Vijana waliomaliza mafunzo JKT, kuandamana kwenda Ikulu kupeleka kilio cha ajira

Zhao vijana wana vichwa vigumu vya kuelewa, yeyote anayebisha apitie website ya jkt aone taratibu na masharti ya kujiunga na jkt, vile vile dhima ya kuanzishwa kwa jkt.
Katiko masharti yaliyoorodheshwa, mojawapo ni kuwa tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba wa kulitumikia jeshi la kujenga taifa(jkt), kama walikosa ajira wasiilaumu serikali kwa kujibagua kwa kuona Kuwa wao kwa kuwa wamepitia jkt basi wanastahili kusikilizwa, tena kwa kuonana na rais moja kwa moja utadhani hakuna vijana wengine wanaohitaji ajira serikalini!!!!au wanadhani kwamba toka jkt ianze ni wao tu ndio hawajaajiriwa?

nitatengeneza ajira 500,000 kila mwaka jk_
hizo ajira laki tano zipo wapi???

!!!
 
Mamia ya vijana waliomaliza mafunzo JKT miaka 2 iliyopita wameapa kuandama kwenda Ikulu kumuona rais ili wamfikishie kilio cha kupatiwa ajira kama walivyoahidiwa.

Vijana hao kutoka nchi nzima wamepanga kukutana Posta siku ya Jumatatu na wameweka bayana wako tayari kukabiliana na polisi.

Pia,vijana hao wamehoji mbona wenzao wa Zanzibar wameshaajiriwa?

CHANZO: Channel 10.

MY TAKE:

JK utakuwa mgeni wa nani?
mimi naona cha msingi ni bora wawagawe makundi wengine wafundishwe study za maisha kama ufundi magari uselemala na kazi nyingine lakini si kufundishwa matumizi ya silaha kisha awapewi ajira
 
nitatengeneza ajira 500,000 kila mwaka jk_
hizo ajira laki tano zipo wapi???

!!!

Hapo ndipo vijana wanapotakiwa kumuhoji jk kuhusu ahadi yake, au yawezekana ajira zimezalishwa ila idadi hiyo haikutosha kwa vijana kutokana wingi wao.
 
Ni rai yangu kwenu. Muwe wavumilivu. Mtapata ajira sehemu mbalimbali kulingana na ujuzi wenu. Kweli tena. Serikali ya CCM ni Serikali sikivu na tulivu. Tulieni na Serikali itatulia na kuwatatulia matatizo yenu ya ajira. Kuanzia sasa,mtapewa kipaumbele katika ajira mkiambatanisha vyeti vyenu vya JKT. Kweli tena.

Mkiandamana, mtapambana na polisi. Si mpambano wa kuumiss lakini unaofilisi na kuleta nuksi. Jengeni hoja za haja na mziwasilishe kwa wakuu wa Serikali. Kuandamana ni kuwindana. Tafadhalini msifanye hivyo. Hoja zenu zitapokelewa na kuzingatiwa. Mwaka huu hatutaki kumuudhi mtu kwakuwa tunataka kitu.

Maisha bora kwa kila mtanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kurudi Dar)
 
mmeanza kuogopa siyo? wamewaambia mafunzo waliyopata polisi na wao wameyapata. Kazi kwenu.
 
Sera za maandamano ni sera za CHADEMA. Hao vijana watakuwa ni wazamiaji tu ndani ya JKT
 
Ni rai yangu kwenu. Muwe wavumilivu. Mtapata ajira sehemu mbalimbali kulingana na ujuzi wenu. Kweli tena. Serikali ya CCM ni Serikali sikivu na tulivu. Tulieni na Serikali itatulia na kuwatatulia matatizo yenu ya ajira. Kuanzia sasa,mtapewa kipaumbele katika ajira mkiambatanisha vyeti vyenu vya JKT. Kweli tena.

Mkiandamana, mtapambana na polisi. Si mpambano wa kuumiss lakini unaofilisi na kuleta nuksi. Jengeni hoja za haja na mziwasilishe kwa wakuu wa Serikali. Kuandamana ni kuwindana. Tafadhalini msifanye hivyo. Hoja zenu zitapokelewa na kuzingatiwa. Mwaka huu hatutaki kumuudhi mtu kwakuwa tunataka kitu.

Maisha bora kwa kila mtanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kurudi Dar)

Ila ukumbuke hatutaki sijui ualimu, ajira za viwandani nk, tunataka na sisi huko BOT, TRA, Bandari, Imigration, Ikulu nk. Msifikiri ualimu unatulipa kivile. Tunataka huko ambako unaanza kazi ndani ya mwaka una gari zuri, nyumba nzuri na miradi kibao, huko kwenye ualimu wapeni hao walioko sasa kwenye hizo idara tulizozitaj ili na wao tuone uzalendo wao. Tunajua wengi walioko kwenye hayo maeneo hawajaingia kwa uwezo bali kwa vimemo.
 
Kuwaita hao makruta kuwa ni wanajeshi ni tusi kwa jeshi.Wamejifunza jeshi kitu gani hiyo hadi waitwe wanajeshi? Ni ile michakamichaka ambayo hata vibaka mitaani wanafanya? Au ni magwaride ambayo hata watoto chipukizi wanafanya wakati wa sherehe? Au wanajiita askari kwa kupewa bunduki na risasi tano kwenda uwanja wa shabaha kulenga bull ? mbona hilo hata wamiliki wa silaha binafsi wanafanya?

Mwanajeshi anakuwa mwanajeshi pale anapoajiriwa na jeshi na kupewa rigorous training ya kijeshi.Hao ni raia waliopitia JKT wakafunzwa kidogo wakarudi uraiani.

Hilo lalamiko lao la kusema serikali inaajiri kampuni binafsi ni upuuzi mtu.Kama wamejua hilo walitakiwa wafanye mambo mawili la kwanza badala ya kulalamika waanzishe kampuni yao binafsi ya ulinzi halafu wakaombe tenda za ulinzi sehemu mbali mbali pili Makampuni binafsi yanawahitaji wangeenda kuomba kazi huko badala ya kutwa kuzurura mabarabarani wakilalamika.

Hakuna aliyewaahidi kuwa wataajiriwa jeshini.Ajira za jeshi hazigawiwi hovyo kama kondomu.

Acha matusi wewe hata ksma baba yako yuko ikulu, hawa vijana wanamafai ya msingi, hawatakiwi kujibiwa kipumbavu kama unavyosema, kama si wanajeshi basi Jakaya kwani wao na serikali yao ndiyo walio anzisha hiyo misemo ya watu bila kupitia Jeshi mtu hawezi kudahiliwa chuo kikuu, mtu bila kuoutia Jeshi mtu hawezi kuajiliwa Magereza na jwingineko, kumbe wakijua wanafundisha mgambo, si wange waambia watu tangu mwanzo wakajua kuwa si jeshi ila ni aina flan ya mafunzo, suala la juanzisha makampuni ya ulinzi ni suala la serikali pia, kwa nini isiwape mitaji uone kama watashindwa kuendesha hayo makampuni ya ilinzi?, kuna oesa kibao TIB na NDC ika nadhani unawajua wanufaikaji wakubwa wa hizo pesa ni wale wenye pesa na kuwaacha wenyeshida na mambo kama haya ndiyo huwa yanazalisha waasi popote pale duniani, na inanikumbusha ile story ya French revolution pale watu walipoandamana kwa sababu hawana mikate(Chakula cha kipindi hicho) na Malkia kwa alivyolewa madaraka kama ulivyolewa wewe akaulize eti"kama hawana mikate si wale keki" na huo ndiyo ukikuwa mwanzo wa mwisho wa utawala wao na haya ndiyo yamekuwa majibu ya kila falling state duniani, sishangai.
 
Kwani mkataba wao ni kuajiriwa au wajitolee kujenga taifa kisha warudi nyumbani?

Wajenge taifa bila tofali..... Suburi tukione cha motot Oktoba... Si unaona sa ivi tushaanza kutungiwa ishu sijui magaidi mara majambazi... Soon itakuwa kweli!!! Hold on and wait!!!!!!
 
Kuwaita hao makruta kuwa ni wanajeshi ni tusi kwa jeshi.Wamejifunza jeshi kitu gani hiyo hadi waitwe wanajeshi? Ni ile michakamichaka ambayo hata vibaka mitaani wanafanya? Au ni magwaride ambayo hata watoto chipukizi lwanafanya wakati wa sherehe? Au wanajiita askari kwa kupewa bunduki na risasi tano kwenda uwanja wa shabaha kulenga bull ? mbona hilo hata wamiliki wa silaha binafsi wanafanya?

Mwanajeshi anakuwa mwanajeshi pale anapoajiriwa na jeshi na kupewa rigorous training ya kijeshi.Hao ni raia waliopitia JKT wakafunzwa kidogo wakarudi uraiani.

Hilo lalamiko lao la kusema serikali inaajiri kampuni binafsi ni upuuzi mtu.Kama wamejua hilo walitakiwa wafanye mambo mawili la kwanza badala ya kulalamika waanzishe kampuni yao binafsi ya ulinzi halafu wakaombe tenda za ulinzi sehemu mbali mbali pili Makampuni binafsi yanawahitaji wangeenda kuomba kazi huko badala ya kutwa kuzurura mabarabarani wakilalamika.

Hakuna aliyewaahidi kuwa wataajiriwa jeshini.Ajira za jeshi hazigawiwi hovyo kama kondomu.

Acha matusi wewe hata kama baba yako yuko ikulu, hawa vijana wanamadai ya msingi, hawatakiwi kujibiwa kipumbavu kama unavyosema, kama si wanajeshi basi Jakaya aliwadanganya kwani yeye na serikali yake ndio walio anzisha hiyo misemo ya watu bila kupitia Jeshi mtu hawezi kudahiliwa chuo kikuu, mtu bila kupitia Jeshi mtu hawezi kuajiliwa Magereza na kwingineko,

kumbe wakijua wanafundisha mgambo, si wange waambia watu tangu mwanzo wakajua kuwa si jeshi ila ni aina flan ya mafunzo,

Pia suala la kuanzisha makampuni ya ulinzi ni suala la serikali pia, kwa nini isiwape mitaji uone kama watashindwa kuendesha hayo makampuni ya ulinzi?,

kuna pesa kibao TIB na NDC ila nadhani unawajua wanufaikaji wakubwa wa hizo pesa ni wale wenye pesa na kuwaacha wenyeshida na mambo kama haya ndiyo huwa yanazalisha waasi popote pale duniani,

na inanikumbusha ile story ya French revolution pale watu walipoandamana kwa sababu hawana mikate(Chakula cha kipindi hicho) na Malkia kwa alivyolewa madaraka kama ulivyolewa wewe akaulize eti"kama hawana mikate si wale keki" yaani watu mikate hawana hiyo keki wanaipata wapi?, na huo ndiyo ukikuwa mwanzo wa mwisho wa utawala wao na haya ndiyo yamekuwa majibu ya kila falling government duniani, sishangai.
 
Wahitimu wa JKT waliomaliza mkataba wao bila kupewa ajira miaka miwili sasa wameoanga kuandamana kwenda Ikulu, wanadai wenzao wamepewa ajira muda sana katika vyombo vya ulinzi na usalama wao hakuna hata dalili na wametoa onyo kama polisi wanataka kupambana nao wawape siraha nao waoneshane nani mtata.

Chanzo: Chaneli Ten Habari

Hata kama walikuwa na sifa za kuajiriwa, kwa sasa wamepoteza sifa moja ya muhimu majeshini ambayo ni nidhamu. Hawafai kuwa askari.
 
Kama ni kweli kama channel ten walivyo tangazo kuwa, eti vijana wanaojiita Vijana waliopitia mafunzo ya Ki-jeshi kupitia JKT wanataka kuandamana kwenda Ikulu kudai ajira.

Ki-sheria za Ki-Jeshi ni kosa la jinai kwa askali kusaliti Jeshi kwa njia yeyote ile, iwe ya Ki-siasa ama ya Ki-maslahi na kufikia hali ya kuandamana.

Ajira zinafanyika kulinganga na mahitaji na wala si kwa mashinikizo. Ifahamike pia ajira huhitajika kuwepo na vigezo vinavyo jitoshereza ikiwa ni pamoja na Utii na Nidhamu. Kwa mazingira hayo hao wanaojiita JKT wa Maandamano wamepoteza sifa za kuajiliwa na jeshi, kama leo kwa miaka miwili wanafikilia kuandamana je wakipata ajira si watakuja kung'ang'ania kazini (Madarakani) au kufikilia kupindua Nchi na Uongozi kwa ujumla?.

Maandamano yapo huko kwenye siasa na ni bora waendelee kutumikia Siasa kuliko kuchanganya mambo. Wanatakiwa kuchunguzwa kwani JKT ni maalum kwa kufundisha Uzalendo na wala si kama wanavyodhani na kama hawakuiva nawashauri waombe maombi upya ili wapikwe vizuri.
 
Nimewasikia kuwa mafunzo waliyopata polisi nao wameyapata. Kama kupimia AK47 wote wanajua. Kesho wanaanza kukusanyana dara ila maandamano yatakuwa jumatatu ya wiki ijayo yaanin tarehe 23/2/2015.

Sasa watakula nini siku hizo zote?
 
Back
Top Bottom