DON YRN
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 475
- 999
Nipo hapa kwa kitanda usiku huu wa manane nikiwa na msongamano wa mawazo na kutafakari mambo mbalimbali kuhusu haya maisha hasa kwa sisi vijana ambao tunajitafuta na bado hatujajipata.
Haya maisha ya utafutaji yamejaa vitu vigumu na vizito ambavyo siyo rahisi mtu kukuelezea ni namna gani aliweza kufanikiwa katika maisha na kufikia level aliyopo.
Tukubali ama tukatae ila ukweli ni kwamba kila mmoja wetu katika maisha ya utafutaji ana LIGHT SIDE na DARK SIDE yake lakini upande unaomtambulisha mtu hadi akawa midomoni mwa walimwengu kwa kile anachokifanya ni DARK SIDE ambayo inakuwa ni SIRI ya muhusika na tusije danganyana. LIGHT SIDE huwa inatumika kama mfuniko na ngozi ya kuficha nyama ya ndani ambayo ni DARK SIDE.
Muda mwingine unaweza kuamini hiki kumbe sicho na kile usichokiamini ndo ndicho, kinachopaswa kuzingatiwa ni kujua na kuelewa namna ya kutofautisha kipi ni sawa na kipi siyo sawa.
Ilikuwa mwaka 2019 nilijichangachanga nikapata kama 2.5 Milion nikafungua biashara ya duka la chakula(duka la mangi) maeneo fulani hapa jijini Dar es Slaam.
Baada ya kufanya biashara kwa takribani miezi 2, nilianza kutotamani kwenda kufungua hii biashara yangu, yaani ilikuwa kila nikitaka kwenda kazini kunakuwa na kaubaridi jumlisha uoga, miguu kuwaka moto nikiwa maeneo ya biashara, kuchoka na kuumwa ghafla ambao hadi leo hii sijawahi kuelewa shida ilikuwa nini, japo mimi huwa ni muoga na kutoamini sana mambo ya nguvu za giza.
Motokeo yake niliamua kufunga ile biashara kwa kuuza vitu kwa bei ya jumla kwa hasara kubwa mno na baada ya hapo niliamua kuachana na masuala ya biashara nikajikita kwenye mishe zangu zingine.
Mwaka jana baada ya zoezi la Sensa (2022), wazo la biashara lilinijia nikajichangachanga nikafungua biashara ya kuuza mabegi ya mtumba hasa haya ya watoto wa shule na watu wazima hasa wale wa kwenda site i.e kubebea vitu vya mafundi.
Niliamua liwalo na liwe hata iweje ile hali ya kukatia tamaa biashara yangu kama ingenijia, ningekaza na nisingejaribu kukata tamaa.
Nilipambana na hiyo biashara wee japokuwa kuna muda ile hali ilikuwa inanijia lakini nilijikaza kiume. Kuna kipindi mwanzoni mwanzoni kama February mwaka huu (2023) biashara ikawa ngumu kiasi hivyo nikaona nihamishe location ya biashara.
Nilihamia sehemu yenye mzunguko wa watu na biashara ilichangamka sana hadi nikawa nauza hadi 20 bags per day.
Baada ya muda kama miezi 3 toka nihamie hii location mpya, biashara ilianza kuwa ngumu ghafla kwangu, ikawa hata kwa siku naweza uza 1 bag au nisiuze kabisa na mzigo upo wa kutosha. Uvumilivu ulinishinda nikamshirikisha mwanangu mmoja hivi akanielekeza kwa mtaalamu (Sangoma) mmoja huko Mbagala Chamazi ndani ndani.
Ni kweli baada ya mtaalamu mambo yakawa mwororo kama kwa muda wa mwezi mmoja hivi na ghafla mambo yakawa magumu tena balaa. Niliona hata kama uvumilivu wa kibiashara si kwa mtindo huu, yaani majumuisho ya mauzo kwa mwezi ni 10 bags. Niliamua kufunga hii biashara maana sikutaka kuwa mtumwa tena wa kwenda kwa mtaalamu.
Enyi motivation speakers hasa wa masuala ya biashara, mkiwa mnawaponda watu wanaofunga biashara kwa falsafa zenu eti kukosa mitaji, ubunifu na usimamizi mbaya, basi muwe mnakumbuka kuwa kuna masuala ya nguvu za giza na mnapaswa kuyajumlisha kama mojawapo ya changamoto zinazosababisha biashara kufungwa.
Wako katika ujenzi wa Taifa,
DON YRN.