Vijana wa zamani 1950-2000 kulinganisha na 2000-2025 katika Jamii

Vijana wa zamani 1950-2000 kulinganisha na 2000-2025 katika Jamii

Mimi naona umri wa kuwa shule watu wanakuwa wadogo sana,. Hebu fikiria mtu yupo chuo na miaka 19 au 20 mwanafunzi wa mwaka wa kwanza..
Hajui chochote kuhusu maisha wala yale yanayoendelea kwenye nchi anaona hayamuhusu.
Kipindi kile utakutamtu ana miaka 30 anaanza chuo akili na fikra zimekomaa kabisa.
Lakini sasa ukienda chuo na imri huo watakuuliza from services eti.
Tusiwalaumu sababu yanayoendelea wanaona hayawahusu kutokana na umri wao wanaona haya ya mama au baba nyumbani.
britanicca
 
Dogo hapo kwenye mabano inatakiwa iwe (to) the nation siyo (for) the nation. AI yako inakudanganya hahaha 😂😂😂🤣 maarassmbusii
Oya Kayngay hiyo nimeweka kwa makusudi ili kukuProve wrong kwamba sio Al kwa maana ingekuwa AI au natumia transalator isingefanya mistake ambayo common kama hiyo.

Halafu mbona hata for sijakosea sana kimtaani inatumika tu ?
 
Huwa najiuliza hawa watoto wa 2000s si wamezaliwa na wazazi wa 1970s-1980s ambao walinyooka kimaadili! Wanalaumiwa watoto badala ya wazazi wao!

Siku tukiacha kutupia lawama watu wengine hata kama makosa tulifanya sisi wenyewe tutakuwa tumejikwamua sana!

Namaanisha ukifanya kosa ama uzembe basi wajibika kwa huo uzembe na makosa yako mwenyewe na usitafute kisingizio chochote!

Mfano halisi ni huu: Wazazi wa 1970s-1980s ambao waliwazaa watoto wa 2000s wengi wao walishindwa jukumu mama la kimalezi kwa watoto wao.Baada ya kushindwa wanawatupia lawama watoto wao wenyewe!
"People blame this generation but they forget who raised it up ".
 
Hawa wataingia tu barabarani siku wakijua adui wa vijana ni vijana wenyewe.

Angalia police vijana wanavyoua vijana wenzao na kuwateka

Nipo ndani ya jeshi kwa muda
Mrefu Sana intake za Magufuli na Samia ndani ya jeshi ndio problem hawana kabisa identity ya uzalendo hata punje wao ni pesa pesa mbele

JKT pia na Moshi Kuna shida kwenye kuandaa Hawa watu

Zao la kukosa elimu bora
Nam
 
Angalia tangu huko mashuleni, sijui wanakula nini, ila watoto wamekuwa kama waoga kupindukia.

Watoto wa kiume, shule ya boys wanavaa shamba dress eti, wamejengewa na uzio kabisa.
😂😂😂😂😂
 
Miaka hiyo elimu haikuwa imechakachuliwa na hata watoto wa viongozi walisoma shule hizo hizo walizosoma watu wengine.

Mfano watoto wa Nyerere walisoma Korogwe girls, Tabora school n.k

Mwinyi huyo wa Zanzibar alisomba Tambaza na wengineo wengi tu walisoma shule hizo.

Walipoona mwanya pekee wa kudhoofisha watanzania ni kupitia elimu ndio walipoanza kuvuruga.

Kuna kiongozi mmoja alitoa mfano kuwa ukitaka kuangusha taifa lolote na kuwatawala watu muda mrefu tumia kalamu[elimu] ni zaidi ya mtutu.

Leo hii mtoto wa Mwigulu kasoma Feza schools, akisogea chuo utashangaa karuka UK au USA na kaandaliwa kuja kuwa kiongozi unafikiri anajua matatizo ya watanzania wengi wa kawaida atakaotakiwa kuwaongoza zaidi ya kuzidi kupalilia ulaji wa generation yao?
 
Back
Top Bottom