Vine yageuka Byte, imesaini mkataba na WEPLAY Group

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
3,403
2,000
Mtandao uliokuwa maarufu duniani kote Vine umefanya mabadiliko na sasa utatambulika kama Byte.

IMG_20200125_052725.jpg


Vine kwa miaka kadhaa ilisimama imara kabla ya kupigwa vikumbo na magwiji Instagram, Snapchat na hata kusogezwa mbali zaidi na Tiktok.

Vine imekuwa ikifanya tafiti na kutengeneza mbinu wezeshi za kuinuka kwake bila mafanikio hadi sasa ilipoamua kuja kivingine kama Byte.

Byte ni mtandao wa kijamii unaopatikana kupitia Android na iOS kwa watumiaji wa simu janja.

Byte imeingia makubaliano na WEPLAY Group kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano kuweza kueneza ubunifu na kukuza brand zote mbili.

CEO Mikio Greutschke, COO Michael Moor na CTO Sajad Sergio wa WEPLAY Group wametia saini makubaliano hayo yatakayoifanya Byte kuwa Mtandao pekee wa kijamii kutoa udhamini.

Malengo ya Byte ni kuweza kueleza, kutoa na kusambaza ubunifu zaidi ukilinganisha na mitandao mingine huku slogan itakayotumika ikiwa "Creativity First"

Mtandao wa Byte kama ulivyo utambulisho wake utakuwa ni mwokozi katika utumiaji data bila kupunguza ubora wa maudhui ya watumiaji.

Ubunifu wa Byte unaambatana na urembo pia nakshi zisizokuwa na kifani wala tafrani ndani yake huku maudhui yakiwalenga watu wote.

Mimi nipo Byte, wewe unasubiri nini?
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,306
2,000
Sergio Watu wa kufuatilia mada zako hatutazidi 9 au 13, nimekuelewa toka ulipoanza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom