Viongozi watorosha Sh trilioni 16 nje! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi watorosha Sh trilioni 16 nje!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Janja PORI, Jul 4, 2012.

 1. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  VIONGOZI na wafanyabiashara nchini, wameelezwa kutorosha na kuhifadhi fedha nje ya nchi kiasi cha Sh trilioni 16.6 fedha ambazo zinazidi bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13.

  Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) alisema hayo bungeni jana wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Tume ya Mipango kwa mwaka 2012/13 na kuituhumu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwa inajua fedha zote zilizofichwa na Watanzania nje ya nchi.

  Mpina mbali na kuituhumu BoT kufahamu fedha hizo zilipo, alisema Benki Kuu ya Uswisi imekiri sehemu ya fedha hizo kuhifadhiwa katika benki za nchi hiyo na Watanzania sita.

  "Taasisi ya Global Financial ilibainisha kuwa Sh trilioni 16.6 zimefichwa nje ya nchi na viongozi na wafanyabiashara wa nchini na Benki Kuu ya Uswisi imesema Sh bilioni 315 ziko nchini mwao zimefichwa na watu sita.

  "Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inajua fedha za Watanzania zilizo nje ya nchi, lakini hadi leo hawajatwambia ni za nani, ziliibwa lini na zitarejeshwa lini! Mbali na kufichwa kwa fedha hizo, Mpina alisema pia kwamba Tanzania inapoteza Sh bilioni 478 kila mwaka, zaidi ya nusu ya Bajeti ya Zanzibar kutokana na fedha hizo kufichwa katika benki za nje ya nchi.

  Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM), akichangia hotuba hiyo, alishauri uundwe Mfuko wa Dharura wa kulipa madai ya watumishi ikiwamo malimbikizo ya mishahara yao ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara.

  Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu (CCM), aliitaka Serikali itangaze nyongeza ya mshahara mapema kama ilivyokuwa zamani ili watumishi wajipange na si kama inavyofanya sasa kuwa siri.

  Mbunge wa Korogwe Mjini, Yusuf Nassir (CCM) alisema katika leseni 28 zilizotolewa na Serikali za utafutaji gesi, hakuna Mtanzania anayefanya kazi hata katika ngazi za chini na taarifa ya mwekezaji ndiyo inapewa Serikali kitendo ambacho si sahihi.


  CHANZO: HabariLeo
   
 2. Muce

  Muce Senior Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duuuh kweli TZ ni nchi ya mafununu, kwa pesa hizo zote kama zingetumika ipasavyo kungekuwa na migomo? Serikali isitutanie irudishe hela hizo halafu wakamilishe madai ya watumishi wake, tuone kama kutakuwa na mgomo tena.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  gazeti la HABARI LEO LIMERIPOTI FRONT PAGE,MWENYE UWEZO AILETE HABAR HAPA,
   
 4. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  bora maana humu ndani kuna watu wabishi sijui nao wapo kwenye Bajeti ya billion 15 ya chai kwa ofisi ya mh baba riz
   
 5. Third Eye

  Third Eye JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaa tanzania,
  nakupenda kwa moyo woteeeeeeee
   
 6. paty

  paty JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,257
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  kweli wahajamaa wanatafuna mapesa yetu - mpaka tukija kufunguka watakuwa wamemaliza kila kitu na kukimbia nchi
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Sishangai... Nilipoanzisha hii thread (Secrets of Swiss Banking) mwaka 2008 sikueleweka, wengine hata HAWAKUIJALI, hawakuangalia hata tip niliyoweka!
   
 8. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nchi hii ina mambo ya kutia aibu sana. Huwa nashangaa sana watu kama Ritz, Zomba na hayawani wengine kutetea udhaliumu huu.
   
 9. Asu tz

  Asu tz JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  loading..........5% Netwok failed
   
 10. S

  SILVANUS NJENGA Senior Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli Tz ni zaidi ya tuhijuavyo.

  Wachache wataendelea kuifaidi na Wengi tutaendelea na kuzidi kuumia tu.

  Pesa zote hizi wajanja wanawapora wa-tz na hakuna hatua zinazo chukuliwa na mamlaka husika, alafu tunaenda tena kuomba misaada ya kipesa tena kwa wazungu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Kama mfumo wa maisha umekubalika kuwa huu yaan wa viongozi kujinufahisha kwa kutumia nafasi zao na wasiokuwa na nafasi muhimu ktk ofsi za umma kuzidi kutoa macho tu, basi hatima ya tanzania si tu kuwa hiko mashakani bali hatarini pia.
   
 11. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 1,375
  Trophy Points: 280
  halafu wanasema hamna hela ya kuwalipa ma-dr
   
 12. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  jamani hivi vasco amerudi kutoka italy? si nilimuona airport juzi anakwenda kumpa balotelli pole!! curapppp presidar of the century!
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280

  Mkuu Invisible juzi nilikuwa naongea na wanajeshi wa monduli walishukuru sana ile habari ya Shimbo kwani matokeo yke walinufaika sana baada ya taarifa hizo ambazo zilianzia JF, kuwa baada ya taarifa hizo vikao vya kuwahusisha hasa askari waliokuwa wameenda sehemu husika vilikuwa haviishi kuwabambeleza eti wazipuuze zile taarifa na baada ya muda waligawiwa pikipiki kila mmoja ili kuwanyamazisha na wao walitafsiri kuwa ni kutokana na habari hizo.. je kati ya hizo trilioni 16 na za Abdalah Shimbo nazo zipo humo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Juzi alikuwa anaenda kula bata kwa kagame kama sikosei maana kulikuwa na maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Rwanda...Hatuana raisi tuna mtarii tu....
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  tupe link yake tuipitie, wengine tumekuwa member hivi karibuni. tusaidie tuisome.
   
 16. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  baada ya kula bata Rwanda huyooooo akapaa zake hadi Burundi kwenye sherehe nyingine, hapo akapewa tuzo kwaniaba ya hayati baba wa taifa. Mawazo mwake nadhani aliwaza hivi: Nami nitapata tuzo siku moja...yaani hata ile ya oscar au ya kola itakosa kweli?
   
 17. k

  kalcha Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  dah, napata shaka ya hizo pesa kurudi! waliotorosha ndo viongozi wa serikali, sa watarudishaje? labda kimya kimya! then utasikia zimeelekezwa kwenye elimu sijui maji, au afya ingawa hakuna mabadiliko ya maana tunayoweza shuhudia! tuache lomolomo! tuitoe hii serikali dhalimu madarakani, tuunde nchi nyingine yenye fikra na utendaji makini kwa manufaa ya wananchi
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wala hakuna vifaa vya x rays na ct scan...
   
 19. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  tupia thread tena mkuu tufanye utatuzi
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kikwete akose hata ya raisi alie safiri kuliko ma-raisi wote duniani hapo nitaandamano...
   
Loading...