babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 13,219
- 16,213
Unajua katika maisha watu tunapitia mambo mengi sana.
Na bila kuyaongea yataendelea.
Kwenye Mada
Siku bana nikalamba bus Dom to Sgd enzi hizo 80s pale vumbi tu njia nzima.
Tumekula njia mdogo mdogo na lile ngala ngala sijui Azan express sijui shalua luxure sikumbuki e banaee Manyoni hiyo tukala mpunga wetu ma soda safii.
Tukaanza safari kuitafuta Singida.
Pale kuna kapori fulani na milima alafu njia panda ya Itigi kwenda Singida mnapinda kulia.
Ile tumepinda jioni jioni hivi bus inaenda mdogo mdogo tunaelekea Singida e banaee hapo kati porini haswa.
Tukakuta jamaa wameweka magogo barabarani.
Hamna gari kupita.
Na magari yenyewe yapo?
Ile bado dereva anaangalia namna ya kutoroka majambazi hayo yakatoka maporini huko zikawashwa risasi 2 na gobole hewani tukaambiwa wote tulale chini.
Wale jamaa walituibia kila kitu,maana ya kila kitu ni kwamba hadi boxer unavuliwa.
Sasa hapo tukawa uchi bus zima,wamama wako uchi wanaume uchi. ebana sijui tulifikaje mjini🤣🤣🤣
ila abiria 65 tumeporwa mpk tunaachwa uchi.
Nakumbuka hadi leo ila haiingii akilini
Kama una mkasa wa mabus weka hapa