Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,874
Tar 8 Desemba 2020.Aliyekuwa Rais wa JMT hayati John Pombe Joseph Magufuli alipokutana na vijana wa JKT hao 2400 ambao walipewa kazi ya kujenga Ikulu Chamwino-Dodoma.Akawaahidi kupewa ajira akisema watakapo maliza ujenzi wa Ikulu wapewe ajira wawe wanajeshi wasipelekwe sehemu nyingine.
Jana tar.17 Aprili 2021 ,CDF Mabeyo alitoa taarifa kwa Rais kufuta mkataba wa vijana wa JKT 854 miongoni mwa waliokuwa wanajenga Ikulu.Sababu alizozitaja kugoma kufanya kazi na kuandamana kwenda Ikulu kumuona Rais,akisema kugoma au kuandamana Jeshi ni uhaini.
Nakubaliana kwamba Mafunzo makubwa na ya mwanzo Jeshini ni utii.Utii wa amri kutoka kwa mamlaka ya kijeshi.
Bila kutaka kujua kwamba vijana hawa waliandama kweli au laa ,walihoji nini au laa ,waligoma kweli au laa ; sababu Jeshini sio sehemu ya kuhoji au kujitetea ikiwa mkubwa amesema.Nilienda Jeshini Msange JKT OP kikwete nilipata kushuhudia haya hata kwa miezi michache niliyokuwepo ,tuliwahi zuiwa kurudi nyumbani kufanya maombi ya vyuo na mikopo elimu ya juu nilihoji kwanini tunazuiwa ikiwa deadline inakaribia nilijibiwa na Captain Bakari "Hiyo ni Amri hupaswi kuhoji Nondo".
Nakiri utii wa amri ya mamlaka ya juu ni muhimu sana Jeshini .Ila tunawajibu sote kwa pamoja,viongozi wa dini na hata viongozi wa nchi kuwaombea msamaha vijana wenzetu hawa.Kwa kuamini wana nafasi kubwa ya kujirekebisha na kufanya vyema kwa maslahi ya taifa letu.
Vijana hawa wapo tangu 2017 ni OP Mererani na OP Makao ,wamefanya kazi kubwa kwa taifa letu .Ndio waliojenga Jengo la Nec Dodoma,waliojenga Hospital ya Uhuru,Msikiti mkubwa Chamwino,Kanisa kubwa Chamwino,Ukuta wa Ikulu km.34 ,Ndio waliojenga Ikulu Dodoma.
Vijana hawa kwa muda mrefu wamejituma na kuvumilia mengi,ikiwa kuna kosa lolote la kimaadili walilofanya nakiri kusema haikuwa dhamira yao bali katika hali ya kuuliza ahadi yao ya kuajiriwa baada ya ujenzi wa Ikulu,muda mrefu maisha yao yalikuwa ya matumaini ya kesho yao katika kulitumikia taifa.
Mimi nina amini kwamba vijana hawa wakisamehewa na kupewa fursa tena,watajirekebisha na kufanya mengi zaidi kuliko kuvunja mkataba na kuwarejesha nyumbani.Kwa pamoja tusichoke kuwaombea msamaha wasamehewe ili wapate fursa ya kujifunza zaidi.
Abdul Nondo.