Vijana watakiwa kuacha tabia ya kuwakimbia wagonjwa wao wanaowapeleka Hospitali ya Mwananyamala

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Ujumbe wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Dar es Salaam umetembelea Hospitali ya Mwananyamala Jijini hapo kuwajulia hali wagonjwa mbalimbali, leo Oktoba 14, 2023 ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere kilichotokea Oktoba 14, 1999.

Msafara huo ulioongozwa na Sheikh Ally Khamis Ngeruko ambaye ni Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania pamoja na Mussa Omary ambaye ni Katibu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Dar es Salaam, kisha kukabidhi baadhi ya mahitaji muhimu kwa wagonjwa mbalimbali.
Capture.JPG
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mahitaji kadhaa muhimu yaliyotolewa na taasisi hiyo, Sheikh Khamis Ngeruko amesisitiza jamii hasa vijana kuzingatia maadili na kuwajibika katika kusaidia watu wenye mahitaji ili kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Amesema “Tumetembelea na kuona wagonjwa na viongozi, changamoto mojawapo tuliyoisikia na kuikuta hapa ni baadhi ya watu kutelekeza wagonjwa wao hasa vijana.
Capture2.JPG

Capture3.JPG
“Changamoto hiyo inaweza kuwa inachangiwa na malezi, vijana wanawaleta walezi wao au watu ambao wanatakiwa kuwahudumia kisha wao wanawatelekeza, shida hii inachangiwa na malezi ya familia ambapo kumekuwa na changamoto kadhaa.

“Tunatoa wito kwa viongozi kuwajibika na kusimamia maadili, Mwalimu Nyerere alikuwa akisisitiza zaidi kuhusu maadili na malezi, alikuwa mlezi na kiongozi, aliweka misingi kwa vijana.

“Vijana wa sasa wanafikiria kila jukumu ni la Serikali wanashindwa kuelewa wao pia ni Serikali, japokuwa hilo nalo linaweza kuwa linatokana na wao kukosa maelekezo, hivyo ni lazima viongozi na walezi wasimamie misingi ya maadili.”

Katibu wa Taasisi
Upande wa Mussa Omary ambaye ni Katibu wa Taasisi amesema “Tunaendeleza fikra na falsafa za Mwalimu kuendeleza mazuri ambayo yalifanywa na Mwalimu kwa kumgusa mtu mmoja mmoja kwa namna ya kipekee, tumeona changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo hiyo iliyosemwa na watoto kuwakimbia wazazi wao.

“Serikali haiwezi kufanya kila kitu, pia tunaposema Serikali siyo tu ule uongozi wa Nchi bali kila mtu ni Serikali, hivyo tushirikiane kutoa usaidizi wa kuwasaidia wenzetu kwa jinsi uwezo wetu unavyoruhusu.

“Kuna Wadi moja ya Watoto tulikuta kuna joto sana, ndio maana leo hii moja kati ya vitu tulivyoleta ni mashine ya maji ya kunywa kwa ajili ya kuwasaidia watoa huduma wanaokuwa katika majukumu hayo.

“Tunamshukuru Rais kwa kuendeleza miradi iliyokuwa ikiendelea ikiwemo Hospitali ya Mwananyamala ambapo kuna majengo yameongezeka, tunamshukuru Mganga Mkuu wa Kinondoni, DMO wa Manispaa ya Kinondoni, Meya wa Kinondoni kwa kupambana kufanikisha tunafanikiwa katika hili jambo.

“Nisisitize uzalendo wa kusaidia wenzetu wasiojiweza kwa kuwa ni moja ya njia itakayosaidia wasiojiweza. Tutaendelea kusaidia jamii kwa kutembelea taasisi nyingine za afya, mwezi huu ni wa kumuenzi Mwalimu, tunatarajia kwenda katika hospitali nyingine kadhaa.”

Hospitali ya Mwananyamala
Pendaeli Massay ambaye ni Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala amesema “Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali nawashukuru Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa kututembelea na kutoa misaada mbalimbali.

“Misaada itawafikia walengwa, nikumbushe tu kuwa maadili kwa vijana yamepungua kwenye jamii na kumekuwa na vijana kadhaa wanaokimbia majukumu yao ikiwemo ya kuwatelekeza wazazi wao .”
 
Daaah Vijana wa sasa tobo kweli

sie tulikuwa tunaingia kwny mgogoro na ugomvi wa kifamilia hadi vikao kisa tu kuna mmoja anang'ang'ania kukaa na Mzee wetu Mgonjwa peke yake.

mpaka iliamriwa tuwe tuna rotate kwa kumuuguza kwa zamu miezi mitatu mitatu


Mzazi au ndugu yako wa damu unaenda kumtelekeza Hospitali na wewe unatulia kabisa na kuendelea na shughuli zako na usingizi unapata kabisaaa ?

Kweli binadamu bila ya Tabia ni Mamalia kabisa kama Mnyama mwingine
 
Ujumbe wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Dar es Salaam umetembelea Hospitali ya Mwananyamala Jijini hapo kuwajulia hali wagonjwa mbalimbali, leo Oktoba 14, 2023 ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere kilichotokea Oktoba 14, 1999.
he tu kuwa maadili kwa vijana yamepungua kwenye jamii na kumekuwa na vijana kadhaa wanaokimbia majukumu yao ikiwemo ya kuwatelekeza wazazi wao .”
pesa pasua kichwa sana dah
 
Si tunaambiwa kijana wa chini kabisa huko dasilama ana milioni TANO.!
muhindi kwenye kubeti kampiga kijana wa dar 3.1m tangu janury mpaka sasa,
tbl na serengeti, konyagi na k-vant wamempiga kijana huyuhuyu 2m kamili tangu january mpaka sasa...
hapo bado jeans za kisasa, raba, pafyumu na kamshahara na posho kidogo za deiwaka.....

nadhani kijana wa dar atakua na 7.9 mpaka 9.5m kwa mwaka, wachek vizuri....
 
Hizo changamoto za malezi zingetajwa.Kwa ufupi familia nyingi sana ni fukara/hawana fedha za kuweza kujihudumia katika masuala mengi ikiwemo magonjwa.Hivi,dunia hii mtu anakuwa na chuki au ugomvi kiasi gani na nduguze au wazazi hadi awatelekeze hospitali?
 
Back
Top Bottom