MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 850
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akionekana katika Sare zake za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).Picha hii inatajwa kupigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 80 wakati huo Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Jeshini.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anne Simamba Makinda. Picha hii ilipigwa Mwaka 1994 wakati Mama Anne Semamba Makinda akiwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.
Pichani ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda (wa Kwanza Kushoto) akiwa pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Bwana Christopher Ole Sendeka (Wa pili kushoto), Aliyekuwa Mkuu wa Mikoa Mbalimbali hapa Nchini, Bwana Ditopile Ukiwaona Mzuzuri (wa tatu kushoto) na wa mwanzo upande wa kulia ni William Vangimembe Lukuvi.Picha hii ilipigwa Miaka ya 80 wakati huo Vijana hawa wakiwa ni Viongozi wa Jumuia ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi.