Viongozi katika mataifa yaliyoendelea hupeleka matukio mahali wanakotokea huku wakiwa viongozi wa kitaifa?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,510
2,060
Juzijuzi rais kaja na kizimkazi kabla hapajapoa waziri mkuu kaja na rwangwa marathon tukiwa hatujui mpango ataibuka na nini kule Buhigwe, kabla hatujasahau yale ya tulia kula Mbeya.

Nimesikia aibu sana leo baada ya waziri mkuu kushindwa kutoa hotuba inayoashiria kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa badala yake amehutubia kana kwamba rwangwa ni nchi na yeye ndiye raisi wa hiyo nchi.

Yaani diamond ametoa hotuba ya kitaifa utadhani yeye ndiye waziri mkuu. Moleli na ndumbaro wakaishia kumnadi majaliwa. Haya ni mambo ya hovyo kabisa.

Matukio haya ukiyafuatilia kwa undani yamejaa kampeni za uchaguzi ujao. Sina tatizo na hilo ila swali ninalojiuliza ni kwa nini mtu atumie madalaka yake kupeleka hizi shughuli nyumbani kwao ili kujijenga kwaajili ya uchaguzi ujao!?
 
Back
Top Bottom