Vipaumbele 9 vilivyowasilishwa na Waziri Ulega Bungeni kuhusu Wizara ya Mifugo na Uvuvi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1683056262665.png

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amewasilisha BAJETI ya Wizara hiyo Bungeni Leo Mei 02, 2023, huku hatua kadhaa zenye lengo la kuifanya iwe na mchango zaidi kwenye Pato la Taifa (GDP) na kupambana na umasikini kwa wafugaji na wavuvi zikitangazwa.

Waziri Abdallah Ulega, amesema kwamba hatua kadhaa zikiwemo za kuongeza ukubwa wa soko la nyama na samaki ndani na nje ya nchi, ufugaji wa kisasa wenye faida zaidi kwa wafugaji, kuongeza malisho ya wanyama na samaki na kuongeza usimamizi wa sekta ya uvuvi zina lengo la kuongeza mchango wa wizara yake kwenye pato la taifa na kupunguza umasikini nchini.

"Kwa sasa, mchango wa sekta ya mifugo kwenye pato letu la taifa ni takribani asilimia saba na sekta ya uvuvi ni asilimia 1.8. Kwa ujumla wizara inachangia asilimia 8.8 ya pato letu na kwa hatua hizi tunazokwenda kuchukua kupitia bajeti hii, tunaamini mchango utakuwa mkubwa zaidi" amesema Waziri Ulega.

Tofauti na miaka ya nyuma, bajeti ya wizara hiyo mwaka huu imeibua msisimko ndani na nje ya viunga vya Bunge la Tanzania - ikitanguliwa kabla na kile kinachoitwa "Wiki ya Protini" ikimaanishamazao makuu yawizarahiyo - nyama na samaki, huku kauli mbiu ya mwaka huu, "MifugoNaUvuviNiUtajiri" ikiwa inatawala katika mitandao ya kijamii kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hii ni bajeti ya kwanza kutangazwa na Ulega akiwa Waziri kamili tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan mnamo Februari mwaka huu. Katika hotuba yake hiyo, mbunge huyo wa Mkuranga ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/2024 yenye thamani ya shilingi bilioni 295.9. Katika fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 112 kitatumika kwenye sekta ya mifugo huku shilingi bilioni 183 kikienda sekta ya uvuvi.

1683056630030.png

1683056671357.png

1683056731163.png

1683056799652.png

1683056993519.png

1683057034235.png

1683057074801.png

 

Attachments

  • Vipaumbele vya Bajeti.pdf
    1.7 MB · Views: 1
  • 1683056837999.png
    1683056837999.png
    183.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom