Vijiji vya Bwasi, Bugunda na Kome kuanza kupata Maji ya Bomba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MAJI YA BOMBA YAENDELEA KUSAMBAZWA MUSOMA VIJIJINI - VIJIJI VYA BWASI, BUGUNDA NA KOME KUPATA MAJI HIVI KARIBUNI

RUWASA inaendelea kufanya kazi nzuri ya kutekeleza miradi ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini.

Jimbo letu lenye Kata 21, lina Vijiji 68 vyenye Vitongoji 374. Vijiji vyote vina miradi ya maji ambayo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Bomba la Bujaga-Bulinga-Busungu

Maji ya bomba hili yanatoka Ziwa Victoria na mashine imejengwa Kijijini Bujaga (Kata ya Bulinga)

Tenki la ujazo wa LITA 200,000 limejengwa Kijijini Busungu (Kata ya Bulinga) na lingine la LITA 150,000 limejengwa Kijijini Bulinga (Kata ya Bulinga)

Maji kutoka kwenye matenki hayo ndiyo yanasambazwa kwenye Vijiji vya Bukima (Kata ya Bukima) na Kwikerege (Kata ya Rusoli)

Mradi wa upanuzi: Bwasi-Bugunda-Kome

Upanuzi unafanyika ili maji ya Bomba la Bujaga-Bulinga-Busungu yasambazwe na kutumiwa kwenye Kata ya Bwasi yenye Vijiji vitatu (Bugunda, Kome na Bwasi).

Gharama ya Mradi:
*Tsh 997,714,196

Urefu wa mtandao wa usambazaji maji:
*Kilomita 31.5
*Vitekea maji 35

Tenki la ujazo la LITA 150,000 linajengwa Kijijini Bwasi

Mradi huu umepangwa ukamilike kabla ya tarehe 30.6.2023

SHUKRANI za dhati zinatolewa kwa Serikali yetu inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusambaza maji safi na salama ya bomba vijijini mwetu.

Picha za hapa zinaonesha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini Bwasi, Bugunda na Kome, Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Ijumaa, 5.5.2023
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-05 at 16.45.18.mp4
    9.8 MB
  • WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.18.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.18.jpeg
    112 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.17.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.17.jpeg
    105.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.18(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.18(1).jpeg
    136.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.19.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.19.jpeg
    115.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.19(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-05 at 16.45.19(1).jpeg
    113.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom