Marekani yatafakari kuongeza vikwazo zaidi vya Chip dhidi ya China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG211287007531.jpg


Kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei, imezindua mfululizo mpya wa simu zake za kisasa za Huawei Mate 60 Pro, hatua ambayo imeendelea kuleta mshutako mkubwa nchini Marekani, ambako wabunge wenye siasa kali wanapendekeza kuongeza vikwazo vya teknolojia za chip na uwekezaji.

Ingawa bado haifahamiki vikwazo gani vingine serikali ya Marekani inaweza kuweka kufuatia mfululizo wa vikwazo vilivyopo tayari, maofisa na wataalamu wa China wanasema msako Zaidi wa Chip za China hauwezi kuzuia maendeleo ya utengenezaji wa Chip ya China, na badala yake yataimarisha ari ya China na uwezo wake wa kujitegemea kiteknolojia. Zaidi ya hayo, misako ama vikwazo kama hivyo vitaongeza maumivu katika viwanda vya Chip duniani, ikiwemo viwanda vikubwa vya nchini Marekani, ambavyo vimekuwa vikifaidika sana kutokana na mnyororo wa ngazi ya juu wa ugavi wa chip duniani.

Kufuatia toleo jipya la simu za kisasa za Huawei Mate 60 Pro, ambazo zinaripotiwa kutumia chip zilizoendelezwa za Kirin, wabunge wenye siasa kali katika Bunge la Marekani wamtoa wito wa vikwazo Zaidi vya chip dhidi ya China. Katika hatua ya hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Wawakilishi la Marekani kuhusu China, Mike Gallagher, alipanga kukutana na kundi la viwanda vya semiconductor ili kuwataka kupunguza uwekezaji wao katika sekta ya chip ya nchini China. Gallagher, ambaye ameibuka kuwa mpinzani mkubwa wa China, mara nyingi ametaka msako na vikwazo dhidi ya kampuni na viwanda vya China, huku akipanga kulitaka Shirikisho la Viwanda vya Semiconductor (SIA) la nchini Marekani kuongeza vikwazo vilivyowekwa mwaka 2022 vinavyohusu mauzo ya chip zilizoendelezwa za akili bandia kwa China na badala yake kutumia chip ambazo hazijaendelezwa.

Wachambuzi wa sekta ya viwanda nchini China wanasema, kuna uwezekano wa Marekani kuongeza vikwazo na msako kwa kampuni za China zinazopata maendeleo Dhahiri katika teknolojia za chip. Hata hivyo, kutokana na vikwazo vikubwa ambavyo tayari vipo, kuna uwezekano kuwa msako zaidi hautaleta maumivu zaidi kuliko yaliyopo sasa, na badala yake, hatua hiyo inaweza kuyadhuru Zaidi makampuni ya Marekani.

Wakati kwa mara nyingine tena kampuni ya Huawei imelengwa na wanasiasa wa Marekani kukazia kuhusu kujitenga kiteknolojia, wakurugenzi wake wamekuwa na mtazamo wa wazi kwa kampuni za Marekani, na hata washindani wake, pamoja na kuwa wanalalamikia vikali misako inayofanywa na Marekani na kuahidi kuendeleza uwezo wa kampuni hiyo.

Mwanzilishi wa kampuni ya Huawei Ren Zhengfei alipotoa hotuba mwezi Agosti mwaka huu, alisema msako wa Marekani dhidi ya kampuni za China unaleta shinikizo lakini pia unaleta hamasa, na katika miaka minne, kwa juhudi za wafanyakazi 200,000 wa Huawei, kampuni hiyo imejenga jukwaa lake lenyewe, na haitalazimika kuandamana na jukwaa la Marekani katika siku zijazo.

Wachambuzi wa masuala ya viwanda nchini China wanasema, kufuatia miaka ya msako na vikwazo vya Marekani, kampuni za China zimeimarisha uwezo wao wenyewe wa uvumbuzi, hata kama zinakabiliwa na changamoto kubwa.

Fu Liang, mchambuzi wa teknolojia aliyeko mjini Beijing anasema, maendeleo yoyote ya sekta ya chip ya nchini China yanafuatiliwa kwa karibu na wanasiasa wa Marekani, ambao pia wanataka kuchukua hatua kukandamiza zaidi kampuni zinazotengeneza chip nchini China. Ameongeza kuwa, juhudi zaidi zinatakiwa ili kuzisaidia kampuni za China kuongeza uwezo wao ili kukabiliana na hatari ya vikwazo zaidi vya Marekani.

Mchambuzi huyu anasema, jaribio lolote la kutenganisha mnyororo wa ugavi duniani utaleta madhara kwa kampuni na viwanda vyote, na kwamba kampuni za Marekani na China ndizo zitakazodhurika zaidi. Amesema wakati wanasiasa wa Marekani wanataka kuweka vikwazo Zaidi, wafanyabiashara wan chi hiyo wanajitahisi kutafuta ushirikiano kutokana na maslahi mapana yaliyopo, na kwamba ushirikiano wa aina hiyo unapaswa kuendelezwa.
 
Back
Top Bottom