Ombi kwa viongozi wetu wa Dini

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Sasa saa imefika kwa viongozi wetu wa Dini kutotenganisha Dini na Siasa.

Wakati umefika viongozi wetu wa Dini wasikubali tena kuambiwa eti Siasa haiwahusu wao kama viongozi wa Dini kwa sababu Dini inafanyika ndani ya Nchi, na Nchi inaongozwa kwa Siasa.

Kwa maana hiyo, naomba viongozi wetu wa Dini zote wasibaki nyuma kufuatilia mwenendo wa Siasa Nchini.
Tunapoelekea kwenye chaguzi zinazotukabili huko mbeleni, naomba viongozi wetu wa Dini kufuatilia kwa umakini sana mwenendo wa Siasa Nchini.

Viongozi wa Dini wanaongoza watu, kwa hiyo, ili kuwa na watu wenye ustawi mzuri tunapaswa kuwa na viongozi wa kisiasa walio wazuri, na ili kuwapata viongozi wa kisiasa walio wazuri ni lazima haki na ukweli vitawale kuanzia upatikanaji wa wagombea mpaka utangazwaji wa matokeo ya uchaguzi.

Viongozi wa Dini wasisite hata kidogo kuwaonya viongozi wetu wa Nchi pale mambo ya uchaguzi na mengineyo yanapokuwa yanakwenda mrama.
 
Back
Top Bottom