Vincent Laswai wa Kibo Palace na Trust Bureau de changes yuko matatani?

Vincent Laswai wa Kibo Palace na Trust Bureau de changes yuko matatani?

Kuna KIBO PALACE na PALACE, Mdau kauliza kama hizo mbili zote ni zake? jibu ni yes, zote mbili anaendesha yeye.

Kibo palace ipo pale mkabala na Aicc Hospital na Palace ipo mkabala na Manispaa, mitaa ya kwa Mkuu wa Mkoa.

Mwanzo baada ya kujenga Kibo Palace walisema yupo share na Basil Mramba, naona sasa wameleta mpya ya Kenyata...Wabongo kwa kuchonga.
umekaririshwa , Arusha Palace ni ya Hans Elingaya Macha nae pia ana Bureau de change Dar na mikoa ya kaskazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna KIBO PALACE na PALACE, Mdau kauliza kama hizo mbili zote ni zake? jibu ni yes, zote mbili anaendesha yeye.

Kibo palace ipo pale mkabala na Aicc Hospital na Palace ipo mkabala na Manispaa, mitaa ya kwa Mkuu wa Mkoa.

Mwanzo baada ya kujenga Kibo Palace walisema yupo share na Basil Mramba, naona sasa wameleta mpya ya Kenyata...Wabongo kwa kuchonga.
Kibo Palace ndiyo anahusika nayo. Ni kweli walisema ni ya Mramba. Hilo kwamba ni ya Mramba, nadhani watu wa system ndivyo wanavyoamini. Ni rumours zilizokuwepo toka wakati inajengwa.

Imekuwa kuhusiahwa na Kenyatta baada ya wakenya kununua share kubwa kama sikosei.
 
Mara ya mramba Mara ya shirima.wa precision air... Ninachojua huyu mzee alianzia kwenye ujambazi front line Kuna kipindi alivamiwa na kina mangeu na wadogo za Alex masawe kisa huko Nyuma waliiba Kisha yy. Akawa double cross wenzie walimvamia saa mbili asubuhi baada ya kumwambia awape nyumba wamuache [emoji23][emoji23][emoji23] ila wale jamaa walikamatwa na mavitu kibao ya wizi maana aliwataja .. trust bureau ndo iliyovamiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sijui kwanini nilisahau kukutag?! Karibu sana boss!
 
Hii habari haiko balanced.

Tunatoa shutuma nyingi kwa serikali lkn uhalisia wa tukio lenyewe ni kuwa tunahisi tu. Inawezekana kabisa tajiri huyu alikuwa na michezo michafu ya kukwepa kodi, kumiliki kiasi kikubwa cha fedha in cash etc Yote hayo ni makosa, mlitaka aachiwe kisa tu anatoa ajira kwa wananchi wa kawaida nk.

Nchi haiendeshwi hivyo lazima tufuate sheria wote maskini na matajiri. Tusubir uchunguzi ukamilike.

Nafahamu kabisa awamu hii ina mambo ya kukomoana kisiasa lkn ukiangalia kwa mfano bureau de changes zote zilizofungwa Arusha Dsm je zote zinamsapot Membe? Mwachen jiwe afanye kazi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii habari imekosa vipi balance. Sema tutarekebisha. Na kama una sapoti operation, hakuna shida weka hoja tu. Hii ni JF watu wanabishana kwa hoja na wala siyo vihoja!
 
Ushauri wa kijinga anza kuutekeleza wewe. Hapa dawa ni kulipa kodi na kufuata sheria za nchi. Watu wafanye biashara halali
Natoa ushauri huu kwa Wafanyabiashara Wote wanaohisi kutofautiana na Utawala huu:
1. Andaa business proposal ya ku expand Biashara yako.
2. Nenda Banks omba mkopo Mkubwa Sana, assets zako ziweke Bond, zote.
3. Pokea mpunga wako, the next day chukua familia Yako, pelekeni fedha mkawekeze Biashara nyingine Nje ya nchi.
Baada ya hapo, walipe watu mishahara Yao, funga Biashara (tangazo la kufunga Biashara unalitolea ukiwa jurisdiction uliyoenda kuwekeza).
Mkifanya hivyo watu 10 tu, hiyo Kodi itakayopotea hapo Ni disaster katika Uchumi. Hawataweza kuchukua assets kwa sababu banks zinakuwa na title over the assets.
Mwisho, chukua uraia wa huko and never look back. Hatuwezi kuwa na nchi ya vinyongo na kutaka kuwakwamisha watu wasiendelee kimaisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibo Palace ndiyo anahusika nayo. Ni kweli walisema ni ya Mramba. Hilo kwamba ni ya Mramba, nadhani watu wa system ndivyo wanavyoamini. Ni rumours zilizokuwepo toka wakati inajengwa.

Imekuwa kuhusiahwa na Kenyatta baada ya wakenya kununua share kubwa kama sikosei.
Hata Palace Mkuu.
 
Kibo Palace ndiyo anahusika nayo. Ni kweli walisema ni ya Mramba. Hilo kwamba ni ya Mramba, nadhani watu wa system ndivyo wanavyoamini. Ni rumours zilizokuwepo toka wakati inajengwa.

Imekuwa kuhusiahwa na Kenyatta baada ya wakenya kununua share kubwa kama sikosei.
Hata ile Naura ya Marehemu walishasema Museven ana hisa, Wabongo ni Wazushi sana...na nadhani wapo Watu wanaotengeneza uzushi wa aina hiyo kwa malengo yao maalumu.
 
Wanajamvi,
Vincent Laswai ni mfanyabiashara maarufu sana pale Moshi. Ndiye mwenye ile Kibo Palace Arusha, mwenye Bureau de changes Moshi na Arusha ambazo zilivamiwa na jeshi kipindi kile, na hadi sasa zimefungwa. Pia ana biashara za jumla kuagiza sukari na bidhaa nyingine kama batteries nk kutoka nje.

Kuna waliokuwa wakisema hiyo Kibo Palace wako na Uhuru Kenyatta. Hoteli hiyo ni maarufu sana. Viongozi wakubwa hufikia hapo. Kuanzia kina Kenyatta, Kikwete, na hata Bernard Membe, ambaye naye inasemekana ni rafiki mkubwa wa ndugu Laswai!

Sasa mida hii ninayozungumza, maafisa usalama pamoja na askari wamezunguka biashara zake na inasemekana anatafutwa. Nadhani tayari alikuwa amesha surrender passport yake, ila kama kachomoka, pengine alikuwa na zaidi ya moja.

Kuna wanaodai kuwa kuna mipango inayoendelea dhidi ya wafanyabiashara flani, wengine wanasema ni ukaribu wake na Bernard Membe ndiyo umemponza! Amekuwa monitored na hakuwa akiweza kuongea hata kwa simu bila kufuatiliwa.

Bado nasubiria kusikia nini hatma yake. Sijui kama ni issue ya utakatishaji fedha au ni kitu gani!

Pia wamebeba computers nk, kama kuna wenye info ya kinachoendelea watueleze. Hapo chini akiwa na JKView attachment 1032828

Update:
Vyombo vya uchunguzi vimevamia biashara za mfanyabiashara tajiri wa Moshi, Vicent Laswai vikimchunguza kwa tuhuma za ukwepaji kodi.

Moshi. Vyombo vya uchunguzi ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vimevamia biashara za mfanyabiashara tajiri wa Moshi, Vicent Laswai vikimchunguza kwa tuhuma za ukwepaji kodi.

Biashara zake yakiwamo maghala matatu ya kuhifadhi bidhaa mbalimbali kutoka nchini Kenya yaliyopo maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na duka la jumla vimewekwa chini ya uchunguzi wa vyombo hivyo

Laswai mwenyewe jana na juzi hakupatikana kueleza juu ya uchunguzi huo kutokana na simu yake kutokuwa hewani na marafiki wa karibu wanadai yuko nchini India kwa matibabu.

Uchunguzi huu mpya unakuja ikiwa ni mwezi mmoja tu umepita, tangu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuamuru kufungwa kwa duka lake kubwa la kubadilisha fedha la Trast lililopo mjini Moshi

Kufungwa kwa duka hilo nako kulikuja miezi mitatu baada ya BoT kufunga maduka 30 ya kubadilisha fedha jijini Arusha likiwamo la Central Forex ambalo lilikuwa ni tawi la duka lake la Trast la Moshi.

Operesheni hiyo iliyohusisha pia polisi lakini Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah hakupatikana ofisini na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi hakupokea ingawa juzi alionekana akiwa na kikosi kazi hicho majengo ya TRA.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alithibitisha kuwapo kwa uchunguzi huo, lakini akakataa kueleza chochote akisema itakuwa ni kuingilia uchunguzi.
Source: Mwananchi.


Update: 1/3/2019

Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo, Leo hii wamevamia nyumbani kwa ndugu Laswai kule Shanty town! Pia inasemekana kuwa mtoto wake anashikiliwa na polisi kule Arusha! Pengine ni kwenye jitihada za kutaka arudi kutoka huko aliko? Maana taarifa rasmi zina sema kuwa yuko India kwa matibabu!
Movie imekolea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ile Naura ya Marehemu walishasema Museven ana hisa, Wabongo ni Wazushi sana...na nadhani wapo Watu wanaotengeneza uzushi wa aina hiyo kwa malengo yao maalumu.
Sasa nimekuelewa mkuu. Wanadai “miluzi mingi humchanganya mbwa”
 
Back
Top Bottom