Waziri Mkuu amshauri Rais Mstaafu kujihadhari mlimani Kilimanjaro
Na Daniel Mjema,Hai
TUKIO la Rais Msaafu wa awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi kupanda Mlima Kilimanjaro linaonekana kuishtua serikali kiasi kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameshauri kuwa si lazima afike kileleni.
Kauli ya Waziri Mkuu aliitoa jana katika lango kuu la Machame wakati akimwaga rasmi Mzee Mwinyi na wapandaji wengine 45 wa Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) walioanza safari ya siku sita ya kupanda mlima huo.
Kabla hata ya Waziri Mkuu kuonyesha wasiwasi huo, hata mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mohamed Babu alisema baada ya kushauriana, serikali imeona rais huyo mstaafu asifike hadi kilele cha Uhuru.
''Tumeshauriana sana tumeona Mzee wetu asifike hadi kileleni yeye aende tu hadi hapo atakapofika arudi lakini asifike kileleni,'' alisema mkuu huyo wa mkoa. Kilele cha Uhuru ni urefu wa meta 5,895 kutoka usawa wa bahari.
Baada ya maelezo hayo ya mkuu wa mkoa,Waziri mkuu naye alisema alipopata taarifa kuwa Mzee Mwinyi anapanda mlima huo alibabaika kidogo kwa sababu Rais huyo mstaafu sasa anakaribu umri wa miaka 83.
''Lakini kama mzee Mwinyi anaweza kwanini sisi tushindwe? Lakini sio lazima ufike Kileleni hapo utakapofikia sisi bado tutakushukuru,'' alisema Waziri Pinda katika tafrija hiyo fupi ya kumwaga Mzee Mwinyi maarufu kama mzee Ruksa.
Mzee Ruksa anapanda Mlima huo kwa kuongozwa na waongoza watalii mashuhuri na wenye uzoefu, Theophill Karia na Faustine Chombo wa kampuni ya ZaraTanzania Adeventures inayomilikiwa na Zainab Ansell.
Alhaji Mwinyi mwenyewe alionekana ana hamu kubwa ya kufika hadi kileleni na alipofika eneo hilo aliwasalimia wapandaji wenzake kuwa, '' Vipi Vijana mko tayari kupanda'' nao wakasema wako imara.
Waziri mkuu alisema uzinduzi wa mwaka huu wa kupanda mlima huo kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi ni ya kipekee na yenye baraka kutokana na kuwepo kwa Mzee Mwinyi.
Pinda alisema lango analolitumia Mzee Ruksa na wapandaji wengine ndiyo njia ngumu sana na hutumiwa na wale wanaoitwa Madume wa kupanda milima hivyo akasema ujumbe anaoubeba Rais huyo mstaafu ni mzito.
''Ujumbe anaoupeleka kwa Jamii ni zaidi ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi�ni ujumbe unaotaka tujitazame upya na kuangalia ushiriki wetu katika mapambano dhidi ya Ukimwi,'' alisema Pinda.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa GGM,Hatibu Senkoro, tangu kuanzishwa kwa zoezi la kupanda mlima huo kuchangisha fedha za Ukimwi mwaka 2002, karibu Sh1bilioni zimepatikana.
Senkoro alisema lengo la mwaka huu ni kuvuka Sh300 Milioni zilizochangwa mwaka jana na kwamba fedha hizo zitatolewa kwa Asasi zinazojishughulisha na masuala ya yatima,wajane na kupambana na Ukimwi.