Viongozi wa juu CHADEMA watofautiana

Viongozi wa juu CHADEMA watofautiana

Viongozi watofautiana that organisation conflicy inaruhusiws. Kosa kulizungumzia pale "conflict'
 
CCM ndo mnaomuwinda ZITTO, lengo lenu mumchonganishe na viongozi wenzake katika hili LENGO LENU KUBWA NI KUONA CDM INAANGUKA hili limeshajulikana ndani ya cdm. Zito mwenyewe keshasema TUSHIKAMANE WANACHADEMA, vita ni kubwa kwa sasa.

Mkuu CCM hawamuwindi ZITTO ila wanamtumia kwa umakini na ustaadi mkubwa sana na yeye analijua hilo kwa sisi wenye weredi mkubwa wa kuchambua mambo tunaliona hilo na ndo maana agombei tena Ubunge kwani anajua nini anakifanya juu ya kuiangamiza CHADEMA chama anachosema anakipienda sana.
 
nadhani chadema kwa sasa inatakiwa sana kuangalia mwendeno wa chama kindani zaidi na isipuuze matukio km haya ndani ya chama,kwani viongozi wengi wakisimama huwa wanaonekana kukataa kuwa kuna mgawanyiko ndani ya chadema tofauti na vyama vingine ambavyo huwa wanakubali, sasa hili kwa chadema linaweza kwua bomu kubwa kwa baadae hasa pale makundi(km yapo)yatakaposhindwa kuvumiliana nakuamu kuweka mambo hadharani, suala la kamanda ZITTO kuonekana hana mahusianao na viongozi wenzake halijaanza ss,hivyo basi ni vyema wakewekana sawa kuliko kila mmoja kutaka kuwaonyesha wanachama kuwa fulani tatizo, mfano suala la LAKWATARE,inaoneka hapo MBOWE kavujisha habari ya barua ili kuweka zitto pabaya kwa wanachama,kuna suala la kugombea nafasi ya uraisi nalo lipo,suala la ZITTO kusema kutaka kuuwawa, namengine, yote haya viongozi wanakanusha kwa nje ila wao wanajua hasa ndani kuna nini.
ushauri wangu chadema wawe waangalifu sana la sivyo chama kinaweza kugawanyika na wasijue pa kushika.
 
Bandiko lililoenda shule kwa kuchanganua mambo kwa kina na kuuliza maswali ya msingi. Shukurani Mkuu Lukolo.
....Mkuu maswali ya msingi yako mengi...inategemea upande uliopo...wa utetezi... au....wa mashtaka
 
Kuna wanandoa wawili walikwenda kuomba ushauri juu ya MGOGORO uliokuwepo kwenye ndoa yao, Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:-
MSHAURI...Mkeo ameshakuja mara nyingi kulalamika juu ya mgogoro uliopo kwenye ndoa yenu
(mume huku akichekacheka)
MUME......Hiyo sio kweli..tunatofautiana kidogo tu..wala hakupaswa kuja kuripoti huku..
MSHAURI..Mawasiliano kwa wanandoa ndio muarobaini wa tatizo lolote ndani ya ndoa...
(mume akadakia)
MUME......Hilo ndio tatizo la mke wangu...kwa mfano jana usiku niliacha ujumbe mezani kuwa nitakuwa na
wageni...leo niliporudi na wageni..nakuta hajaandaa chochote...nilipomuuliza anasema hakuona huo
ujumbe...ina maana hakufanya usafi sebuleni ?
(jamaa alihoji kwa ukali )

Kama kwa mtazamo wako huu sio mgogoro ( KUTOFAUTIANA) basi pia hao viongozi wa chadomo hawatofautiani.

ZITO ANATUMIA BARUA KUWASILIANA NA VIONGOZI WENZAKE.....mmmmmmh
 
Mbowe alisema ikidhihirika Lwakatare amerekodi basi awajibishwe.

Imedhihirika kuwa ni KWELI Lwakatare alirekodiwa na Tundu Lissu anamjua mpaka aliyemrekodi Lwakatare. Mbowe huyohuyo anawaambia kuwa sasa asiwajibishwe.

Hii ni kwa sababu Mbowe kashajua kuwa vijana mnalaghaika kirahisi.

Usilaghaike - Uamuzi ni wako...

Mimi ninavyojua lwekatare bado ni mtuhumiwa na anastahili haki zake zote mbele ya sharia,CDM awawezi kumuhukumu sasa kabla ya mahakama,ndio maana mh zitto katoa maoni kuwa chama kifanye uchunguzi wake wa dani alafu ikibainika hatua stahiki zipo,kwa sasa mh mbowe alichosema ndio yaliyofikiwa katika vikao ndani ya chadema,ndani ya chadema kuna wasomi wakubwa na maamuzi yote yanafikiwa baada ya majadiliano wapo akina prof safari,dr kitilya,tindu lissu,marando,zitto jamani hawa watu na wengine wengi ndani ya kamati kuu awaburuziki
 
Kwani mtu kujiuzuru ni kuadhibiwa?

Mbona Lowassa aliwajibika wakati akiwa "mtuhumiwa"?
 
Jamani wanachadema wenzangu tusipoteze muda kwa hoja dhaifu namna hii.bila shaka mawakala wa ccm ndani ya chadema tunawajua.mwanachadema makini lazima anajua kuwa jamaa mmoja kutoka k.g ni pandikizi la nguvu.limeshanunuliwa na mafisadi.naunga mkono kauli za mh freeman mbowe zaidi ya 100%
 
Kwani mtu kujiuzuru ni kuadhibiwa?

Mbona Lowassa aliwajibika wakati akiwa "mtuhumiwa"?

Mkuu tofautisha ishu ya lowasa na lwekatare,lowasa tayari bunge lilimtia hatiani kwa kushindwa kuwajibika na kuisababishia serikali kuingia katika mkataba tata,tena bunge likaagiza na wengine nao wachukuliwe hatua za kinidhamu,ila kamati kuu ya ccm baadaye ikamsafisha kwa kusema kuwa hakuwa na hatia yoyote ila aliwajibika kisiasa kulinda heshima yake na chama chake(je,wewe unaamini ni kweli?)lakini mh lwekatare yeye ameshitakiwa mahakamani,kwa kosa la jinai,wakati ukifika atawajibika tu kwa kuiacha nafasi aliyonayo katika chama.kwa sasa akifanya hivyo italeta tafsiri mbaya kwa jamii,pia na chama pia.Pia katika hali ya kawaida ata kama mahakama itamkuta hana hatia ni lazima ataondoka kwani anakosa credibility ya kuwa mkuu wa usalama katika chama
 
Hivi ni lini Bunge lilianza kuwa chombo cha kutoa hukumu?

Na hata kingekuwa chombo cha kutoa hukumu, umeshawahi kuona wapi mtu anahukumiwa bila kupewa fursa ya kujieleza?
 
Back
Top Bottom