Vijana waandaliwe kuvamia mataifa mengine. Bado muda tunao.

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,597
Reaction score
91,924
Hamjambo wote!

Hili nitaendelea kulisema kila nikipata nafasi. Kwa sababu najua kile ninachokisema. Nakijua kwa sababu ndio usalama wa nchi yetu na future yetu.

Niliitambulisha sera ya uvamizi miaka kadhaa iliyopita. Nikiwasihi viongozi na wale wenye mpango wa kuwa viongozi waitafakari, kisha wachukue hatua kadiri iwezekanavyo.

Sisi Watibeli tunaona Mbele kwa sababu tulishaishi wakati mnaouita ujao. Tunajua nini kipo mbele.

Kanuni ninayoipendelea ni kushambulia zaidi kuliko kupark basi. Kusubiri kuanzwa. Hiyo wengi huitafsiri kama ukorofi, uchokozi, ubabe, na kutokutenda haki.

Iko hivi, hii Dunia ni kama mzazi. Unachagua upande. Kuwa Simba ule wanyama wengine au uwe Swala uliwe.

Unachagua uendeshe au uendeshwe.
Unachagua uvamie au uvamiwe.
Hiyo ndio HAKI ya DUNIA.
Haki ya Asili. Haki ya viumbe hai.

Hii ni tofauti na haki za kifalsafa na kisaikolojia.

Kiasili, ni haki ya Simba kumla Swala. Hiyo ni HAKI.
Lakini kisaikolojia na kifalsafa inaweza isiwe Haki.

Ukitaka ulinde Haki za ndugu zako lazima uminye haki za watu wasio ndugu zako. Hiyo ni nature.
Kisaikolojia haipo hivyo.

Ili taifa letu liendelee lazima kuna taifa fulani litapaswa limenyeke, likandamizwe.

Na kama hakuna taifa linalomenyeka kwaajili yetu. Ni wazi sisi tutakuwa tunamenyeka kwaajili ya taifa jingine. Hili nimekuwa nikilisema.

Njia ya usalama ni kuondoa usalama upande mwingine.
Njia ya usafi ni kutupa taka sehemu nyingine.
Njia ya kuondoa ushetani ni kupeleka ushetani mahali pengine.

Huwezi kuzuia ubaya kwa kupambana nao bila kutafuta pakuupeleka. Hizo ni falsafa za Kitibeli.

Ukitaka usigombane na mkeo au mumeo ili familia yako uwe na nguvu. Hauna budi kupeleka magomvi familia zingine. Hii inakuwa kama exist doors.

Ili kupunguza migogoro ya ndani, lazima uanzishe migogoro ya nje. Kimedani na kiutawala au kimahusiano ndivyo mambo yalivyo.
Umoja wenu hauji tuu kwa sababu mnatendeana Haki na Wema. Nope! Umoja na nguvu zenu utatokana pia na uwezo wenu wa kumtengeneza mhusika wa kumlaumu, kumpa matatizo na kumsingizia. Kumzushia migogoro. Mtibeli anakuchanganya?

Uvamizi ni moja ya mbinu ya kitibeli ambayo inadumisha falme kwa karne na karne.

Ni lazima tuandae vijana wakuvamia. Vijana watundu, jasiri, wenye akili zilizoshindikana.

Ukishindwa kuvamia. Matokeo yake mtaanza kusumbuana wenyewe kwa wenyewe. Kusumbuana ndugu kwa ndugu. Kushikana uchawi.

Katika vita. Usalama wa taifa upo kwa kuwa na adui asiye wa ndani ambaye mnamtengeneza ninyi wenyewe kama taifa.

Unapokuwa huna adui. Basi ujue ndani yako adui yupo. Umefuatwa nyumbani kwako. Na utapigwa nyumbani kwako. Au adui atatoka ndani yako.

Kitibeli, kanuni ya uvamizi inakupa nafasi ya kumfuata adui kabla ya vita kupangwa. Unamfuata adui bila yeye kujua. Wakati wa amani. Akiwa comfortable. Akijua kila kitu kipo sawa. Kumbe adui yupo.

Ni kama magonjwa makubwa. Yanapoingia mwilini mwako. Huwezi kuyahisi. Unajihisi uko salama. Kumbe yaliingia siku nyingi sana. Siku yakianza kukushenyeta ukienda hospitality unaambiwa yaliingia miaka 10 iliyopita. Unabaki unabung'aa. Uvamizi!

Mimi nimemaliza. Leo nilisali Mwenge SDA. Barikiweni.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Serikali ibadili hii sera. Vinginevyo sio muda tutachapana humu ndani.
Nchi nyingine zinawezesha vijana wao kwenda Nchi nyingine hasa za Ulaya kwaajili ya utafutaji

Wanajua baada ya muda wataanza kupokea fedha za kigeni

Sisi huku imekuwa tofauti, watawala wanahisi jamaa wakienda nje ya Nchi itawashinda kuwatawala
 
Tanzania haina uraia pacha, wakiona fursa zinapatikana kwa rai wa mataifa hayo wakazifuatiliwa watakosa uraia wa Tanzania, Wakenya, waganda, na wanyarwanda wanazifukuzia sana fursa hizo bila kuwa na hofu ya kupoteza uraia wa nchi zao.

Tanzania ina sera za uraia za kizamani sana.
 
Hawahawa vijana useless kina adriz de mbusii?
 
Nchi nyingine zinawezesha vijana wao kwenda Nchi nyingine hasa za Ulaya kwaajili ya utafutaji

Wanajua baada ya muda wataanza kupokea fedha za kigeni

Sisi huku imekuwa tofauti, watawala wanahisi jamaa wakienda nje ya Nchi itawashinda kuwatawala

Wanakosea sana.

Kuwaachia wengine waende kupambana huko na huko huku mkiwawekea mifumo na miundombinu ya kiusalama na kusaidia nchi ni mbinu ambayo itanufaisha nchi na usalama wa wakati ujao.
 
Ni kweli, watawala inawapasa waanze kufikiri kwa manufaa ya Nchi nzima badala ya kuwaza matumbo yao pekee

Hata ujasusi wa Kiuchumi hawafanyi tena, ndiyo maana Nchi inabaki hapa ilipo kwa miaka mingi
 
Tanzania haina uraia pacha, wakiona fursa zinapatikana kwa rai wa mataifa hayo wakazifuatiliwa watakosa uraia wa Tanzania, Wakenya, waganda, na wanyarwanda wanazifukuzia sana fursa hizo bila kuwa na hofu ya kupoteza uraia wa nchi zao.

Tanzania ina sera za uraia za kizamani sana.

Serikali ibadili huo mtazamo.
Inatengeneza watu waoga, ambao wakivamiwa hawana uwezo wa kujitetea.
 
Ni kweli, watawala inawapasa waanze kufikiri kwa manufaa ya Nchi nzima badala ya kuwaza matumbo yao pekee

Hata ujasusi wa Kiuchumi hawafanyi tena, ndiyo maana Nchi inabaki hapa ilipo kwa miaka mingi

Ni kweli. Fursa ziko nyingi Sana. Lakini ili ndani kuachia lazima utoboe tundu la nje.
 
Vijana wa nchi hii wanawaza uzinzi, ulevi, betting, na nyongeza kuu kupinga USHOGA, hapo ndipo wanaweza sana, na sio hiki unachokisema wewe hapa, HAWAWEZII.

Kwanza kuwa specific, wazamie nchi gani? Au bara lipi? Usitaje Europe na America, huko hapana, maana keyboard warriors wa hapa wao wako against na 🌈, sasa huko 🌈ni maskani makuu.

Najua watakuja kuhemkwa hapa, nasemaje, pandeni muwezavyo, mkimaliza mseme niwashushe.

😂😂😂
 
Kama naelewa kitu lakini pia tujue Kuna athari hasi juu ya hili swala
 
Niliwahi kusema Tanzania ilifanya kosa kubwa sana kuiruhusu Rwanda na Uganda kuimarika lakini pia inafanya makosa yaleyale kupambania Congo DRC kuimarika na sasa Burundi imeshamaliza tofauti za ndani inajiimarisha. Very bad in the near future.
 
Back
Top Bottom