kwenye uchochoro ule mpana tuliotumia kuingilia huku yard ya pili.

Hapo tukamkuta jamaa fulani hivi mrefu na ana mwili mkubwa wa mazoezi. Alikuwa amevaa Nguo za kifungwa lakini tofauti na wafungwa wengine yeye alikuwa na mkanda kiunoni.
Ingawa hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia gerezani lakini nikaelewa kuwa huyu atakuwa ni Nyapala.

"Huyu ndo mwenzako?" jamaa akauliza kitemi.

"Ndio huyu" Godi akamjibu.

"Kwahiyo mnataka selo namba mbili kubwa si ndio?" Akaukiza tena.

"Ndio hivyo Mkuu" Godi akajibu tena kistaarabj tofauti kabisa na kawaida yake.

Jamaa hakuongea tena chochote. Mkononi alikuwa na kifuko fulani hivi cheusi. Akatoa vipande kadhaa vya sabuni akanikabidhi mimi vitano Godi akampa vitano.

Sasa wadogo zangu ole wenu hiyo jumapili nisipate hiyo elfu kumi ndio mtajua uchungu wa jela" jamaa akaongea serious huku anaondoka.

"Utapata mkuu usijali" Godi akajibu tena kistaarabu kabisa kiasi sijawahi kumuona.

Tukaondoka tena na kurudi yard ya pili.

"Whaaaatt!! Are you crazy?? Tunaitoa wapi hiyo elfu kumi sina hata shilingi mia" nikammaindi.

"Wewe nawe hebu niachie vingereza vyako, ndio uchekeche akili sasa ujue tunaipataje?" Godi akanijibu kwa kutojali hatari ya alichokifanya kama kawaida yake.

"Kwanza sabuni zote hizi za nini umemwambia atupe? Mimi sihitaji sabuni zote hizi nguo pekee nilizonazo ni hizi nilizo vaa, misabuni yote hii ya nini?" Nikaongea kwa kekereka.

"Acha ubwege. Hizo sabuni ni sawa na hela humu! Humu jela unanunua kitu kwa kutumia hela yenyewe au unatumia sabuni. Mfano hapa wote hatujala tumechelewa msosi wa jela umetupita, so itabidi tufanye mpango baadae tutumie sabuni kadhaa kununua belenge moja la ugali.!" Godi akaongea.

"Belenge? Ndio kitu gani"

"Tuliza mshono mtoto wa kike! Utaona hapo hapo"

"***!"

"Mwenyewe"

Tukajikuta tunacheka tu na ile taharuki ikayeyuka. Tukaendelea kidogo na stori, mara ghafla tukamuona yule nyapala anapita anapayuka….

"Kaba selooooooooo! Kaba selooooooooo"

Watu wakaanza kunyanyuka na kutembea haraka haraka huku na huku.

"Muda wa kulala huo!" Godi akaongea huku anatabsamu.

"Ndio inaitwa 'kaba selo'" nikamuuliza huku nanyanyuka.

"Yeah! Ukisikia wanatangaza 'kaba selooooo' unatakiwa ukasimame mbele ya selo yako." Godi akaongea huku anamuigiza kikomedi yule nyapala anavyopayuka 'kaba selooooo'.

Tukainuka na kuelekea yard ya kwanza kisha tukatoka na kile kimlango kidogo mpaka upande uke mwingine wa gereza wenye jiko.

Kwa mujibu wa Godi hapa ndipo wageni inabidi msubirie nyapala aje kuwapangia selo ya kulala.

Wafungwa na mahabusu ambao walikuwa wanalala kwenye 'selo kubwa' zilizoko upande huu wa gereza nao tuliwakuta wamejipanga nje ya selo zao namba moja kubwa, mbili kubwa na selo namba tatu kubwa. Wote walikuwa wamevua mashati na kuchuchumaa.

Kama dakika kumi baadae yule nyapala akaja pale tuliposimama na kutuambia twende selo namba mbili kubwa.
Hakukumbusha chochote kuhusu 'hela yake' Godi aliyoahidi jumapili tutampa. Alituongelesha kana kwamba hatujaongea kabisa hapo kabla.

Tukaenda kupanga mstari na kuchuchumaa nje ya selo namba mbili kubwa tukiwa tumevua mashati kama wenzetu.

Tukiwa tumechuchumaa pale pale chini nikaona nimuulize Godi swali lililokuwa linanitatiza kichwani.

"Oi! Kuna mtu nimejaribu kupepesa sana macho lakini sijamuona na nina fahamu yuko gereza hili"

"Nani?" Godi akaniuliza.

"Eric Kaburu" nikamjibu.

Godi hakusema chochote akabakia kimya tu.

"Yupo humu kweli?" Nikamuuliza.

"Yupo! Una shida naye gani?" Godi akajibu bila uchangamfu na kwa kiasi fulani alikuwa na wasi wasi kwa mbali.

"Nimeuliza tu" nikamjibu.

Hakusema chochote. Akakaa kimya tu. Ila nilihisi jinsi hofu fulani ilivyomuingia nilipomtajia jina la Eric Kaburu.

Kule mbele ya mstari askari magereza alikuwa anatuhesabu na kisha ukishahesabiwa unainuka unaingia ndani ya selo. Ni kama vile ng'ombe wanavyohesabiwa jioni wakirudi zizini.

Nami nikahesabiwa. Nikasimama na kuingia ndani ya selo.

Siku ilikuwa imeisha. Sasa yanipasa niwe na mkakati wa kumsaka Eric Kaburu kesho na nijaribu kuzungumza naye.
Sikujua kwanini lakini ile hofu niliyoiona usoni kwa Godi nilipomtajia jina la Eric Kaburu, ilinitisha. Nikamuomba Mungu awe nami.


Itaendelea Jumanne Ijayo..

Join my exclusive whatsapp group kusoma simulizi na makala kila siku - 0718 096 811 (kuna "sbscription fee")
 
NEW EPISODE (EPISODE 10) POST # 3176



Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici T-@mij TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu
 
hii ya kuleta one episode per week inanikumbusha zamani wakati tunasubiri Kaole na kidedea... haha so kwa sisi vijana wa zamani kiukweli unatukumbusha Enzi...[emoji23]
Halafu ni dakika 45 kama sio 30 ..


Enzi hizo kama hujaangalia mchezo, basi jumamosi yako inakua mbaaya sana !! [emoji23] [emoji23]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom