Byte iliyokuwa Vine ni Fursa ya kisasa kwa vijana kiuchumi

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
4,125
6,250
Byte ni mtandao wa kijamii wenye kuruhusu utuamiaji wa video fupi "Clips" zenye sekunde sita, kupitia Byte utaweza kuona kurasa rasmi kutoka kwa wafuasi na unao wafuata katika Kurasa Baba "Feed"

Byte iliyoasisiwa pakubwa na aliyekuwa mvumbuzi mwenza wa Vine, Dorn Hoffman ilianza shughuli ramsi January hii baada ya miezi sita ya majaribio yaliyofanyika nchini Ujerumani, Marekani, Tanzania, Colombia, Australia, Brazil, Uswiss, Afrika ya Kusini na Czech Republic. Ni ingizo jipya la kuweza kutengeneza kipato kwa vijana pia kutengeneza umaarufu kwa wanaoutafuta.

Kama ilivyo Tiktok, Triller, Lasso from Facebook, Likee, Snapchat and co. Byte imeundwa kivingine na kwa ubunifu maridhawa kuweza kukupa mahitaji muhimu ya kimtandao kwa ubora wenyewe levels za kimataifa.

Kikubwa kupitia Byte hivi karibuni utaweza kuingia katika mfumo wa "Partner Program" mfumo huu utakuwezesha kufanya "Monetization" ambayo itakuwa chagizo kwako kuweza kutengeneza kipato kwa kutumia mtandao.

Kama wafanyavyo YouTube lakini Byte itakuwa ikitoa asilimia kadhaa ya fedha kwa mtumiaji ambaye video yake itakuwa imesambaa zaidi "Viral".

Muda wowote tutegemee kitega uchumi kipya chenye ubatizo wa furaha, maarifa na ubunifu ndani yake. Hii ndio Byte, Creativity first.

Vijana ni vyema kuangalia wapi kuna maarifa, ubunifu na kikubwa zaidi maslahi.

Mimi nipo Byte, wewe unasubiri nini?
 
Nmewahi seat nipe link nikainyake nimechooshwa na uhuni na ujima na YouTube pamoja na adsense yao masharti kama mganga wa kienyeji malipo hafifu.
Kwa kupitia byte.co utaweza kupakua app hiyo itakapokuwa tayari kwenye eneo lako.

Lakini kwa wataalamu wa masuala ya server unaweza kutumia mfumo unaotumika kupata access ya Spotify.
 
Sasa inaletaje vitu ambavyo ni vya kisadikika eleza vizuri njia za kuipata huduma hiyo me niko serious ujue
Vitu gani vya kusadikika?! Byte.co ilifanyiwa majaribio na kisha hivi sasa maeneo mengi ya Africa yamewekewa restrictions kutokana na watumiaji wengi wa mitandao kutojielewa.

Ndio sababu utaweza kuona Spotify, Lasso na YouTube Music (Ilikuwa) zimezuiwa kwa Africa.

Byte ilikuwa wazi kipindi cha majaribio hasa Tanzania na sasa imekuwa restricted kutokana na watu wachache mliojitokeza kwa support ya jaribio.

Hivi sasa Byte inapatikana ramsi kwenye maeneo baadhi kama ilivyo Spotify lakini hilo halizui kuwapatieni fursa hiyo inayotolewa na Byte.

Kikubwa kama upo ya Central-Sub Saharan Countries unaweza kupitia Byte.co kupakua au unaweza kutumia mfumo wa VPN kupata access kama ilivyo Spotify.

Fursa ni hiyo itumie.
 
Back
Top Bottom