Vilio na kusaga meno kwa mawakala kupigwa vimezidi, Hapa nimeorodhesha baadhi ya tahadhari za kuchukua ili kupunguza utapeli

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
524
1,476
Mbinu hizi zinapunguza utapeli sio full proof guarantee, kila muda zinagunduliwa mpya

Hapa niameorodhesha baadhi ya tahadhari za kuchukua ili kuliepuka hilo:-

01. Usiwe na haraka kwenye kufanya muamala, haijalishi mteja atakuwa na haraka gani. Mruhusu aondoke kama anaonekana ana haraka, kwa sababu katika namna nyingi watu wengi wametapeliwa kwa sababu matapeli wengi wanaonekana wana haraka.

02. Usitoe hela kabla ya kuona meseji kwako, na Usiweke hela kabla ya kupewa hela na kuzihakiki.
03. Kama ukimrudishia mteja hela, akakurudishia zihakiki hela tena, uhakiki ina maana ya kuzikagua idadi na thamani yake.

04. Usimfanyie mteja muamala kwenye simu yake, muamala wa mteja hufanywa na mteja.
05. Kwa namna yoyote ile usimpe simu ya wakala mtu yeyote aidha kuweka namba au kuhakiki meseji kama imerudi. Utampa mwanya wa kupigwa.

06. Usihudumie wateja zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Weka utaratibu wa kuhudumia mteja mmoja baada ya mwingine.

07. Kwa mawakala wa AIRTEL, hakiki meseji kwenye simu ya mteja, kwa sababu kuna wakati huchukua namba na kuwatumia watu walioko mbali na eno lako, kisha wanaripoti kukosea muamala.

08. Kama kuna watu zaidi ya mmoja wametoa pesa kwa wakati mmoja, usiulize nani katoa shingapi! Muulize jina, kisha omba simu yake angalia kiasi alichotoa kama kinaendana na jina lake. Hapa kuna mchezo, wanakuja wawili wanatoa, halafu mmoja anajifanya anaongea na simu, yule mwingine anachukua hela ya huyu anayeongea na simu, akishaondoka huyu wa simu anakuja kuchukua hela na ana meseji kamili utafanyaje?

09. Usimuamini mtu yeyote, usitume pesa kwa boss wako kwa sababu amekutumia meseji! Mpigie kuhakiki kama ni yeye au lah!

10. Mtoa huduma wa simu atakupigia kukuliza kama muamala unaoombwa kurudishwa ni halali na kwamba haukumhudumia, hawatakuuliza salio, wala ni nani kafanya muamala wa shingapi! Kuwa makini na hawa watu! Mtoa huduma atakupigia kwa namba 100 TU.
Ukipokea simu yoyote mbali na 100 ikidai ni mtoa huduma, hao ni matapeli.

11. Ikiwa huna uhakika na muamala kama umeufanya au lah, unaweza kumuomba mtoa huduma akupe muda kidogo kuhakiki kama umefanya muamala huo au lah! Na utakapojiridhisha unaweza kuruhusu au kukataa.

12. Usitumie namba ya wakala kwa mawasiliano binafsi ni HATARI.

13. Usimtajie mteja float/cash uliyonayo endapo kiasi anachotaka hauko nacho. Kuna wateja wanafika wanataja hela kubwa wakitaka kujua unashingapi! Sasa mtu amekwambia anaweka milioni 1, halafu unamwambia hauna, anakuuliza una shingapi! Inahusu nini wakati hata ukimtajia haitafika milioni moja.

14. Tunza vizuri simu za uwakala, na fedha zako. USIRI NI MUHIMU.
Ahsante..

15. USIWE NA HARAKA KUFANYA MIAMALA, NI VIZURI KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA LAKINI WAKIJA NA HARAKA WARUHUSU WAENDE.

Unaweza kuongezea mbinu nyingine................
 
boss anawez kuwa anajua hii michezo ila anaemuweka dukani hajui chochote, jamani tutoe elimu sana kwa wafanyakazi wetu
 
hujazungumzia UCHAWI & USHIRIKINA kwa namna yoyote ile.

kuna mawakala wanapigwa bila kujielewa wamepigwaje

mtu akishaondoka ndio fahamu huja

au lingine kuna CHUMA ULETE kali sana kwenye hizi kazi zinazohusisha miamala.

wachunge sana
 
hujazungumzia UCHAWI & USHIRIKINA kwa namna yoyote ile.

kuna mawakala wanapigwa bila kujielewa wamepigwaje

mtu akishaondoka ndio fahamu huja

au lingine kuna CHUMA ULETE kali sana kwenye hizi kazi zinazohusisha miamala.

wachunge
Hili nalo wakaliangalie.
 
Hiyo namba 9 nilipigwa laki 3 way back ,2016
Ndugu yangu ndie alikua dukani
Mm nipo Dodoma , akatumiwa meseji kua atume laki 3 ,nae bila kuuliza akatuma
 
Pamoja na hizo mbinu, kwa ushahidi usio na mashaka, wafanyabiashara mawakala hupoteza hela kwa sababu ya kushindwa kusimamia biashara kwa kufanya hesabu sawasawa, kutunza mahesabu kwa kuweka kila record na detail ya fedha na miamala, hasa mahesabu ya kila siku wakati wa kufunga, na kushindwa kuwa na kumbukumbu sahihi na zinazoeleweka ambazo zinaweza kurejewa hata miaka 100 ijayo.

Baada ya research ya muda mrefu, tumekuja na suluhu ya kidigitali - mfumo rahisi sana kutumia, ambao utawawezesha mawakala kusubmit taarifa za kila siku za bisahara, na mfumo kufanya mahesabu yote ya kifedha, kuweka kumbukumbu, na kukupa picha ya jinsi biashara yako inavyoenda.

Kubwa zaidi, mfumo huu unamwezesha mmiliki wa biashara kupokea taarifa za mwenendo wa biashara kila siku bila yeye kuwepo eneo la biashara.

Pia unawawezesha watu zaidi ya mmoja kusubmit taarifa za biashara kutoka location yoyote ile - no time, spatial or physical constraints.

Mfumo pia una uwezo wa kufanya analytics na kukupa visual insights za trend ya biashara yako.

Pia, mfumo unaweza kutumika kumanage biashara yoyote ile.

NB: Tunaendelea kuutengenezea huu mfumo taarifa zote za kifedha - full accounting and bookkeeping packages, mfano:
  • Balance sheets.
  • Income statements.
  • Cash flow statements.
  • Statements of shareholders' equity.
  • etc.,
Kazi yako itakuwa ni kuclick tu na kugenerate report unayoitaka.

Angalia screenshot ili upate mwanga juu ya aina ya report ambayo mfumo unatengeneza:

sh1.png
sh2.png
 
Back
Top Bottom