baunsa nyoka
Member
- Apr 16, 2015
- 19
- 0
hahahaHao Wtumishi wa Mungu wamshukuru Mungu hicho kikao Lissu hakuhudhuria, wasingesikilizwa.
hahahaHao Wtumishi wa Mungu wamshukuru Mungu hicho kikao Lissu hakuhudhuria, wasingesikilizwa.
Kwa ujumla Tundu Lissu hatukani mtu, bali hana nafasi ya kumrembea mnafiki bila kujali nafasi yake katika jamii. Kama wewe ni mnafiki basi Tundu Lissu hakulazi na mkopo bali na cash tu.
Ndugu yangu , Septemba mosi utashiriki??????
Ha ha ha haaaaaaaaaaa! Aisee. Hawa wapinzani kweli wachumia matumbo. Walishapiga mahesabu kwamba kitakachofuata Kama hawatarudi mjengoni Ni kufutiwa posho zote na mshahara - JPM akikohoa tu "futa mshahara na posho zao" ndio imetoka hiyoWakirudi watakuwa wamenyooka na yale maplasta yao sasa wameyatupa huko jalalani.
Duh umeona mbali.Ha ha ha haaaaaaaaaaa! Aisee. Hawa wapinzani kweli wachumia matumbo. Walishapiga mahesabu kwamba kitakachofuata Kama hawatarudi mjengoni Ni kufutiwa posho zote na mshahara - JPM akikohoa tu "futa mshahara na posho zao" ndio imetoka hiyo
Kwa bahati mbaya mimi huwa sishiriki maandamano ya aina yoyote wala sijawahi kushiriki maana hapa jukwaani maoni yangu yanajitosheleza. Kuna mbinu nyingi sana za kufikisha ujumbe na kila mtu anatumia mbinu yake ili kufikia lengo. Halafu kwenye hizi nchi zetu za kiafrika maandamano ya kuipa changamoto serekali huwa kuna ukiukwaji mkubwa sana wa haki za binadamu kwa sababu viongozi wetu wengi wa kiafrika huwa hawawajibiki kwa wananchi wao bali vyama vyao na maslahi yao binafsi. Kwa hiyo kwao sifa kubwa ni kuhakikisha wanawauwa ama kuwaumiza waandamanaji na wala sio kufanyia kazi kinacholalamikiwa. Na kwa sehemu kubwa huwa hawana majibu ya kinacholalamikiwa hivyo namna pekee ni kuwauwa waandamanaji kama sehemu ya kujibu matwaka yao.
Nimeyapenda maelezo yako Ndugu yangu...isipokuwa katika suala la kuwaumiza na hata kuwaua waandamanaji, kasoro hii haiko kwa viongozi wa Afrika peke yake...hata ulaya ukiandamana na kuleta fujo unauawa, na ukiuawa utaambiwa wewe ni 'terrorist'...huko Marekani weusi wanaoandamana nao huuawa kama wanyama kwa kupigwa risasi...Kwa ufupi viongozi wa ulaya wanafanya mambo ya kinyama kuliko hata viongozi wa Afrika, lakini sisi tunaaminishwa kuwa viongozi wa Afrika eti ndio ambao hawajui au hawazingatii demokrasia....hizi ni propaganda tu, wazungu pia ni wakatili sana...angalia mauaji ya huko Kosovo, Serbia na kadhalika namna walivyokuwa wakiuana yaani walikuwa wanaua mithili ya wanyama kabisa yaani hata yule 'Kony' wa Uganda anaweza kuonekana kuwa ni 'malaika'...Angalia huko Marekani namna Wamarekani weusi wanavyouawa, ni hatari...wiki chache zilizopita huko Marekani polisi wapatao watano waliuawa kinyama sawa na kilichotokea kwetu huko Mbande....
Msimwingize mod kwenye malumbano, hiyo picha n ya Lissu baada ya kushinda mahakamani akitetea ubunge wake.Mods tupieni macho hiyo kitu.
Anawezaje kuweka kitu ambacho ni irrelevant?
Hapo Tundu Lissu alikuwa kwenye msiba wa dada yake, huyo Mleta post anatoa tafsiri nyingine kabisa....
Mkuu hiyo ulaya unayoitaja wewe ya Eastern Europe hizo nchi zilizokuwa za kisoshalist hakuna demokrasia kule. Demokrasia yetu kwa sehemu kubwa ni ya Ulaya magharibi. Ama umewahi kusikia nchi zetu zinaiga demokrasia ya kosovo, hungary, bulgaria nk? Hapo unaposema ukiandamana na kuleta fujo unauwawa. Je waandamanaji wa hapa nyumbani wamewahi kuleta fujo ama polisi ndio huwa wanawapiga wananchi pindi tu wanapowaona wanaandamana? Maana mara zote polisi ndio huwa wanaanza kuwapiga waandamanaji kwa kile nilichokuambia watawala hawataki kusikia ukweli na mara nyingi huwa hawana majibu ya kile kinacholalamikiwa, ama hawako tayari kujirekebisha. Kwa huko Marekani ni tofauti na maandamano ya huku kwetu kwani maandamano ya kule ni ya ubaguzi wa rangi ambapo hapa kwetu ni tofauti kidogo. Ila kule US hatua stahiki zinachukkuliwa kwa wale polisi wanaoua raia tofauti na hapa kwetu polisi wanaoua wanapandishwa vyeo kwani wamewalinda watawala wasiambiwe ukweli. Kwa upande wa hapa nchini kwetu ukweli tuna rais mzuri lakini mwenye udhaifu wa uvumilivu na usikivu.
NB: Hili la mauji ya polisi huko Mbande wanasiasa wameliweka kuwa na taaswira ya kisiasa kwa ajili ya kuficha madhaifu yao. Kwa maneno marahisi kuna upuuzi wa aina fulani kwenye hili la mauji ya polisi pale Mbande. Hili tulipe muda tutajua ukweli na ushenzi ulio nyuma ya hili jambo.
Mkuu walimiss juice ya Ikulu wamesahau walikua wanaitwa kwa heshma ya Slaa,sasa mtakunywa ya miwa pale bugurun kwa mfuga mbwa ya ikulu mmechambia simeNjaa mbaya kaka,
huwezi kuwa na kiburi mbele ya hela.
Alafu huo mgomo wao sijui umeleta faida gan? Walifikiri watabembelezwa waende ikulu tena kama kipindi cha JK?
Mkuu hiyo ulaya unayoitaja wewe ya Eastern Europe hizo nchi zilizokuwa za kisoshalist hakuna demokrasia kule. Demokrasia yetu kwa sehemu kubwa ni ya Ulaya magharibi. Ama umewahi kusikia nchi zetu zinaiga demokrasia ya kosovo, hungary, bulgaria nk? Hapo unaposema ukiandamana na kuleta fujo unauwawa. Je waandamanaji wa hapa nyumbani wamewahi kuleta fujo ama polisi ndio huwa wanawapiga wananchi pindi tu wanapowaona wanaandamana? Maana mara zote polisi ndio huwa wanaanza kuwapiga waandamanaji kwa kile nilichokuambia watawala hawataki kusikia ukweli na mara nyingi huwa hawana majibu ya kile kinacholalamikiwa, ama hawako tayari kujirekebisha. Kwa huko Marekani ni tofauti na maandamano ya huku kwetu kwani maandamano ya kule ni ya ubaguzi wa rangi ambapo hapa kwetu ni tofauti kidogo. Ila kule US hatua stahiki zinachukkuliwa kwa wale polisi wanaoua raia tofauti na hapa kwetu polisi wanaoua wanapandishwa vyeo kwani wamewalinda watawala wasiambiwe ukweli. Kwa upande wa hapa nchini kwetu ukweli tuna rais mzuri lakini mwenye udhaifu wa uvumilivu na usikivu.
NB: Hili la mauji ya polisi huko Mbande wanasiasa wameliweka kuwa na taaswira ya kisiasa kwa ajili ya kuficha madhaifu yao. Kwa maneno marahisi kuna upuuzi wa aina fulani kwenye hili la mauji ya polisi pale Mbande. Hili tulipe muda tutajua ukweli na ushenzi ulio nyuma ya hili jambo.
Ndugu yangu nashukuru kwa maelezo yako lakini nadhani inabidi tukubaliane kuwa hatuwezi kukubaliana...Hapa Tanzania maandamano mengi yametokea na watu wanaleta fujo katika maandamano hayo...Sijui umri wako lakini nakumbuka miaka ya 1990 watu wengi waliandamana kule magomeni mwembechai...polisi aliuawa na fujo kubwa zilitokea ukiwemo uharibifu wa mali...Yule polisi aliyeuawa alikuwa anakwenda kazini kwake akiwa na uniform ...lakini waandamanaji walianza kumfukuza kama mbwa wakampiga mawe mpka akafa..ndipo dola ikaingilia kati na kuzima maandamano hayo na mpka watu kadhaa wakafa (ingawa tulitangaziwa kuwa wamekufa wawili), na huo ndio ulikuwa mwisho wa hadithi ya mwembechai...maandamano yalizimwa kwa nguvu na watu walikimbia mpaka kibaha kwa hofu...yale ya mwembechai hayatarudia tena, isipokuwa sasa wanataka kuleta maandamano ya UKUTA, tusubiri tuone kitakachotokea, lakini mimi nimeionya familia yangu sitaki kuona mtu anavinjari ovyo ovyo kwenye 'mikusanyiko' ya watu....Ninavyofahamu mimi polisi hawawezi tu kuanza kuwapiga waandamanaji pasipo sababu...Na awali ya yote maandamano hayo ya UKUTA yameshapigwa marufuku, na kukaidi maandamano hayo ni ukaidi kwa hiyo mtu lazima atandikwe kisawasawa...
jaribu kuelewa hoja na mantiki ya hoja mkuu.Ni vyema kushukuru pale ambapo umoja wa taifa letu linaporejea na siyo kushangilia mpasuko wa taifa letuHahahahahahahahahaha safi sana Dr. Tulia
jaribu kuelewa hoja na mantiki ya hoja mkuu.Ni vyema kushukuru pale ambapo umoja wa taifa letu linaporejea na siyo kushangilia mpasuko wa taifa letu
.............Hivi kuna demokrasia ya ulaya mashariki, ulaya magharibi, afrika na kadhalika???!!!! Najiuliza tu....
Mkuu ni kweli sitaki kupinga angalizo lako, lakini mara nyingi waandamanaji huwa wanafikia hatua hiyo baada ya kuchoka na hali fulani, ni dhahiri binadamu anapofikia hatua ya kuandamana anakuwa amefikia hatua ya mwisho ya uvumilivu, hivyo kuna wengine wanaongozwa na mihemuko. Na miaka hiyo ya 90 ndio watu walikuwa wanaanza mambo hayo ya maandamano hivyo hata wale waliokuwa wanawaongoza hawakuwa wanahubiri kuwa maandamano ya amani. Let me give you vivid example, niliwahi kuona maandamano ya cdm arusha 2011, kwa kweli maandamano yale yalikuwa ya amani na chanzo cha fujo na mauaji yale yalikuwa ni polisi kutokana na kupokea maelekezo toka kwa watawala waliokuwa wanaongozwa na utashi wa itikadi za kisiasa. Nikijaribu kuwasikiliza viongozi wa cdm wanarudia kila mara kwamba ni maandamano ya ukuta ni ya amani, na ninadhani wengi wa waandamanaji wao wako tayari kufanya maandamano ya amani, na kama halitatokea kundi jingine likaingilia ili kuyapa maandamano hayo taswira tofauti kwani tabia hizo tunajua watawala wanaweza kuzitumia ili kuhakikisha ujumbe sahihi haufikishwi kwa minajili ya kukwepa ukweli mchungu. Ni watu wachache sana wanaopenda kusikia ukweli, hasa aina ya kiongozi wetu sio mvumilivu wa hali hiyo, kwa hili namsamehe kwani ndio ubinadamu ila wanatakiwa washauri nasaha ili kumfunda kiongozi wetu kwamba nafasi yake haihitaji mihemuko bali busara na uvumilivu zaidi. Nje ya haya mapungufu yake anafanya vizuri, ni juu yake kuyafanyia kazi hayo mapungufu yake ili kama taifa tuende mbele pamoja.
Ni rahisi kusema au kutamka kuwa maandamano yatakuwa ya amani, lakini utekelezaji wake ndiyo tatizo...polisi au dola ikishasema kuwa maandamano hayo hayatakiwi ni muhimu watu watii sheria au amri na agizo hilo...sheria zetu ziko wazi kabisa kuhusu suala la maandamano, 'assembly' au mikusanyiko ya watu kisiasa...Chama kinaweza kutoa taarifa kwa polisi, na sheria hiyo hiyo inatamka wazi kuwa ikiwa polisi wataona unaweza kutokea uvunjifu wa amani wanaweza kuwaandikia 'wahusika' kuwa maandamano au mikusanyiko hiyo hairuhusiwi...sasa kuna watu wengine wana 'masharubu' na wanakaidi na kutafsiri vibaya sheria hiyo eti kwamba wanachopaswa kufanya wao ni kutoa taarifa tu kwa polisi...yaani watu hao wananukuu vifungu nusu nusu...hii ni mbaya kabisa...sheria hiyo imetoa nafasi kwamba wasiporidhika waende kutafuta haki mbele akiwemo Waziri, sasa watu hao hawataki...nchi hii haiwezi kuwa na mamlaka mbili, ikitokea hivyo itakuwa ni fujo...Baadhi ya wanasiasa wametamka kuwa watahakikisha wanafanya maandamano na fujo ili nchi hii isitawalike...lakini wakati huo huo wanapuliza kuwa eti maandamano yatakuwa ni ya amani...umesema humu kuwa mara nyingi waandamanaji huwa wanafikia hatua hiyo baada ya kuchoka na hali fulani, ni dhahiri binadamu anapofikia hatua ya kuandamana anakuwa amefikia hatua ya mwisho ya uvumilivu, hivyo kuna wengine wanaongozwa na mihemuko.
Kwa kauli yako hiyo hapo juu mimi najiuliza hivi Tanzania hii kuna tatizo gani mpaka watu wachoke na hali iliyopo??? Mimi nimebahatika kutembelea nchi kadhaa na hata kusoma historia ya nchi kadhaa...hivi kweli Tanzania ni nchi ambayo eti watu wamechoka na hali Fulani kama unaqvyosema??? Nadhani watanzania wamechoka na amani iliyopo....