Vijana wa Heche ni wakorofi, waonywe

Vijana wa Heche ni wakorofi, waonywe

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,864
Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa familia ya Suguta ambayo imepata msiba wa kijana wao. Nikiri pia kuifahamu familia ya Heche kwa sababu tunatoka maeneo ya karibu nyumbani ni kijiji cha Nyabisaga na ukoo wa Heche unaishi vijii vya Nyabitocho, Kitagasembe, Sirari, Tarime na wengine wilaya serengeti.

Nimeona bandiko la mdau mmoja akihoji "Polisi wana nini na vijana wa Heche" ni kweli pia kwamba vijana wa Heche wamekuwa wakikumbana na masahibu mbalimbali na jeshi la polisi lakini mara nyingi inatokana na ukorofi wao, vijana hawa wamekuwa wanakuwa wakorofi, wakaidi na mara nyingi wamekuwa wakiizuia jeshi la polisi kufanya shughuli zao inafika kipindi vijana hawa wanawazaba vibao askari wa usalama barabarani vibao.
Kuna matukio ya ukorofi wao wamekuwa wanafanya hata kwa watu wa kawaida, mfano ukihitilafiana na mmoja wanaitana wanakuja ukoo mzima na kushambulia.
Mambo haya mhe. Heche anayajua na alishawahi kukiri kipindi anaomba kura na akasema atawakataza.
Wito wangu kwa mbunge Heche kaa chini zungumza na familia yenu zile zama za utemi zilishapita, waambie wajifunze kuheshimu askari wetu wa jeshi la polisi.
 
Watu wa Tarime na Sirari, wengi wao kukiwa na mtu ndani ya familia awe na pesa au awe na cheo au awe na rafiki mwenye cheo serikalini huwa na ukorofi wa kipumbavu hujawahi ona. Kwa wanaokumbuka mwaka 2004 kulikuwa na askari mkubwa kwa cheo hapo Tarime alikuwa ni mjaluo yule bwana, watoto wake hakuna ambalo ungemwambia lililosawa akalitii, rejea matukio aliyokuwq akiyafanya Zakaria na kundi lake la vijana.
 
Ni kweli kabisa mkuu
 
Hapa unamaanisha nini kwamba walichokifanya polisi kwa Suguta kilikua sahihi kwa sababu alikua mkorofi?
 
Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa familia ya Suguta ambayo imepata msiba wa kijana wao. Nikiri pia kuifahamu familia ya Heche kwa sababu tunatoka maeneo ya karibu nyumbani ni kijiji cha Nyabisaga na ukoo wa Heche unaishi vijii vya Nyabitocho, Kitagasembe, Sirari, Tarime na wengine wilaya serengeti.

Nimeona bandiko la mdau mmoja akihoji "Polisi wana nini na vijana wa Heche" ni kweli pia kwamba vijana wa Heche wamekuwa wakikumbana na masahibu mbalimbali na jeshi la polisi lakini mara nyingi inatokana na ukorofi wao, vijana hawa wamekuwa wanakuwa wakorofi, wakaidi na mara nyingi wamekuwa wakiizuia jeshi la polisi kufanya shughuli zao inafika kipindi vijana hawa wanawazaba vibao askari wa usalama barabarani vibao.
Kuna matukio ya ukorofi wao wamekuwa wanafanya hata kwa watu wa kawaida, mfano ukihitilafiana na mmoja wanaitana wanakuja ukoo mzima na kushambulia.
Mambo haya mhe. Heche anayajua na alishawahi kukiri kipindi anaomba kura na akasema atawakataza.
Wito wangu kwa mbunge Heche kaa chini zungumza na familia yenu zile zama za utemi zilishapita, waambie wajifunze kuheshimu askari wetu wa jeshi la polisi.
Wrong timing for this advice mkuu
 
Siungi mkono mauaji yale, lakini ukiuliza watu wengi marehemu ndio alikuwa mkorofi. Na sijui ni kwanini askari yule alishindwa kujizuia mpaka akafanya mauaji yale.
Umeshapigwa pingu mkononi unafanyaje ukorofi?
Kwahiyo majibu ya ukorofi ni kisu cha ngariba?
 
Ndiyo ujinga wao wakishaua wanaanza kutafuta wa kumtupia lawama ili kuhalalisha kuua.
Crazy part ni when that shit works, utakuta mtu kashupaza shingo akikwambia sasa mliandamana mlitaka nini? Vijana ni wakorofi mlitaka nini?
 
Kwa Hiyo ukoo wa heche ni kama careone family's, wakurya jambo dogo mtu kashatoa pañga na halirudi
 
Back
Top Bottom