KERO Ving'ora na Plate Number zisizo rasmi vimekuwa kero Mitaani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Hizi namba za 3D imekuwa Ghafla sana kung'olewa, na Jeshi la polisi limesimama imara katika Hili, Ombi langu kwa Jeshi la Polisi ni hili:-

Namba za Ajabu
Mtaani huku kuna namba nyingi ambazo sio rasmi, Nyeusi, Nyeupe na Njano hapo nyuma mlitoaga tamko lakini hizi namba bado zipo na hatujui zinaama gani, Gari ya 2023 ina namba ya mwaka 2003.

Pia kuna hawa maafisa usafirisha almaarufu kama BodaBoda na bajaji unakuta wamekunja plate number haisomeki kirahisi unakuta anakuchubua njiani na unashindwa hata kukariri namba

Ving'ora
Kuna gari nyingi sana ambazo zina Namba za kiraia zina Ving'ora utadhani ni kiongozi mkubwa alafu unakuta ni muhindi mwenye LC 600 yake kaiweka king'ora na hata barabarani wana act kama watu wa Ulinzi na Usalama, Hawa hata traffic hawawapigi mkono je hii ni sahihi? kama sivyo basi itokomezwe, tukianza kuishi khivi taifa litakuwa la watu wanaojiamulia, ikiwa Jeshi la Ulinzi na Usalama lipo Imara na linaweza Shughulikia hili.
Police car.jpg


Tunawaamini tunaomba hili mkalifanyie kazi



UPDATED: 13 MACHI, 2024

Jeshi la polisi limetoa tamko juu ya swala hili, Mamlaka kweli imesimamia Haki, sasa wale jamaa wa Vingora na gari zao binafsi, mkae mkao
Screenshot_20240313-212618.jpg


Pia soma SACP. Ramadhan Nga'nzi: Msako utaanza kuwakamata waliokiuka agizo la kuondoa namba za 3D
 
Yaani vitu vinafanyika vya hovyo kabisa utadhani hakuna serikali, humo barabarani ndio hovyo kabisa, kila mtu anapita upande anaojiamulia na kwa namna anayojiamulia. Shida tupu

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kuna taa wamefinga bodaboda kama disco light aisee hizo ni hatar zaid washenz wale
 
Back
Top Bottom