Vijana wengi wa Marekani wamekata tamaa na siasa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG31460510585.JPG

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 29 nchini Marekani yaliyotolewa Aprili 25 na Taasisi ya Siasa ya Kennedy ya chuo kikuu cha Harvard HKS, 36% ya waliohojiwa wanaona kuwa "shughuli za kisiasa ni nadra kuzaa matokeo halisi", na 42% ya waliohojiwa walisema kura zao "hazikuwa na athari yoyote". Utafiti huo pia uligundua kuwa asilimia 59 ya vijana Wamarekani wenye asili ya Afrika, asilimia 43 ya vijana Wamarekani wenye asili ya Asia na asilimia 37 ya vijana Wamarekani wenye asili ya Hispania walisema walishambuliwa "mara nyingi" nchini Marekani. Kwa hakika, magonjwa mengi sugu katika jamii ya Marekani, kama vile matumizi ya bunduki, ubaguzi wa rangi, dhuluma ya kijamii, na pengo kati ya tajiri na maskini, yanaathiri maendeleo na mustakabali wa vijana wa Marekani.

Vijana wa Marekani wanajitumbukiza kwenye hali mbaya ya kiuchumi

Tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, vijana wa Marekani wamekuwa moja ya makundi yanayoathiriwa zaidi kiuchumi. Kulingana na takwimu kutoka Ofisi ya Sensa ya Marekani, mwaka 2020 kiwango cha umaskini nchini Marekani kilipanda juu zaidi kwenye historia hadi 11.4%, na idadi ya watu maskini ilifikia milioni 37.2. Miongoni mwao, kiwango cha umaskini cha watu walio chini ya umri wa miaka 18 kiliongezeka kutoka 14.4% ya mwaka 2019 hadi 16.1% ya mwaka 2020.

Watu zaidi na zaidi wanatafuta msaada wa chakula kote Marekani, wakiwemo vijana. Hivi majuzi kulikuwa na video kwenye mtandao wa kijamii wa TIKTOK, ambapo msichana mdogo wa Marekani akiwa amekaa kwenye ngazi mbele ya nyumba huku masimulizi yakisema "Wamarekani milioni 49 wanateseka kwa ukosefu wa chakula, lakini wanachohitaji zaidi sio mlo mmoja, bali ni mabadiliko." Ndani ya siku tatu tu, video ilipata likes zaidi ya milioni 1.7 na kutazamwa na watu milioni 9.3. Hili ni tangazo la huduma za umma lililopigwa mwaka 2015 na shirika lisilotafuta faida la Marekani "Share Our Strength". Laura Washburn, msemaji wa shirika hilo, alisema, "Video hii ilikusudiwa kutafuta ufuatiliaji wa watu kwa tatizo la njaa nchini Marekani. Kwa bahati mbaya, nchi yetu bado inashughulikia tatizo hili hadi leo."

Vijana wa Marekani wanakata tamaa na Demokrasia ya Marekani

Hali mbaya ya kiuchumi, pamoja na kuongezeka kwa matatizo ya kijamii na migawanyiko ya kisiasa nchini Marekani, imewafanya vijana wa Marekani kukata tamaa na aina ya demokrasia ya Marekani. Mwishoni mwa mwaka jana, Taasisi ya Siasa ya Kennedy katika Chuo Kikuu cha Harvard ilifanya utafiti wa vijana wa Marekani. Katika utafiti huo, ni asilimia 7 tu ya vijana waliohojiwa walifikiri aina ya demokrasia ya Marekani ilikuwa bora, wakati asilimia 55 walifikiri kwamba mustakabali wa Marekani ulikuwa ukisuasua. Taasisi hiyo ilieleza kuwa utawala usiofaa wa Biden na marais kadhaa waliopita unasababisha kizazi cha vijana wa Marekani kupoteza "imani" na hisia ya kujiamini kuwa bora.

Hivi majuzi, kulitokea tukio la ufyatuaji risasi katika shule ya sekondari mjini Detroit, jimboni Michigan, Marekani. Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ethan Clumberley mwenye umri wa miaka 15 aliwafyatulia risasi wanafunzi wenzake shuleni na kuwaua wanafunzi wanne na kuwajeruhi wengine saba. Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani CDC, mwaka wa 2019, mashambulizi ya bunduki yalikuwa sababu ya pili ya vifo vya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 nchini Marekani, na kila watu laki moja, kuna 17.4 waliouawa kwa bunduki. Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia Ghasia za Bunduki katika kituo cha afya cha Northwell, mfumo mkubwa zaidi wa afya mjini New York Chethan Sathya alisema, umaskini, ukosefu wa usawa kwenye jamii, na matumizi ya bunduki vinahusiana kwa karibu. "Huwezi tu kutatua moja bila kutatua mengine, na vijana wa Marekani wanatoa tahadhari.” alisema John Volpe, mkurugenzi wa masuala ya upigaji kura za maoni katika taasisi ya siasa ya Kennedy ya Chuo kikuu cha Havard.

Vijana wa Wamarekani wana mashaka zaidi Kuhusu 'Ndoto ya Marekani'

Jarida la "The Atlantic " la Marekani hivi majuzi lilisema kutokana na serikali kushindwa kudhibiti janga hilo, takriban watoto laki 2 wa Marekani wamekuwa yatima, ambao asilimia 65 kati yao walitoka familia za kipato cha chini, zisizo za watu weupe. Miongoni mwa yatima hao wapya 200,000 wengi wao wamekuwa kwenye tabaka la chini katika jamii ya Marekani tangu kuzaliwa kwao na wana nafasi ndogo ya kubadili hatima yao. Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 30 kuanzia 1980 hadi 2010, Marekani ndiyo nchi pekee iliyoendelea ambayo wastani wa kipato cha watu wa tabaka la chini kilidumaa bila kuongezeka. Janga hilo pia limewachukua wazazi wao na kutumbukiza maisha yao katika hali mbaya zaidi, na kwamba kuacha shule, matumizi ya dawa za kulevya, na vurugu huenda mambo haya yakawaandama katika maisha yao yote. Kama alivyosema Susan Hillis, mwenyekiti mwenza wa timu ya tathmini ya watoto walioathiriwa na Covid-19 duniani, "Kuwa yatima sio jambo ambalo linaweza kupona baada ya wiki mbili."

Tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, serikali ya Marekani imetoa msaada wa matrilioni ya dola, na fedha walizo nazo matajiri wakubwa zaidi zimeongezeka hata kwa 50% wakati wa janga hilo, lakini hakuna sheria au kanuni ya kiutendaji iliyotoa ulinzi kwa hawa yatima. Mtaalamu wa masuala ya jamii wa Marekani Charles Mills aliwahi kusema katika kitabu cha "Power Elite" kuwa "demokrasia ya Marekani inatawaliwa na watu wachache wenye mali na mamlaka, na kwa kweli ni fantasia ya kudanganya umma!"

Matatizo kama vile pengo kati ya tajiri na maskini, ukosefu wa haki kwenye jamii, na migogoro kati ya watu wenye rangi tofauti yamewafanya vijana wa leo wa Marekani wasijivunie tena na nchi yao. Gazeti la "Newsweek" la Marekani lilinukuu matokeo ya kura za maoni ya kampuni ya ushauri ya Gallup yakisema kwamba hisia ya jumla ya kujivunia ya vijana wa Marekani ilishuka hadi kiwango cha chini zaidi kihistoria mwaka 2020, ambapo ni asilimia 36 tu ya waliohojiwa wenye umri wa miaka 18 hadi 24 "waliojivunia kuwa Wamarekani”, huku asilimia 35 ya waliohojiwa walisema "wanajivunia kidogo, au hawakujivunia kabisa kuwa Wamarekani."
 
Hilo la kutojivunia utaifa wako lipo kote hats kwa jirani zetu Tanzania.
Mtanzania Bora ajitambulishe kuwa mkenya kuliko utanzania.
Nb ishu ya ukabila mtz Ni Bora ajitambulishe kuwa mchaga, mnyakyusa, mpare lakini sio mnyiramba, mmasai ama mmang'ati.
 
Kichwa chako kimejaa maji badala ya akili?
Nyinyi kenya mna nn cha maana kuizidi Tz mpaka mtu akane utaifa wake eti kisa kinchi chenu uchwara.
 
Hilo la kutojivunia utaifa wako lipo kote hats kwa jirani zetu Tanzania.
Mtanzania Bora ajitambulishe kuwa mkenya kuliko utanzania.
Nb ishu ya ukabila mtz Ni Bora ajitambulishe kuwa mchaga, mnyakyusa, mpare lakini sio mnyiramba, mmasai ama mmang'ati.
Yaan wewe mkikuyu una vituko. Huko Kenya Kuna nn Cha kujivunia. Yaan huko ndo Kuna shida zaidi kuliko huku Tanzania. Mlivyo na life ngumu hivyo mnalinganisha na Tanzania.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Kuna vitu vinaniahangazaga sana kwenye nchi za ulaya na Marekani kwamba gharama za chakula, nyumba umeme ni kubwa kuliko kawaida inashangaza mtu anafanya kazi zaidi ya tatu Ila bado life haliko Sawa itambidi asave kuliko kawaida Africa tuko nyuma na mambo mengi Ila dah maisha yetu yanaurahisi kiasi chake

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
ikitokea tanzania basi kelele zake sasa
 
View attachment 2227466

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 29 nchini Marekani yaliyotolewa Aprili 25 na Taasisi ya Siasa ya Kennedy ya chuo kikuu cha Harvard HKS, 36% ya waliohojiwa wanaona kuwa "shughuli za kisiasa ni nadra kuzaa matokeo halisi", na 42% ya waliohojiwa walisema kura zao "hazikuwa na athari yoyote". Utafiti huo pia uligundua kuwa asilimia 59 ya vijana Wamarekani wenye asili ya Afrika, asilimia 43 ya vijana Wamarekani wenye asili ya Asia na asilimia 37 ya vijana Wamarekani wenye asili ya Hispania walisema walishambuliwa "mara nyingi" nchini Marekani. Kwa hakika, magonjwa mengi sugu katika jamii ya Marekani, kama vile matumizi ya bunduki, ubaguzi wa rangi, dhuluma ya kijamii, na pengo kati ya tajiri na maskini, yanaathiri maendeleo na mustakabali wa vijana wa Marekani.

Vijana wa Marekani wanajitumbukiza kwenye hali mbaya ya kiuchumi

Tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, vijana wa Marekani wamekuwa moja ya makundi yanayoathiriwa zaidi kiuchumi. Kulingana na takwimu kutoka Ofisi ya Sensa ya Marekani, mwaka 2020 kiwango cha umaskini nchini Marekani kilipanda juu zaidi kwenye historia hadi 11.4%, na idadi ya watu maskini ilifikia milioni 37.2. Miongoni mwao, kiwango cha umaskini cha watu walio chini ya umri wa miaka 18 kiliongezeka kutoka 14.4% ya mwaka 2019 hadi 16.1% ya mwaka 2020.

Watu zaidi na zaidi wanatafuta msaada wa chakula kote Marekani, wakiwemo vijana. Hivi majuzi kulikuwa na video kwenye mtandao wa kijamii wa TIKTOK, ambapo msichana mdogo wa Marekani akiwa amekaa kwenye ngazi mbele ya nyumba huku masimulizi yakisema "Wamarekani milioni 49 wanateseka kwa ukosefu wa chakula, lakini wanachohitaji zaidi sio mlo mmoja, bali ni mabadiliko." Ndani ya siku tatu tu, video ilipata likes zaidi ya milioni 1.7 na kutazamwa na watu milioni 9.3. Hili ni tangazo la huduma za umma lililopigwa mwaka 2015 na shirika lisilotafuta faida la Marekani "Share Our Strength". Laura Washburn, msemaji wa shirika hilo, alisema, "Video hii ilikusudiwa kutafuta ufuatiliaji wa watu kwa tatizo la njaa nchini Marekani. Kwa bahati mbaya, nchi yetu bado inashughulikia tatizo hili hadi leo."

Vijana wa Marekani wanakata tamaa na Demokrasia ya Marekani

Hali mbaya ya kiuchumi, pamoja na kuongezeka kwa matatizo ya kijamii na migawanyiko ya kisiasa nchini Marekani, imewafanya vijana wa Marekani kukata tamaa na aina ya demokrasia ya Marekani. Mwishoni mwa mwaka jana, Taasisi ya Siasa ya Kennedy katika Chuo Kikuu cha Harvard ilifanya utafiti wa vijana wa Marekani. Katika utafiti huo, ni asilimia 7 tu ya vijana waliohojiwa walifikiri aina ya demokrasia ya Marekani ilikuwa bora, wakati asilimia 55 walifikiri kwamba mustakabali wa Marekani ulikuwa ukisuasua. Taasisi hiyo ilieleza kuwa utawala usiofaa wa Biden na marais kadhaa waliopita unasababisha kizazi cha vijana wa Marekani kupoteza "imani" na hisia ya kujiamini kuwa bora.

Hivi majuzi, kulitokea tukio la ufyatuaji risasi katika shule ya sekondari mjini Detroit, jimboni Michigan, Marekani. Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ethan Clumberley mwenye umri wa miaka 15 aliwafyatulia risasi wanafunzi wenzake shuleni na kuwaua wanafunzi wanne na kuwajeruhi wengine saba. Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani CDC, mwaka wa 2019, mashambulizi ya bunduki yalikuwa sababu ya pili ya vifo vya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 nchini Marekani, na kila watu laki moja, kuna 17.4 waliouawa kwa bunduki. Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia Ghasia za Bunduki katika kituo cha afya cha Northwell, mfumo mkubwa zaidi wa afya mjini New York Chethan Sathya alisema, umaskini, ukosefu wa usawa kwenye jamii, na matumizi ya bunduki vinahusiana kwa karibu. "Huwezi tu kutatua moja bila kutatua mengine, na vijana wa Marekani wanatoa tahadhari.” alisema John Volpe, mkurugenzi wa masuala ya upigaji kura za maoni katika taasisi ya siasa ya Kennedy ya Chuo kikuu cha Havard.

Vijana wa Wamarekani wana mashaka zaidi Kuhusu 'Ndoto ya Marekani'

Jarida la "The Atlantic " la Marekani hivi majuzi lilisema kutokana na serikali kushindwa kudhibiti janga hilo, takriban watoto laki 2 wa Marekani wamekuwa yatima, ambao asilimia 65 kati yao walitoka familia za kipato cha chini, zisizo za watu weupe. Miongoni mwa yatima hao wapya 200,000 wengi wao wamekuwa kwenye tabaka la chini katika jamii ya Marekani tangu kuzaliwa kwao na wana nafasi ndogo ya kubadili hatima yao. Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 30 kuanzia 1980 hadi 2010, Marekani ndiyo nchi pekee iliyoendelea ambayo wastani wa kipato cha watu wa tabaka la chini kilidumaa bila kuongezeka. Janga hilo pia limewachukua wazazi wao na kutumbukiza maisha yao katika hali mbaya zaidi, na kwamba kuacha shule, matumizi ya dawa za kulevya, na vurugu huenda mambo haya yakawaandama katika maisha yao yote. Kama alivyosema Susan Hillis, mwenyekiti mwenza wa timu ya tathmini ya watoto walioathiriwa na Covid-19 duniani, "Kuwa yatima sio jambo ambalo linaweza kupona baada ya wiki mbili."

Tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, serikali ya Marekani imetoa msaada wa matrilioni ya dola, na fedha walizo nazo matajiri wakubwa zaidi zimeongezeka hata kwa 50% wakati wa janga hilo, lakini hakuna sheria au kanuni ya kiutendaji iliyotoa ulinzi kwa hawa yatima. Mtaalamu wa masuala ya jamii wa Marekani Charles Mills aliwahi kusema katika kitabu cha "Power Elite" kuwa "demokrasia ya Marekani inatawaliwa na watu wachache wenye mali na mamlaka, na kwa kweli ni fantasia ya kudanganya umma!"

Matatizo kama vile pengo kati ya tajiri na maskini, ukosefu wa haki kwenye jamii, na migogoro kati ya watu wenye rangi tofauti yamewafanya vijana wa leo wa Marekani wasijivunie tena na nchi yao. Gazeti la "Newsweek" la Marekani lilinukuu matokeo ya kura za maoni ya kampuni ya ushauri ya Gallup yakisema kwamba hisia ya jumla ya kujivunia ya vijana wa Marekani ilishuka hadi kiwango cha chini zaidi kihistoria mwaka 2020, ambapo ni asilimia 36 tu ya waliohojiwa wenye umri wa miaka 18 hadi 24 "waliojivunia kuwa Wamarekani”, huku asilimia 35 ya waliohojiwa walisema "wanajivunia kidogo, au hawakujivunia kabisa kuwa Wamarekani."
Dah mbona mnatukatisha tamaa sisi ambao tuna mipango ya kwenda kubeba boksi huko.
 
Hilo la kutojivunia utaifa wako lipo kote hats kwa jirani zetu Tanzania.
Mtanzania Bora ajitambulishe kuwa mkenya kuliko utanzania.
Nb ishu ya ukabila mtz Ni Bora ajitambulishe kuwa mchaga, mnyakyusa, mpare lakini sio mnyiramba, mmasai ama mmang'ati.
Una matatizo wewe ya akili

Yaani tumewazidi kuanzia maliasili za Taifa hadi uzuri wa muonekano

Sasa tujitambulishe kwa Taifa hilo ili tupate nini

Em nenda tu hapo South Africa uone kati ya Mkenya na Mtz nani anaheshimika pale na kuonekana mjanja

Achana na propaganda za media.
 
Back
Top Bottom