Vijana wanaamini wakivuta bangi wanapata Samaki wengi Ziwa Victoria

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
download.jpg
Imani ya matumizi ya bangi kwa wavuvi katika Ziwa Victoria imetajwa kuwa tishio kwa vijana na watoto.

Vijana hao huamini kuwa wanapotumia dawa ya kulevya aina ya bangi, hupata samaki wengi sambamba na ongezeko la nguvu za kufanya kazi nyakati za usiku.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kwamba matumizi ya bangi kwenye mialo ya wavuvi wa samaki unatokana na kutokuwepo kwa udhibiti kutoka mamlaka husika.

Aidha, upatikanaji wa dawa hizo umekuwa mwepesi zaidi kwa siku za karibuni kutokana na wauzaji na wasambazaji kubuni njia ya kupitisha ziwani, ikilinganishwa na awali walipokuwa wakipitisha kwa njia ya barabara.

Habari kutoka chanzo cha habari (jina linahifadhiwa) kimeieleza Nipashe kuwa dawa hizo zinazalishwa kwa wingi kwenye visiwa ndani ya Ziwa Victoria, huku watumiaji wengi wakiwa vijana na baadhi ya watoto wanaojihusisha na shughuli za uvuvi.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Udhibiti wa Rasilimali za Uvuvi ndani ya Ziwa Victoria (BMU) mwalo wa ufukwe wa Chato, Kamese Malima, anakiri kuwapo kwa matumizi ya bangi kwa baadhi ya wavuvi wanaotumia mwalo huo.

"Ni kweli wako wavuvi wanaotumia bangi kabla na baada ya kwenda kuvua samaki. Japo mimi si msemaji katika suala hilo, ninavyoona udhibiti wake unakuwa mgumu kutokana na baadhi ya viongozi kufumbia macho,"alisema Kamese.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chato, Makonzere Phinias, alithibitisha matumizi ya bangi kwa wavuvi walioko kwenye kijiji chake, huku akisema amekuwa akichukua hatua za kuwaelimisha kuachana na matumizi holela ya dawa hizo.

KAULI YA DCEA
Kwa mujibu wa Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA), Dk. Peter Mfisi, bangi haina uhusiano wowote na imani za kufanikiwa kupata samaki kwa wingi ndani ya maji.

"Bangi inavutwa mwilini wakati samaki wako ndani ya maji na mvutaji akimaliza kuweka nyavu zake huondoka na kurejea baadaye. Kungekuwa angalau na ukweli kiasi iwapo bangi ingelikuwa inatandazwa na nyavu halafu samaki wakapatikana lakini kinachofanyika ni kuvutwa na kubaki mwilini," anasema.

Dk. Mfisi anasema ni ukweli kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nao wamejiingiza kwenye matumizi ya bangi, huku akisema ni kichocheo kikubwa cha vijana kujidunga sindano wakiamini wanapunguza mawazo na baadhi yao kuwa na imani potofu za kuongeza akili za kufikiri.

Mbali na bangi, dawa zingine zinazotumika nchini ni pamoja na heroin, mirungi, cocaine, petroli pamoja na gundi.



Chanzo: Nipashe
 
Siko hapa kutetea uvutaji wa bangi, ila wavuta bangi wana utu na ubinadamu kushinda hata watu wa kidini.
Wavuta bangi ni watu wasio na unafiki
 
Back
Top Bottom