Hivi kwanini baadhi ya gari za 'Patrol' zinatolewa Plate Number na Askari wake hawatoi Vitambulisho?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
images.jpeg

Wakuu, Kuna kitu kinanipa shida sana kuhusu utendaji wa Idara za Ulinzi na Usalama nchini, bado zinafanya kazi kizamani na kikoloni sana. Wakati dunia imeadvance kwenda kwenye Teknolojia wao bado wanafanya kazi kwa utaratibu wa kishamba sana.

Kuna huu utaratibu wao kutumia magari yasiyo na Plate Number au namba za Nje ya Nchi, unakera na kutishia usalama wa Raia kwa kiasi kikubwa. Na kimsingi hawana sababu ya msingi kufanya hivyo.

Kwanini uondoe Plate Number au Utumie namba ya nje kama nia yako ni njema na unalenga kutafuta Uhalifu ndani ya nchi yako?

Mtakumbuka hata tukio la kutekwa Mfanyabiashara Mo Dewji lilifanyika kwa kutumja gari lenye plate number za nje.

Utaratibu huu kwa kiasi kikubwa umekuwa ukichangia matukio mengi ya uvunjwaji wa Sheria na Haki za Binadamu na wahusika kutojulikana kwasababu ya kuficha utambulisho wao kuanzia namba za Magari.

Ni vema sasa Jeshi la Polisi na Idara nyinginezo za Ulinzi, Upelelezi ziache kufanya kazi kwa kutisha raia.
 
MC si bodaboda hizo?
anyway sababu ya msingi ni nature ya mission zao, kuna wakati wanakuwa na mission za ki TISS , mfano alivyokamatwa roma, mdude, mo... so kuficha utambulisho kunawaweka salama wao, na inakuwa ni rahisi kukana kuwa huyu mtu wenu hayuko kwao...
ni mambo ya watu weusi wakishakuwa na madaraka wanageuka manyang,au
 
Back
Top Bottom