Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,893
- 3,200
Ni matumaini yangu nyote mko salama.
Nimeona nilisemee hili maana limeenda!
Hivi kiongozi unatoa wapi ujasiri wa kukataa kuwasikiliza waliokuweka madarakani?
Hivi unavaaga viatu vya wale unaokataa kuwasikiliza?
Hebu fikiria umedhurumiwa na kiongozi fulani, unakwenda kushitaki kwa mamlaka ya juu, hiyo mamlaka inakwambia rudi kwa huyo huyo aliekudhurumu ili akupe haki yako! Hii si sawa kabisa.
Kwa ninavyofahamu, kiongozi wa juu kabisa mfano Rais, anawajibika kwa kazi zote za kuwaletea watu wake ustawi wao pamoja na ustawi wa nchi kwa ujumla. Hao wengine aliowateua au walioajiriwa na serikali yake, wanafanya kazi kwa niaba ya Rais.
Kwa mantiki hiyo, Rais ni Mwalimu, Daktari, Mwanasheria, Hakimu, Jaji, Mbunge, Diwani, Balozi, Mtendaji, Ustawi, n.k.
Hivyo, kwa mtu wa hali ya chini kuwa na ujasiri wa kutaka kusikilizwa na mtu wa hali ya juu, inamaanisha kwamba huku kwengine, kumeshashindikana.
Sasa cha ajabu, anatokea kiongozi anakuambia muda wa kukusikiliza ni mchache, nchi ni kubwa, na ina wananchi wengi sana!
Ama kweli, ngoja mambo yaendelee hivi hivi tuone, maana mwisho wa siku ni sisi hawa hawa ambao hatusikilizwi nao, huwa tunawachagua kuingia madarakani kwa kishindo!
Mwisho tutakapochoshwa na hayo, tutaongea lugha moja.