Vijana wengi wanaishi FAKE LIFE, wasikupe presha

Nebuchadneza

JF-Expert Member
Oct 6, 2023
415
1,032
Moja kwa moja nazama kwenye hoja nikiwa najiuliza kwanini vijana wengi wanapenda kuishi FAKE LIFE.

Kwanini ukarifishe moyo? Yanini hujipe presha?

Asilimia kubwa ya vijana wengi wanaigiza maisha yao,utawaona wanapost kwenye mitandao kuwa wana maisha manzuri kiukwel ni makapuku ya kutupwa,wanaigiza kwa jamii wana good life ila wenyewe wanaishi maisha magumu.

Utawakuta wamekopa pesa kwa watu ili wanunue nguo na viatu vya bei ya juu,wanashindwa kurudisha mikopo hiyo na kusababisha kulipwa tako.

Ishi maisha yako usiige kwa mtu atakama mmelingana umri kama kakuzidi kakuzidi tu yanini hujipe mawazo nakutaka maisha yao?

Ukikutana nao mtaani utawashangaa sana,ni makapuku ya kutupwa,wengi wanapost wameegemea magari ya watu, hash tag yao sasa tafuta pesa.

Ishi maisha yako maana ni yako yanini kuiga ya mtu,ulimbukeni na ushamba wa kijinga kujisifiwa kuwa una pesa.

Vijana tuache sifa za kijinga,tutafute pesa zetu iwe Mia ni yako umeitafuta kwa jasho,tusipende kuiga.

Ni hayo tu
 
Kuna Mmoja last week kapost yupo Zanzibar kaenda na Ndege full kujirekodi, haya Juzi kapost tena kaenda Zanzibar kwa BOAT la Azam kakaa VIP... na Hotel alifikia zile za Kitalii mivimbo mingii..

Haya bhana jana ikabidi anivutie waya kwamba Mambo magumu anahitaji Kazi yoyote ya mkataba. (Anafanya sehem kama Intern so anapelekwa bure bure).

Mie nikamuuliza tuu ni kwel au unanitania aksema yupo serious.... hana hata balance ya nauli ya wiki nzima.

Nikajifunza Watu wengi wanafake LIFE ili kupunguza mifadhaiko ya Kimaisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom