Zito aliaminiwa sana katika CHADEMA, na ndio maana pamoja na kuwa na umri mdogo, aliibuka na vyeo vikubwa vikubwa katika Chama. tatizo lake ni kwamba hakuwa na subira. kwa kuwa ni kijana mdogo, alitakiwa aendelee kutumikia chama kwa uaminifu kama alivyofanya Slaa. ilibidi aendelee kupata "trust" ya wengi katika chama. mbona JK alipoenguliwa kugombea urais mwaka 1995 hakuhama chama wala hakuanzisha zogo? alivuta subira na akaja kushinda kwa kishindo mwaka 2005. kama kweli Zito alikuwa anaipenda Chadema, asingetumia njia hiyo ya confrotation, akijua kwamba angekigawa chama. amekiumiza chama kwa maslahi binafsi, kiasi kwamba hata CCM wanamtetea. sasa ukiona mpinzani unatetewa na CCM, ujue wewe siyo mpinzani wa kweli.