VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Jana Machi 27, shamba la familia ya Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta lilivamiwa na uharibifu pamoja na wizi kufanyika. Shambani humo moto mkubwa uliwashwa; miti ya mbao na nguzo ilikatwa na wizi wa mali mbalimbali wakiwemo mamia ya kondoo ulifanyika.
Tundu Lissu, mnamo Septemba 7, 2017 alishambuliwa kwa risasi na 'watu wasiojulikana' kulikokuwa nyumbani kwake Area D, jijini Dodoma. Lissu alipata maumivu makali na shambulio hilo limemuachia 'ulemavu' wa kudumu mwilini na akilini mwake.
Ni utaratibu wa dunia nzima kuwa makazi na mali za viongozi wakuu wastaafu kulindwa kwa namna yoyote. Hata makazi yao baada ya kustaafu hulindwa na askari wanaobadilishana zamu kila uchao. Sasa Kenyatta wawili wameshakuwa marais wa Kenya.
Ni utaratibu wa nchi yetu kuwa makazi ya Mawaziri, Ofisi ya Spika na Wabunge kule Dodoma hulindwa kila uchao kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa viongozi wetu hao. Lissu alikuwa Mbunge na alikuwa akiishi kwenye makazi yaliyokuwa na ulinzi mkali, Area D.
Wakati wa uvamizi wa shamba la Kenyatta jana hakukuwa na wala hawakufika maafisa wa usalama-kama polisi kwa ajili ya kulinda shamba hilo dhidi ya uvamizi huo. Hata Septemba 7, 2017 Area D wakati wa shambulio la Lissu haikuwa na ulinzi kama ilivyokuwa kawaida yake. Inashangaza na kutafakarisha.
Raila Odinga si wa kupuuzwa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba ( safarini Nairobi, Kenya)