Viongozi wetu wajifunze kutoka kwa Uhuru Kenyatta

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Ni muhimu viongozi wetu wajifunze kuwa na busara wanaposhughulika na watu wanaotofautiana nao. NItaeleza.

Mnamo mwaka 2018 huko Kenya, mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2017 ambapo Uhuru Kenyatta alitangazwa kushinda kiti cha urais akimshinda mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Raila hakukubali matokeo hayo na akapinga matokeo hayo mahakamani. Mahakama ilitengua matokeo hayo na ikaamuru uchaguzi wa urais urudiwe kati ya Uhuru na Raila. Hata hivyo Raila alisusia marudio ya uchaguzi. Ndipo mnamo mwaka 2018 Raila akatangaza kuwa ataapishwa kama "Rais wa watu".

Na kweli mnamo January 2018 aliapishwa. Wakati maandalizi ya kuapishwa yalipokuwa yakiendelea, Mwanasheria Mkuu wa Kenya wa wakati huo Prof. Githu Muigai alimuonya Raila kwamba jambo analotaka kufanya ni tendo la uhaini ambalo adhabu yake ni kunyongwa.

Baada ya Raila kuapishwa na mwanasheria wake, Rais Uhuru akapata shinikizo la watu wake amkamate Raila na kumshtaki kwa kosa la uhaini. Uhuru alikataa na akawajibu "Si Raila amekwisha kuapishwa sasa baada ya kuapishwa kwani amekwenda ikulu au nyumbani kwake. Si amekwenda kwake!" Mambo yakaishia hapo. Viongozi wetu wajifunze kutumia busara.
 
Hata hivyo Kenya Iko mbali kidemokrasia. Mandamano yaliyofanyoka Kenya, ingekuwa Tanzania Odinga angeozea jera.
 
Angekuwa ndo amejiapisha Kiongozi wa Chadema Huku Tanzania mbona angekoma, Kunyongwa asingenyongwa Ila kingechomkuta kutoka kwa Policcm ingebaki Fundisho kwa ukanda huu Wa Africa Mashariki na Kati.
 
Ni muhimu viongozi wetu wajifunze kuwa na busara wanaposhughulika na watu wanaotofautiana nao. NItaeleza.

Mnamo mwaka 2018 huko Kenya, mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2017 ambapo Uhuru Kenyatta alitangazwa kushinda kiti cha urais akimshinda mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Raila hakukubali matokeo hayo na akapinga matokeo hayo mahakamani. Mahakama ilitengua matokeo hayo na ikaamuru uchaguzi wa urais urudiwe kati ya Uhuru na Raila. Hata hivyo Raila alisusia marudio ya uchaguzi. Ndipo mnamo mwaka 2018 Raila akatangaza kuwa ataapishwa kama "Rais wa watu".

Na kweli mnamo January 2018 aliapishwa. Wakati maandalizi ya kuapishwa yalipokuwa yakiendelea, Mwanasheria Mkuu wa Kenya wa wakati huo Prof. Githu Muigai alimuonya Raila kwamba jambo analotaka kufanya ni tendo la uhaini ambalo adhabu yake ni kunyongwa.

Baada ya Raila kuapishwa na mwanasheria wake, Rais Uhuru akapata shinikizo la watu wake amkamate Raila na kumshtaki kwa kosa la uhaini. Uhuru alikataa na akawajibu "Si Raila amekwisha kuapishwa sasa baada ya kuapishwa kwani amekwenda ikulu au nyumbani kwake. Si amekwenda kwake!" Mambo yakaishia hapo. Viongozi wetu wajifunze kutumia busara.
Asante! Ni kama umeniwahi kuutoa huu uzi.

Binafsi, nakubali Uhuru kama mmoja wa viongozi waliouonesha ukomavu mkubwa sana wa kisiasa kipindi cha uongozi wake.

Fikiri tu, hilo la Raila Odinga lingefanyika Tanzania kungetokea nini?
 
Back
Top Bottom