Viongozi watorosha Sh trilioni 16 nje!

Hapo ndipo nnapopata fursa ya kumsifu Kikwete, hii kazi aliianza na kuifanya kwa kubadilisha sheria humu ndani ya nchi zinazohusiana na utoroshaji wa fedha na rushwa, hakuishia hapo akakazania sana kuhusu sheria ya Umoja wa Mataifa itakaruhusu fedha zilizopo nje ya Afrika za Waafrika ziwekwe wazi na kurudishwa ikigundulika hazijapatikana kihalali, hata juzi juzi alilisemea sana alipokuwa Arusha kwenye mkutano wa majaji wa jumuiya madola.

Alilitilia mkazo pia walipokutana na wakuu wa kuzuia rushwa afrika mashariki.

Sasa japo tunaona manufaa ya kazi yake, angalau tunajuwa ziko ngapi hapo Uswisi tu na bado zipo nje kwingine nyingi tu na Kikwete haziachi hizo, kama alivyorudisha fedha za rada na hizi zitarudi tu.

Hapo ndipo nnapompendea Kikwete, nyie semeni yeye anafanya.

Kuwakumbusha tu kuwa kazi hii kaianza zamani na leo mna matunda yake nimewawekea links tofauti hapa chini mjikumbushe:

http://www.google.com/url?sa=t&rct=...sg=AFQjCNFvwvy_VMA6ZAlVx1gVoe4GvFP36w&cad=rja

Kenya: Kikwete calls for uniform tax system in East Africa

Zimefichuka » Blog Archive » KIKWETE'S CAMPAIGN AGAINST CORRUPTION PROMISING

Kikwete on money laundering and corruption - Google Search[+Arusha
 
Chenji zingine hizoooo!!!!Sasa naona nchi itaanza kuishi kwa chenji.kama chenji kubwa kuliko bajeti ya nchi neema imeanza
 
ama kweli tuna kobolewa ile mbaya. .... lakini kule bungeni mbona wanaonekana wote wanauchungu na raia.... wote wajidai kumtetea mnyonge..!
 
ama kweli tuna kobolewa ile mbaya. .... Lakini kule bungeni mbona wanaonekana wote wanauchungu na raia.... Wote wajidai kumtetea mnyonge..!
sasa jamani si wapunguze deni angalia trilioni 22-16= zibaki sita tu. Hawa watu hawana huruma hata chembe itafika time watapiga watu hadharani. Maana sasa wameanza kufanya kwa kificho. Ingawa wanaumbuka.

Watanzania nawaonya ukiona wanapinga kutetea wafanyakazi maanake wanaunga mkono wafanyakazi kukandamizwa. Na yeyote atakayewatetea ni lazima wadeal naye perpendicularly, diagonally, horizontally, profundally and vertically.

My take

Tuanze kufuatilia matamshi ya Lameck Mwigulu Nchemba. Alitamka mwenyewe kuwa chadema wanawaunga mkono wanaotetea haki zao na hivyo wanachochea migomo. Hivi chemba ni kwanini ulizaliwa kizazi hiki??.

Kizazi hiki mambo hadharani nina mashaka unajitenga na kujiunga na wazee ambao tayari wanasubiri kuomdoka hali wewe bado ni mtoto
 
SIRI zinazoendelea kufichuka kuhusu matrilioni ya fedha ambazo viongozi na wafanyabiashara hapa nchini wamezificha katika benki nje ya nchi sasa zimeanza kutoa mwanga na majibu kuhusu sababu hasa za Watanzania kuendelea kuwa maskini wa kutupwa ilhali nchi yao ina rasilimali nyingi na utajiri mkubwa.

Ni majibu ambayo Watanzania wamekuna vichwa kwa muda mrefu wakitaka kuyapata, huku baadhi yao wakiwa tayari wamekata tamaa kiasi cha kujenga dhana potofu kwamba pengine Mwenyezi Mungu amelaani nchi yetu, hasa baada ya baadhi ya viongozi wetu wakuu kusema kwamba nao hawajui kwa nini nchi yetu ni maskini.

Kufichuka kwa siri hizo hivi karibuni kumetufumbua macho kwamba umaskini wetu haukutokana na laana za Mwenyezi Mungu, bali ufisadi wa viongozi na kukosekana kwa utawala bora na uwajibikaji katika uendeshaji wa serikali tangu chama tawala cha CCM kilipolizika Azimio la Arusha.

Itakumbukwa kwamba wiki iliyopita siri ilifichuka kuwa, Watanzania sita wameficha zaidi ya Sh303 bilioni katika akaunti za benki mbalimbali nchini Uswisi na kwamba fedha hizo ziliwekwa katika akaunti hizo na baadhi ya makampuni ya kuchimba mafuta na gesi yanayofanya kazi hapa nchini. Na katika kuthibitisha kwamba fedha hizo ni za kifisadi, kwa maana ya kutolewa kwa lengo la kuwahonga viongozi, wenye akaunti hizo hawajaweka hata shilingi moja kwenye akaunti hizo.

Tayari zipo ripoti kadhaa za kimataifa kuhusiana na fedha zilizofichwa ughaibuni na viongozi wa nchi mbalimbali barani Afrika. Pamoja na Serikali ya Uswisi kukiri kwamba fedha za Watanzania hao sita ziko katika benki kadhaa nchini humo, hadi sasa majina ya watu hao bado hayajafahamika na Serikali haijaonyesha nia na dhamira ya kushirikiana na mamlaka za kimataifa kuwasaka na kuwatia mbaroni watu hao wenye fedha hizo chafu za kifisadi.

Kama hiyo haitoshi, juzi Bunge linalokutana mjini Dodoma lilipewa taarifa ya kushtusha kwamba viongozi na wafanyabiashara kadhaa nchini wametorosha na kuhifadhi katika benki nchi za nje fedha zipatazo Sh16.6 trilioni. Akichangia hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Rais, kwa mwaka 2012/13, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) alisema ripoti ya mwaka 2008 ya taasisi ya kimataifa inayochunguza fedha chafu kutoka barani Afrika (Global Financial Intergrity Report 2008) imebainisha kwamba Sh16.6 trilioni zimefichwa nje ya nchi na viongozi na wafanyabiashara wa hapa nchini na kuituhumu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwa, pamoja na benki hiyo kufahamu suala hilo, hadi leo haijabainisha ni za nani, ziliibwa lini, majina ya wamiliki wa fedha hizo na lini fedha hizo zitarejeshwa nchini.

Kama tulivyoeleza hapo juu, ‘siri' hizo sasa zimewafanya Watanzania wajue kwamba chanzo cha umaskini wao ni ufisadi wa viongozi na washirika wao ambao wamekuwa wakiingia katika mikataba mibovu na wawekezaji, pamoja na kutorosha fedha, maliasili na rasilimali za nchi yetu kwenda nchi za nje. Kwa mfano, Sh16.6 trilioni zilizofichwa nje ya nchi ni kikubwa mno, kwani ni zaidi ya bajeti ya Serikali ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka mmoja wa fedha, kwani bajeti ya mwaka huu wa fedha ni Sh15 trilioni.

Huo bila shaka ni uhujumu mkubwa wa uchumi wetu, kwani fedha hizo zingebaki nchini zingesaidia uchumi wetu, kwa maana ya kuziwekeza katika sekta muhimu za maendeleo. Tunapata wakati mgumu kuelewa sababu za kupeleka fedha nje kama kweli zimepatikana kwa njia halali, kwani kama ni kutafuta fedha za kigeni tayari tuna benki za kigeni hapa nchini.

Matokeo ni kwamba fedha zetu zinajenga uchumi wa nchi nyingine, zikiwamo nchi tajiri sana duniani. Haya ni matokeo ya viongozi wetu kukosa uzalendo na kukumbatia ufisadi. Tunaishauri Serikali ihakikishe fedha hizo na nyingine ambazo hazijabainishwa zinarejeshwa nchini na wahusika wote wanawajibishwa kisheria.


CHANZO:
Serikali irudishe Sh16 trilioni zilizofichwa ughaibuni
 
Back
Top Bottom