China yaendelea kupaza sauti kuhusu vikundi vya nchi kukwamisha maendeleo ya nchi nyingine

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111452783346.jpg


Kwenye mkutano wa baraza kuu la 78 la umoja wa mataifa uliofanyika hivi karibuni mjini New York, Makamu wa Rais wa China Bw. Han Zheng, alirudia tena mwito ambao China imekuwa inautoa kwa muda mrefu, kwamba hatua za upande mmoja ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya nchi nyingine duniani, na hatua hizo zinaleta mateso na maumivu kwa wahanga bila kuwa na mafanikio yoyote.



Katika hotuba yake ya dakika 15, Makamu wa Rais wa China Bw. Han Zheng alitaja mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kueneza umwamba (hegemonisim), hatua za upande mmoja (unilateralism) na kuendeleza hisia za vita baridi. Bw. Han alitoa wito jamii ya kimataifa kukabiliana na mfumo usio wa haki uliopo sasa kwa pamoja.



Alichokisema Bw. Han ni jambo linaloonekana wazi kwenye dunia ya sasa na limekuwa ni changamoto kubwa kwa usalama na maendeleo ya dunia nzima, haswa katika nchi mbalimbali zinazoendelea. Kwa mfano, Marekani imekuwa ikitumia kinachoitwa tunu za magharibi (western values) kama vile demokrasia na haki za binadamu, kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kuzishawishi nchi rafiki za magharibi kuziadhibu nchi zinazoonekana kwenda kinyume na matakwa yake. Kisingizio cha vikwazo hivyo ni kwamba, kuzibana serikali na kuepusha shari zaidi, lakini ukweli ni kuwa vinaleta maumivu zaidi kwa watu wa kawaida.



Nchi za Afrika ndio zimekuwa wahanga wakubwa wa hatua za upande mmoja za vikwazo vya kiuchumi vya Marekani, ni pamoja na Burundi, Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mali, Libya, Zimbabwe, Somalia, Sudan Kusini. Lakini vikwazo hivyo vikiangaliwa kwa undani, vinaonesha kuwa ni chuki binafsi ya Marekani na sio kama vinalenga matatizo, na wakati mwingine inaonekana kama vinawekwa tu na kuachwa viendelee kuwepo hata bila sababu ya msingi.



Mfano mzuri ni nchi Zimbabwe, ambapo Umoja wa Afrika na nchi mbalimbali za Afrika wamekuwa wakipaza sauti ya kuondolewa kwa vikwazo hivyo, kwani vimesababisha upungufu wa chakula, dawa na hata huduma za msingi kwa watu wa kawaida wa Zimbabwe. Imekuwa ni wazi kabisa kuwa vikwazo hivyo ambavyo Marekani na nchi za magharibi zinadai kuwa vimewekwa dhidi ya serikali ya Zimbabwe na maofisa wake, vinawalenga watu wa Zimbabwe. Kibaya zaidi ni kuwa kwenye orodha ya watu waliowekwa kwenye orodha hiyo pia yupo aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe aliyefariki mwaka 2019.



Licha ya kuwa makamu wa Rais wa China aliongea kwa muda mfupi, alichoongea kimeungwa mkono na nchi nyingi zinazoendelea hasa nchi za Afrika, kwani alichosema ni kweli. Ni wazi kabisa kuwa inachopeleka China kwenye nchi za dunia ya tatu ni miundombinu, biashara na fursa kwa nchi hizo, hicho ni tofauti kabisa na kinachopelekwa na Marekani. Ni wazi kabisa kuwa kwenye machaguo haya mawili, wenye busara watajua ni upande gani wa kuufuata.
 
Back
Top Bottom