Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Huku mitaa ya manzese ukiwaona vijana wamebeba mabegi makubwa kama watalii...ujue wapo kazini wanahifadhi vitu wanavyokwapua...yaani ukifua nguo zako na ukasema uende ndani kidogo....imekula kwako kwani tayari vijana wameshaanua tena zikiwa mbichi.......au wale wakina mama wenye tabia za kuosha vyombo nje nao pia mara nyingi huwa ni wahanga wa hao vijana wenye mabegi mgongoni kutwa nzima kama kobe.......kuna siku halmanusura tumuue mmoja baada kutaka kuiba nguo nyumba ya pili....ndio nikajua maana ya yale mabegi kuwa ni zaidi ya urembo.......
Na pia kuna mabinti nao wanaobeba mabegi makubwa utaweza kudhani ni wanachuo kumbe kazi zao ni kuiba nguo huko mitumbani na madukani.....wakirudi nyumbani wanauza.......

Vile vile hao vijana wanaobeba mabegi kama ukipanda nao gari moja uwe zaidi ya makini kwani wengine ni wezi wa mifukoni na hayo mabegi hutumika kuhifadhi hivyo vitu..........
7049dc4a928ce81283a8927af38c8f52.jpg
 
Jamani si amesema hao wabeba mabegi wanafiki ofisini na kuyaweka ukutani bila kuchukua kitu chochote toka kwenye hizo begi!!? Sasa habari za laptop inakuwaje tena au wanazitumiaje ndani!
Sasa yeye amemuona mmoja au ameona wangapi? ina maana muda mwingi mtoa post kazi yake ni kuchunguza wabeba mabegi wanachokifanya: ama kweli huko Dasilamu kuna mambo!
 
laptop, external hard disk, charger, documents, leso,ka tshirt kidogo ka emergency,earphone,atm cards, ids ... vitu vingi aisee.
sasa sijui hivi vyote uvibebe kwa bahasha au fuko la lambo, mzee tuko kijiditali we baki analogia
Kweli hii ni digital mkuu.
 
Hahahaha nimecheka sana wee hujui baadhi yao wanaweka lipshine wanja simu kubwa feki nk hahaha
 
Mi bachelor napita ata Sokoni naweka matunda kwenye mfuko kisha ndani ya beg mtu asione
 
Mifuko ya Rambo imepigwa marufuku sasa ww unataka tubebe nn?
 
Mimi kwenye bag yangu huwa nabeba laptop na chaji yake, chaji ya simu, mswaki na dawa, mafuta, body spray na perfume, pasport, kuna document kibao, yaani nisipotoka na bag nahisi kama nimepungukiwa kitu fulani siku hiyo,
Hapa naandika niko na bag yangu Pembeni
Wee jamaa sasa unatembea na Ofisi kabisa!!
 
Is for emergency purpose. Hujui kuwa tupo kwenye mchakato wa kupiga vita matumizi ya mifuko ya lambo na vifungashio vyake?
Itafikia mahala ukienda kwa marikiti kununua tunguja, kabeji na vitunguu unatia kwa begi yako.
Hahahahaahahahah
 
Ukiona huelewi jua haikuhusu, ila ngoja nikujibu huku kwetu begi mgongon Wanabebea cha Arusha either Wa kuuza Au kutumia
 
Kuna jamaa mmoja anatembea na bag lake mgongoni 24/7 ndani utakuta kuna nyanya, mafuta ya kupikia, mchele nusu, vitunguu, chumvi suruali, tshert na bukta hvi ni vichache tu! halafu jamaa sijawah kumuuliza anafanya kazi gani ngoja leo nikimuona niweke picha yake hapa!
 
1. laptops
2 ipads
3. lunchboxes
4. diaries
5. lesson
6. Biblia
7. connecting cables
8. any other electronic gadgets ans stuffs
9. wallts full of Cash
10. cheque books
 
Back
Top Bottom