Vincent Laswai wa Kibo Palace na Trust Bureau de changes yuko matatani?

Ila Tanzania kuna mambo ya kifala sana sasa wakimnyanyasa uyo waliojariwa anaowalipa mshahara na wana familia inakuaje? Hio serikali iliopo iliwekwa kwa kuamua wenyewe au wapiga kura waliojajwa mil 8 sijui kweli au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo tu awamu hii ila kwa ujumla mfanya biashara HATAKIWA hata siku moja kujikomba komba kwa wanasiasa! Huwezi kujua kesho kitatokea nini! Mfanyabiashara unatakiwa uwe neutral na usitumie wanasiasa au nguvu za fedha kujipatia vitu kwa njia haramu. Bakresa ni mmoja ya wanafanyiabisha wanaopaswa kuigwa kwa hapa Tanzania.
Kwani Bakresa nae alipona? Mbona nae alipata misukosuko sana chini ya utawala huu na kumbuka juzi juzi tu ndio maziwa yake yamerudi sokoni
 
Wanajamvi,
Vincent Laswai ni mfanyabiashara maarufu sana pale Moshi. Ndiye mwenye ile Kibo Palace Arusha, mwenye Bureau de changes Moshi na Arusha ambazo zilivamiwa na jeshi kipindi kile, na hadi sasa zimefungwa. Pia ana biashara za jumla kuagiza sukari na bidhaa nyingine kama batteries nk kutoka nje.

Kuna waliokuwa wakisema hiyo Kibo Palace wako na Uhuru Kenyatta. Hoteli hiyo ni maarufu sana. Viongozi wakubwa hufikia hapo. Kuanzia kina Kenyatta, Kikwete, na hata Bernard Membe, ambaye naye inasemekana ni rafiki mkubwa wa ndugu Laswai!

Sasa mida hii ninayozungumza, maafisa usalama pamoja na askari wamezunguka biashara zake na inasemekana anatafutwa. Nadhani tayari alikuwa amesha surrender passport yake, ila kama kachomoka, pengine alikuwa na zaidi ya moja.

Kuna wanaodai kuwa kuna mipango inayoendelea dhidi ya wafanyabiashara flani, wengine wanasema ni ukaribu wake na Bernard Membe ndiyo umemponza! Amekuwa monitored na hakuwa akiweza kuongea hata kwa simu bila kufuatiliwa.

Bado nasubiria kusikia nini hatma yake. Sijui kama ni issue ya utakatishaji fedha au ni kitu gani!

Pia wamebeba computers nk, kama kuna wenye info ya kinachoendelea watueleze. Hapo chini akiwa na JKView attachment 1032828

Update:
Vyombo vya uchunguzi vimevamia biashara za mfanyabiashara tajiri wa Moshi, Vicent Laswai vikimchunguza kwa tuhuma za ukwepaji kodi.

Moshi. Vyombo vya uchunguzi ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vimevamia biashara za mfanyabiashara tajiri wa Moshi, Vicent Laswai vikimchunguza kwa tuhuma za ukwepaji kodi.

Biashara zake yakiwamo maghala matatu ya kuhifadhi bidhaa mbalimbali kutoka nchini Kenya yaliyopo maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na duka la jumla vimewekwa chini ya uchunguzi wa vyombo hivyo

Laswai mwenyewe jana na juzi hakupatikana kueleza juu ya uchunguzi huo kutokana na simu yake kutokuwa hewani na marafiki wa karibu wanadai yuko nchini India kwa matibabu.

Uchunguzi huu mpya unakuja ikiwa ni mwezi mmoja tu umepita, tangu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuamuru kufungwa kwa duka lake kubwa la kubadilisha fedha la Trast lililopo mjini Moshi

Kufungwa kwa duka hilo nako kulikuja miezi mitatu baada ya BoT kufunga maduka 30 ya kubadilisha fedha jijini Arusha likiwamo la Central Forex ambalo lilikuwa ni tawi la duka lake la Trast la Moshi.

Operesheni hiyo iliyohusisha pia polisi lakini Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah hakupatikana ofisini na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi hakupokea ingawa juzi alionekana akiwa na kikosi kazi hicho majengo ya TRA.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alithibitisha kuwapo kwa uchunguzi huo, lakini akakataa kueleza chochote akisema itakuwa ni kuingilia uchunguzi.
Source: Mwananchi.

Update: 1/3/2019

Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo, Leo hii wamevamia nyumbani kwa ndugu Laswai kule Shanty town! Pia inasemekana kuwa mtoto wake anashikiliwa na polisi kule Arusha! Pengine ni kwenye jitihada za kutaka arudi kutoka huko aliko? Maana taarifa rasmi zina sema kuwa yuko India kwa matibabu!
Tuna kila sababu ya kuendelea kumshukuru sana Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa mambo makuu aliyotutendea mwaka huu. Isingelikuwa ni yeye watu wake tungeendelea kuaibishwa hata sasa.
 
Kibo Palace hotel ni ya Basil pesambili mramba. Aliyewahi kuwa waziri wa fedha. Lasway amebambikiwa tu
 
Kibo Palace ni ya Marehemu Basil Mramba (Waziri wa fedha wa zamani)...huyo Laswai amewekwa tu ili Basil asijulikane kama mmiliki
 
Back
Top Bottom