KERO Urasimu Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mfanya biashara ya chakula cha mifugo kama pumba na mashudu.

Ukinunua mashudu au pumba,ili kusafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine inatakiwa kuwa na kibali ambacho kinatolewa na wizara kwa kuomba kwenye mfumo wa Mifugo Integrated Management Information System(mimis) ambao ulikua introduced kwa ajili ya kurahisisha mchakato wa uombaji na upatikanaji wa vibali hivyo.

Cha ajabu ni kwamba tunaomba vibali na inachukua siku kadhaa kwa watumishi hao kupitisha na kutoa control number za kulipia badala ya kutumia masaa kadhaa au hata dakika kadhaa kama ilivyokusudiwa. Tukiwapigia simu wanajibu kwa jeuri na kiburi kama vile tunaomba msaada wakati ni wajibu wao na tunalipia. Hawatoi vibali kwa wakati na wanakua wanaringa na kutengeneza mazingira ya rushwa.

Tunaomba tupaziwe sauti washughulikiwe na wawajibike ipasavyo. Wasilete viburi na jeuri wakati ni kodi zetu ndo wamekalia hapo.
 
Back
Top Bottom