Paul Makonda amkosha Rais Samia kwa uchapa kazi wake, ataka viongozi wengine waige mfano huo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,763
Ndugu zangu Watanzania,

Nilishawaambieni sana humu jukwaani na hata mitaani kuwa Rais Samia anafuatilia sana kila kinachokuwa kinaendelea katika ziara za Mheshimiwa Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara.na nikawataka viongozi huko mikoani kuwa makini sana na kuacha mara moja na haraka sana kufanya kazi kwa mazoea .lakini pia nikawasihi sana kuwa mtoke maofisini na mwende mitaani kwa wananchi kusikiliza kero zao na kutoa majibu au kutatua kero zao zote.

Niliwaambiane ya kuwa ukimuona mwamba na Jabali la siasa Paul Makonda mkoani kwako basi ujuwe kuwa ni chama cha Mapinduzi kimefika kuangalia utekelezaji wa ilani yake na namna wananchi wanavyohudumiwa na kupewa haki zao.nilisema kuwa kwa hiyo isitokee kiongozi akaleta nyodo na kiburi au dharau ya aina yoyote ile.maana CCM ndio iliyoomba kura kwa wananchi na ndio iliyounda serikali na siyo serikali iliyoiunda CCM.kwa hiyo CCM Ndio sikio la watanzania ambapo ikikuita jukwaani kiongozi ni lazima utoe majibu stahiki.

Sasa leo Mheshimiwa Rais mbele ya macho ya Dunia nzima ameonyesha kukoshwa na kufurahishwa na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa na kutamka hadharani kabisa na kuwataka wengine waige mfano huo kwa kwenda chini huko kuwasikiliza wananchi kero zao na kutatua.amewataka wawe na ratiba za kwenda kwa wananchi kutatua kero za wananchi.

Ukiona mkuu wa nchi anatoa pongezi kwako na kukupongeza kwa uchapa kazi wako basi ni lazima upate moyo na nguvu za kusonga mbele zaidi. Kwa hakika Makonda mwamba mwenyewe anastahili sana sana pongezi .anapigwa vita lakini ndio kwanza anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania wanyonge ,ambao wanamuona kama mtetezi na sauti yao. Makonda mwamba mwenyewe ipo siku atakuwa Rais wa Taifa letu kama ambavyo nilishaandika hapa jukwaani.

Anajituma kupita kiasi,anachapa kazi mpaka kazi zinapiga saluti ya kijeshi kwake ,ni mzalendo asiyetiliwa mashaka,ni jasiri aliyepitiliza,anajiamini mpaka shetani mwenyewe anamwogopa asikiapo sauti yake ikiunguruma jukwaani,anakubalika na watanzania kwa kiwango cha hali ya juu sana.ni kiongozi mbunifu sana na aliyekamilika katika kila idara .kuanzia mwakani anastahili kupewa nafasi nyeti serikalini katika serikali itakayoongozwa na Rais Samia ili amsaidie katika kuwatumikia watanzania.

Mheshimiwa Paul Makonda songa mbele kaka .usiogope wala kurudi nyuma katika kuwatetea watanzania,usitetereke wala kuhofu kwa kuwa Mungu wa mbinguni yupo upande wako na ndio alikuinua tena katikati ya furaha ya maadui zako waliokuwa wamekutangazia mwisho wako .atakulinda kama alivyomlinda Daudi zidi ya hila na mkono wa Sauli.atakupigania vita yako na utakuwa mshindi wakati wote.wajapokuja kwa njia moja watatawanyika kwa njia saba. Utawapiga kwa Neno na silaha zao hazitaweza kuinuka mbele yako.watapotea mbele yako na wasiweze kuonekana tena mbele yako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

IMG-20240206-WA0027.jpg
IMG-20240202-WA0004.jpg
img_tmp_tag1705908502140.jpg
 
Hivi Lucas unalipwa bei gani kwa hii kazi
Wazalendo kama mimi huwa hawafanyi kazi kutafuta malipo wala kulipwa.kwa hiyo mimi silipwi kitu na mtu yeyote yule zaidi ya kuusema ukweli hata kama ni mchungu kwa wasiopenda ukweli na wenye chuki Binafsi kwa wazalendo wa kweli wa Taifa letu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nilishawaambieni sana humu jukwaani na hata mitaani kuwa Rais Samia anafuatilia sana kila kinachokuwa kinaendelea katika ziara za Mheshimiwa Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara.na nikawataka viongozi huko mikoani kuwa makini sana na kuacha mara moja na haraka sana kufanya kazi kwa mazoea .lakini pia nikawasihi sana kuwa mtoke maofisini na mwende mitaani kwa wananchi kusikiliza kero zao na kutoa majibu au kutatua kero zao zote.

Niliwaambiane ya kuwa ukimuona mwamba na Jabali la siasa Paul Makonda mkoani kwako basi ujuwe kuwa ni chama cha Mapinduzi kimefika kuangalia utekelezaji wa ilani yake na namna wananchi wanavyohudumiwa na kupewa haki zao.nilisema kuwa kwa hiyo isitokee kiongozi akaleta nyodo na kiburi au dharau ya aina yoyote ile.maana CCM ndio iliyoomba kura kwa wananchi na ndio iliyounda serikali na siyo serikali iliyoiunda CCM.kwa hiyo CCM Ndio sikio la watanzania ambapo ikikuita jukwaani kiongozi ni lazima utoe majibu stahiki.

Sasa leo Mheshimiwa Rais mbele ya macho ya Dunia nzima ameonyesha kukoshwa na kufurahishwa na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa na kutamka hadharani kabisa na kuwataka wengine waige mfano huo kwa kwenda chini huko kuwasikiliza wananchi kero zao na kutatua.amewataka wawe na ratiba za kwenda kwa wananchi kutatua kero za wananchi.

Ukiona mkuu wa nchi anatoa pongezi kwako na kukupongeza kwa uchapa kazi wako basi ni lazima upate moyo na nguvu za kusonga mbele zaidi. Kwa hakika Makonda mwamba mwenyewe anastahili sana sana pongezi .anapigwa vita lakini ndio kwanza anaendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania wanyonge ,ambao wanamuona kama mtetezi na sauti yao. Makonda mwamba mwenyewe ipo siku atakuwa Rais wa Taifa letu kama ambavyo nilishaandika hapa jukwaani.

Anajituma kupita kiasi,anachapa kazi mpaka kazi zinapiga saluti ya kijeshi kwake ,ni mzalendo asiyetiliwa mashaka,ni jasiri aliyepitiliza,anajiamini mpaka shetani mwenyewe anamwogopa asikiapo sauti yake ikiunguruma jukwaani,anakubalika na watanzania kwa kiwango cha hali ya juu sana.ni kiongozi mbunifu sana na aliyekamilika katika kila idara .kuanzia mwakani anastahili kupewa nafasi nyeti serikalini katika serikali itakayoongozwa na Rais Samia ili amsaidie katika kuwatumikia watanzania.

Mheshimiwa Paul Makonda songa mbele kaka .usiogope wala kurudi nyuma katika kuwatetea watanzania,usitetereke wala kuhofu kwa kuwa Mungu wa mbinguni yupo upande wako na ndio alikuinua tena katikati ya furaha ya maadui zako waliokuwa wamekutangazia mwisho wako .atakulinda kama alivyomlinda Daudi zidi ya hila na mkono wa Sauli.atakupigania vita yako na utakuwa mshindi wakati wote.wajapokuja kwa njia moja watatawanyika kwa njia saba. Utawapiga kwa Neno na silaha zao hazitaweza kuinuka mbele yako.watapotea mbele yako na wasiweze kuonekana tena mbele yako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.View attachment 2933333View attachment 2933334View attachment 2933336
🚮
 
Back
Top Bottom