Vinara wa kueneza Udini Tanzania

Vinara wa kueneza Udini Tanzania

Status
Not open for further replies.

Uyole12

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2010
Posts
595
Reaction score
176
Kwangu mie nyeupe ni nyeupe, nyeusi ni nyeusi. Nitasema ukweli hakuna mtu wa kumwogopa!

Najua chloroquine chungu lakini INATIBU leo nitatoa orodha ya baadhi ya watu na RADIO mbalimbali ambazo zinaongoza kwa kueneza udini Tanzania sijajua kama wanajitambua au wanafanya makusuudi.

Asilimia kubwa ya watu wanapatikana Chama cha mapinduzi yani CCM nadhani ndo dhana ile inaendelea ya watu wenye makosa kujificha CCM nina maana Mauzaji wa pembe za ndovu, Mafisadi wote wapo CCM, Wauza unga aka dawa za kulevya wote CCM.

Watu binafsi.
1. Shekhe ponda(Yupo jela now)
2. Nape Nnauye (CCM)
3. Shekh Isango (Radio Iman)
4. Juliana Shonza(CCM)
5. Mtela Mwampamba(CCM)
6. Shekhe Ilunga (MWANZA)
5. Mwigulu Nnchemba

RADIO zinazoongoza kusambaza udini tanzania ni Kama zifuatazo:
1. Radio Iman
2. Clouds Fm (Hawa wanaongoza kwa kutoa air Time kwa watu wanaoeneza udini Tanzania)
3. Radio Uhuru (CCM inahusika moja kwa moja na hii radio kwa kutoa air time kwa hawa watu wanaoeneza udini Tanzania)

Kama kuna mtu anazani kuna mtu anatakiwa kuongezwa au Radio inayotakiwa kuingizwa kwenye hii list ya waeneza udini Tanzania unaruhusiwa kuongeza. Nimeamua kuwataja ili watanzania kwa umoja wetu tuwakemee hawa watu na Taasisi zinazoeneza udini Tanzania kwa nguvu zote bila kuchoka.

Hatuwezi kuwaacha watu wakawa wanendelea kueneza udini nasi tunawachekelea kama serikali imeshindwa kuwadhibiti basi ni zamu yatu watanzania tusiopenda udini kuwakemea hawa watu kwa nguvu zetu zote.

Tumechoka kuona Makanisa yakichomwa moto, Mapadre wakiuwawa, Mashekhe wakimwagiwa tindikali etc kwa sababu ya hawa watu tusimame Tuwakemee
 
mbona mnazungukazunguka, mueneza udini na aliyetufikisha kwenye hali hii ya mpaka kuuana ni RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE, nani anabisha au nani hajui kuwa kampeni zake za 2010 ndio kwa kiasi kikubwazilichochea udini waziwazi. na damu ya wanaokufa bila hatia ITAMTAFUNA HADI WAJUKUU WA WAJUKUU ZAKE
 
Ni vizuri kama ukimuongeza Jakaya mrisho kikwete.
 
Nadhani pia NEC nikimaanisha Tume ya taifa ya uchaguzi na Msajiri wa Vyama vya siasa ndo mhusika mkuu!! HAWAJATUTENDEA HAKI HAWA KWA KURUHUSU UPUUZI MWINGI UNAOKIUKA TARATIBU ZA NCHI KUTOFUATWA.
 
Sijaona taasisi hata moja hapo...ok ngoja niongeze na mimi j.f na necta kinara cha udini
 
Haina ubishi jk ni namba moja katika hili.
 
Haina ubishi jk ni namba moja katika hili.

Keen, unauhakika na hilo unalosema? Yaani unataka kunambia kwenye hiyo orodha ya Uyole12 huyu ndugu anatakiwa awe namba 1!!

Hapana, bado kidogo kuamini hebu dadavua kidogo ni kwa nini awa #1 ?
 
Baadhi ya mods wanaocha mada za Kipuuzi puuzi hapa JF
 
Tume ya taifa ya uchaguzi ndo namba moja kwa kueneza udini na chuki miongoni mwa watanzania
 
Keen, unauhakika na hilo unalosema? Yaani unataka kunambia kwenye hiyo orodha ya Uyole12 huyu ndugu anatakiwa awe namba 1!!

Hapana, bado kidogo kuamini hebu dadavua kidogo ni kwa nini awa #1 ?

Kamanda Bill, nimekupata vizuri. Mh. JK kama mkuu wa kaya hana namna ya kukwepa kutokuwa namba moja katika kueneza udini nchini maana yote yanafanyika chini ya uongozi wake. Meli ikizama mtu wa kwanza kumtia nguvuni ni nahodha hata kama waliosababisha au waliopelekea meli izame ni watu wengine. JK ni nahodha wa nchi yetu, kila linalotokea liwe la kiuchumi, kisiasa, kijamii, etc. anawajibika kama namba 1. Leo watu wanasifia maendeleo ya Rwanda kwa kumsifu Rais Kagame hata kama waliopelekea kuwepo na hayo maendeleo ni watendaji wake. Rais Kikwete alipewa Honorary Degree ya Udaktari wa Philosophy pengine kwa mchango wake katika maeneo fulani, kwa nini wasipewe watendaji wake kama magufuli, and the like. Mh. JK, namheshimu sana rais wangu lakini katika hili la udini lazima niwe mkweli ameshindwa kulisimamia kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi.
 
Sasa tumekwisha!Kweli hatima yataifa iko ICU!Post mods muwe nayo makini sana.Nawasilisha.
 
Kama unataka kauli yako iaminike ongeaza chadema kwenye lisit
 
Matatizo ya udini yameanzishwa na CCM wakidhani wanapambana na Dr. Slaa, sasa fitina yenu ime backfire mkiwa madarakani na kinara akiwa JK. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa serikali haina jitihada za dhati kuidhibiti hiyo hali na chokochoko za kidini.
JK aliendeleza ukinara wake wa udini katika utendaji wa serikali hasa katika teuzi alizokuwa anazifanya. Mifano ipo mingi na lawama zilishatolewa na watu wengi sina haja ya kurudia. Malipo ya hii fitna ni hapa hapa duniani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom