☯️🔴🔵 VIJUE VIGEZO (17) VYA KUTOFAUTISHA MABASI (DARAJA LA KAWAIDA, DARAJA LA KATI NA LA KIFAHARI)

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,907
Ukiwa na changamoto yoyote kwenye basi, wasiliana na LATRA 0800110020.
MAGUFULI BUS TERMINAL 0734450010.


Watu wengi au abiria bado hatuna elimu ya kutofautisha haya madaraja ya mabasi licha ya mamlaka kupanga nauli kulingana na vyombo husika bado tunahitaji uelimishwaji wa hali ya juu. Leo ungana nami kuna kitu kipya utakipata

Mabasi yapo kwenye madaraja tofauti kulingana na vigezo vinavyotumika na mamlaka kutoa leseni ya usafirishaji lakini leo tuangalie haya madaraja matatu (3) ambayo yamezoeleka hapa nchini kwetu Tanzania

1. Daraja la Kawaida (Ordinary Bus)
2.Daraja la Kati (Semi- Luxury Bus )
3.Daraja la Kifahari (Luxury Bus)

Vifuatavyo ni Baadhi ya Vigezo Unavyoweza Kutumia Kutofautisha Mabasi Kulingana na Madaraja Yake

(I) Kigezo: Ukomo wa Urefu wa Basi

Daraja la Kawaida: mita 12.5
Daraja la Kati: mita 12.5
Daraja la Kifahari: mita 12.5

(ii) Kigezo: Ukomo wa Upana wa Basi

Daraja la Kawaida: mita 2.6
Daraja la Kati: mita 2.6
Daraja la Kifahari: mita 2.6

(iii) Kigezo: Ukomo wa Kimo (Urefu wa Kwenda Juu)
Daraja la Kawaida: mita 4.6
Daraja la Kati: mita 4.6
Daraja la Kifahari: mita 4.6

(iv) Kigezo: Uwezo wa Kubeba Watu(Abiria)-Jumuisha na Dereva (Seating Capacity)

Daraja la Kawaida: 65
Daraja la Kati: 60
Daraja la Kifahari: 51/60

(v) Kigezo: Hali ya Mahitaji ya Viti

Daraja la Kawaida: Endapo viti vipo kwenye uelekeo mmoja umbali wa egemeo kati ya kiti cha mbele na nyuma usizidi milimita 680 na kwa hapo si lazima kiti cha abiria kiwe cha kurekebishika (adjustable)

Daraja la Kati: Viti vyote vya abiria lazima viwe vinarekebishika (adjustable) na endapo viti vipo kwenye uelekeo mmoja umbali wa egemeo kati ya kiti cha mbele cha abiria na nyuma yake usipungue milimita 690

Daraja la Kifahari: Sawa na daraja la Kati

(vi) Kigezo: Mpangilio wa Viti Kwa Ukubwa

Daraja la Kawaida: 3x2 au 2x2 (Yaani mstari mmoja wa viti uwe na vitatu vitatu na mwingine uwe na viwili viwili

Daraja la Kati: 2x2 (Yaani kila mstari kwenye basi pande zote mbili ziwe na viti viwili viwili

Daraja la Kifahari: Sawa na Daraja la Kati

(vii) Kigezo: Mikanda Kwenye Viti

Daraja la Kawaida: Viti vyote vya abiria pamoja na kiti cha dereva viwe na mkanda wa kutumia kwa ajili ya usalama

Daraja la Kati:Sawa na Daraja la Kawaida
Daraja la Kifahari: Sawa na Daraja la Kawaida

(viii) Kigezo:Taa za Ndani

Daraja la Kawaida: Angalau lazima ziwepo taa 3 za kutumia na ziwekwe umbali sawa

Daraja la Kati: Angalau kwenye kila mpangilio wa siti za abiria kuwepo taa juu ya kuangaza mwanga

Daraja la Kifahari: Sawa na Daraja la Kati

(ix) Kigezo: Kiyoyozi

Daraja la Kawaida: Si lazima kiwepo

Daraja la Kati:Si lazima kiwepo

Daraja la Kifahari: Lazima Kiyoyozi Kiwepo

(x) Kigezo: Redio na Kaseti ya Redio

Daraja la Kawaida:Ni hiari kuwepo (Si lazima)

Daraja la Kati: Lazima viwepo

Daraja la Kifahari:Sawa na Daraja la Kati

(xi) Kigezo: Televisheni (TV)

Daraja la Kawaida: Hakuna TV /Ni hiari

Daraja la Kati: Lazima TV iwepo

Daraja la Kifahari: Sawa na Daraja la Kati

(xii) Kigezo: Microphone/Kipaza Sauti

Daraja la Kawaida:Muhimu Kiwepo

Daraja la Kati: Muhimu Kiwepo

Daraja la Kifahari: Muhimu Kiwepo

(xiii) Kigezo: Heater (Tumezoea neno "Hita" yaani Kifaa Maalum Cha Kuchemsha/Kupasha vinywaji viwe vya moto

Daraja la Kawaida: Ni hiari kuwepo

Daraja la Kati: Ni hiari kuwepo

Daraja la Kifahari:Lazima kuwepo na Heater ya kuchemsha maji na kutengeneza vinywaji mfano kahawa, chai n.k

(xiv) Kigezo: Friji/Kifaa Maalum Cha Kugandisha

Daraja la Kawaida:Ni hiari kuwepo

Daraja la Kati: Ni hiari kuwepo

Daraja la Kifahari: Lazima kuwepo

(xv) Kigezo: Utolewaji wa Vinywaji

Daraja la Kawaida: Ni hiari

Daraja la Kati: Ni hiari

Daraja la Kifahari : Lazima kuwepo usambazaji wa vinywaji baridi

(xvi) Kigezo: Pazia Madirishani

Daraja la Ni hiari

Daraja la Kati: Muhimu Kuwepo

Daraja la Kifahari: Muhimu Kuwepo

(xvii) Kigezo: Huduma za Choo cha Ndani

Daraja la Kawaida: Hakuna huduma za choo cha ndani

Daraja la Kati: Hakuna huduma za choo cha ndani

Daraja la Kifahari: Ni Muhimu Kuwepo
 
Nimepitia hivyo vigezo, nimegundua ni usanii kwa 100%. Kivipi?

1. Zaidi ya 70% ya hivyo vigezo havina tofauti kati ya daraja la kati na juu. Vinafanana kwa madaraja yote.

2. Zaidi ya 70% ya vigezo vya kujitofautisha kati ya daraja na kawaida na daraja la juu sio vigezo vya lazima. Vimetajwa kama vigezo muhimu lakini sio vigezo vya ulazima.

3. Kuna vigezo vinavyohitaji kufuatiliwa na kusimamiwa wakati wote wa safari ili basi likidhi kuwa daraja la juu, jambo ambalo haliwezekani. Kwa mfano
-Ugawaji wa vinywaji baridi
-Taa zinazowaka
-AC inayofanya kazi kwa ufanisi wakati wote wa safari.
-Redio inayofanya kazi
-Friji inayofanya kazi.0


Swali kuu kuliko yote ni hili, nani huwa anawajibika kukagua hayo mabasi mwanzo wa safari, katikati ya safari au mwisho wa safari ili kuona vigezo vimezingatiwa?
 
Nimepitia hivyo vigezo, nimegundua ni usanii kwa 100%. Kivipi?

1. Zaidi ya 70% ya hivyo vigezo havina tofauti kati ya daraja la kati na juu. Vinafanana kwa madaraja yote.

2. Zaidi ya 70% ya vigezo vya kujitofautisha kati ya daraja na kawaida na daraja la juu sio vigezo vya lazima. Vimetajwa kama vigezo muhimu lakini sio vigezo vya ulazima.

3. Kuna vigezo vinavyohitaji kufuatiliwa na kusimamiwa wakati wote wa safari ili basi likidhi kuwa daraja la juu, jambo ambalo haliwezekani. Kwa mfano
-Ugawaji wa vinywaji baridi
-Taa zinazowaka
-AC inayofanya kazi kwa ufanisi wakati wote wa safari.
-Redio inayofanya kazi
-Friji inayofanya kazi.0


Swali kuu kuliko yote ni hili, nani huwa anawajibika kukagua hayo mabasi mwanzo wa safari, katikati ya safari au mwisho wa safari ili kuona vigezo vimezingatiwa?
CCM kupitia LATRA wanatuzingua
 
Kwa uchambuzi wao ni wa Bus Coach, Kwenye daraja la Juu kuna Sleeplinner Bus ingawa Tanzania hakuna.

Daraja la juu basi inaweza kuwa Luxury Coach au Sleepliner. Kwenye seat zinakuwa na uwezo wa kulala mpaka angle 30 au pungufu mithili ya kitanda na space ni kubwa na seat inaegemeo la miguu.
 
Back
Top Bottom