Vijana tunapitia wakati mgumu sana kwenye utafutaji. Chukua hii, itakufikirisha zaidi

DON YRN

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
474
999
Nipo hapa kwa kitanda usiku huu wa manane nikiwa na msongamano wa mawazo na kutafakari mambo mbalimbali kuhusu haya maisha hasa kwa sisi vijana ambao tunajitafuta na bado hatujajipata.

Haya maisha ya utafutaji yamejaa vitu vigumu na vizito ambavyo siyo rahisi mtu kukuelezea ni namna gani aliweza kufanikiwa katika maisha na kufikia level aliyopo.

Tukubali ama tukatae ila ukweli ni kwamba kila mmoja wetu katika maisha ya utafutaji ana LIGHT SIDE na DARK SIDE yake lakini upande unaomtambulisha mtu hadi akawa midomoni mwa walimwengu kwa kile anachokifanya ni DARK SIDE ambayo inakuwa ni SIRI ya muhusika na tusije danganyana. LIGHT SIDE huwa inatumika kama mfuniko na ngozi ya kuficha nyama ya ndani ambayo ni DARK SIDE.

Muda mwingine unaweza kuamini hiki kumbe sicho na kile usichokiamini ndo ndicho, kinachopaswa kuzingatiwa ni kujua na kuelewa namna ya kutofautisha kipi ni sawa na kipi siyo sawa.

Ilikuwa mwaka 2019 nilijichangachanga nikapata kama 2.5 Milion nikafungua biashara ya duka la chakula(duka la mangi) maeneo fulani hapa jijini Dar es Slaam.

Baada ya kufanya biashara kwa takribani miezi 2, nilianza kutotamani kwenda kufungua hii biashara yangu, yaani ilikuwa kila nikitaka kwenda kazini kunakuwa na kaubaridi jumlisha uoga, miguu kuwaka moto nikiwa maeneo ya biashara, kuchoka na kuumwa ghafla ambao hadi leo hii sijawahi kuelewa shida ilikuwa nini, japo mimi huwa ni muoga na kutoamini sana mambo ya nguvu za giza.

Motokeo yake niliamua kufunga ile biashara kwa kuuza vitu kwa bei ya jumla kwa hasara kubwa mno na baada ya hapo niliamua kuachana na masuala ya biashara nikajikita kwenye mishe zangu zingine.

Mwaka jana baada ya zoezi la Sensa (2022), wazo la biashara lilinijia nikajichangachanga nikafungua biashara ya kuuza mabegi ya mtumba hasa haya ya watoto wa shule na watu wazima hasa wale wa kwenda site i.e kubebea vitu vya mafundi.

Niliamua liwalo na liwe hata iweje ile hali ya kukatia tamaa biashara yangu kama ingenijia, ningekaza na nisingejaribu kukata tamaa.

Nilipambana na hiyo biashara wee japokuwa kuna muda ile hali ilikuwa inanijia lakini nilijikaza kiume. Kuna kipindi mwanzoni mwanzoni kama February mwaka huu (2023) biashara ikawa ngumu kiasi hivyo nikaona nihamishe location ya biashara.

Nilihamia sehemu yenye mzunguko wa watu na biashara ilichangamka sana hadi nikawa nauza hadi 20 bags per day.

Baada ya muda kama miezi 3 toka nihamie hii location mpya, biashara ilianza kuwa ngumu ghafla kwangu, ikawa hata kwa siku naweza uza 1 bag au nisiuze kabisa na mzigo upo wa kutosha. Uvumilivu ulinishinda nikamshirikisha mwanangu mmoja hivi akanielekeza kwa mtaalamu (Sangoma) mmoja huko Mbagala Chamazi ndani ndani.

Ni kweli baada ya mtaalamu mambo yakawa mwororo kama kwa muda wa mwezi mmoja hivi na ghafla mambo yakawa magumu tena balaa. Niliona hata kama uvumilivu wa kibiashara si kwa mtindo huu, yaani majumuisho ya mauzo kwa mwezi ni 10 bags. Niliamua kufunga hii biashara maana sikutaka kuwa mtumwa tena wa kwenda kwa mtaalamu.

Enyi motivation speakers hasa wa masuala ya biashara, mkiwa mnawaponda watu wanaofunga biashara kwa falsafa zenu eti kukosa mitaji, ubunifu na usimamizi mbaya, basi muwe mnakumbuka kuwa kuna masuala ya nguvu za giza na mnapaswa kuyajumlisha kama mojawapo ya changamoto zinazosababisha biashara kufungwa.

Wako katika ujenzi wa Taifa,

DON YRN.
 
Daaah umeandika kwa hisia sana.

Ila kaa ukijua biashara yoyote kama ulivyo fanya hiyo ya mabag huwa kuuza 10 bags per month ni kawaida kwani huwa ni ya msimu so learn how to stay low key na siku ukija msimu wa high peak komaaa kufa kupona uuze bags kama kichaaa maana pesa huwa zinamwagika....

Huwezi kuuza kila siku hata uwe location nzuri...
 
Nilipambana na hiyo biashara wee japokuwa kuna muda ile hali ilikuwa inanijia lakini nilijikaza kiume.
Mwili wako hautaki ufanye hio kazi/biashara hio ni moja mbili wapo watu wanakuona kua wewe hufananii na hio biashara na tatu wapo watu wanaona wewe haustahiri kufanya hio biashara

Umesema ulienda kwa Sangoma yaan maana yake ulienda kujiandikisha kwenye kitabu cha wachawi nikama unavyoenda hospital pale unaacha data zako zote zinahifadhiwa kuanzia jina umri na kila kitu means ulitakiwa uanze kuishi kichawi na uchawi unataka ufanyiwe recharge kila baada ya muda ndio maana ukaona baada ya mwezi Mambo yakakata ilibidi uende ukarecharge au umwambie mtaalamu wako akuelekeze jinsi ya kurecharge,

Hujaelewa? Uchawi wa Sangoma ni nguvu ya Giza mfano ni km ilivyo simu yako ya Android/iOS hio unayoitumia sasa ili simu iendelee kutumika unahitaji uichaji kila chaji inapoisha la sivyo simu itazima mazima yaan na Uchawi upo hivyo hivyo kila baada ya mda inakubidi urecharge ndio mafanikio yanaongezeka sasa wewe charge ilipoisha ukaacha kuchaji unafikiri hio nguvu ya Giza itatoka wapi?

Mambo ya Giza sio Mambo ya motivation yanahitaji ujuzi na uvumilivu maana kuna kipindi hilo Giza pia linaweza likakutafuta likatoweka na wewe usionekane tena duniani
 
Unamtisha mshkaji 🤣
 
Unamtisha mshkaji 🤣
Sio kwamba namtisha ndio ilivyo hivyo uliza popote hakuna anaeuza duka ambae halogi wengi wanafanya Uchawi wanazidiana tu maana Mambo ya Giza yapo kila sehemu sasa alichoshindwa mtoa mada ni kuchagua kua mchawi ili afanikiwe

Means ukichagua upande chagua upande wapo wachawi wa biashara na ni watu wa dini balaa Ila ni wachawi kiboko ukiambiwa huwezi amini Ila kuna mda Uchawi unaweza ukakutafuta Giza nalo linataka shibe ukikosa cha kulilisha Giza litaondoka na wewe
 
Kingine cha kuongezea Ila sio cha umuhimu wanasema njia namba moja ya kufanikiwa kibiashara ingia ukiwa Mbumbumbu yaan mjingamjinga apechealolo namaanisha km ulitoka na Masters yako huko ya BA weka pembeni fanya km hujawahi kumaliza hata darasa la Pili hio inaitwa kujitoa muhanga unabeba hio risk aidha upate au upoteze kitafahamika huko mbele ya Safari

Ntakupa kisa hii sio motivation speaking ni kweli na imetokea namaanisha ni kisa cha kweli

Unaambiwa kuna jamaa alianza biashara kwa Pesa ya mkopo kausha damu ili kufanya marejesho round ya kwanza biashara ikakubari akafanya marejesho akakopa tena round ya Pili biashara ikajibu akarudisha rejesho akakopa tena sasa round ya 3 akachezea za mbavu Biashara ikagoma unaambiwa watu wa mkopo walizoa kila kitu akabakia mweupe peee yaan walimuacha yeye na nguo zake na viatu vyake walizoa hadi shelves zile za dukani na meza na kila kitu

Akakopeshwa mkopo na rafiki yake mmoja ambae ni mtu wa Mambo ya Ndagu biashara ikarudi km ilivyokua mwanzo akaanza kuneemeka Ila usisahau kitu chochote cha giza ipo siku Giza litadai rejesho lazima upeleke chochote Gizani

Km ulipata Pesa kwa Giza ukanunua Gari usisahau ipo siku Giza litakufuata ukiwa kwenye Gari na kukudai rejesho usipotoa litaondoka na wewe au litaondoka na Gari

Km ulipata Pesa kwa Giza ukanunua nyumba ipo siku Giza litakutafuta ukiwa kwenye nyumba na kukudai rejesho usipotoa litaondoka na wewe au litaondoka na nyumba

Km ulipata Pesa kwa Giza ukaanzisha biashara ipo siku Giza litakufuata ukiwa kwenye biashara yako na kukudai rejesho usipotoa litaondoka na wewe au litaondoka na biashara

Km ulipata Pesa kwa Giza ukatafuta cheo ukapata cheo kwa Pesa zako za Giza basi jua ipo siku Giza litakufuata ukiwa kwenye cheo chako na kukudai rejesho usipotoa litaondoka na wewe au litaondoka na cheo

Mtoa mada unapotaka kufanya biashara ukachanganya na Giza lazima ujue kuna gharama ya Giza lazima uilipe moja lazima ukubari kwa hali na mali kushiriki ibada zote za Giza mbili lazima upeleke rejesho kwenye madhabahu ya Giza tatu usisahau hayo mawili maana ukisahau utakumbushwa na usipotii utapelekwa Gizani mazima au kubakia ukiwa mikono mitupu
 
Km ulipata Pesa ukatafuta cheo ukapata cheo kwa Pesa zako za Giza basi jua ipo siku Giza litakufuata ukiwa kwenye cheo chako na kukudai rejesho usipotoa litaondoka na wewe au litaondoka na cheo

Mtoa mada unapotaka kufanya biashara ukachanganya na Giza lazima ujue kuna gharama ya Giza lazima uilipe moja lazima ukubari kwa hali na mali kushiriki ibada zote za Giza mbili lazima upeleke rejesho kwenye madhabahu ya Giza tatu usisahau hayo mawili maana ukisahau utakumbushwa na usipotii utapelekwa Gizani mazima au kubakia ukiwa mikono mitupu
🤣🤣🤣🪑
 
nimekuelewa hapa. Na mbaya zaidi giza linapodai yake linaweza kusababisha wasiohusika kukumbwa na kadhia . Wenyewe wanaita collateral damage
 
Giza litakutafuta kudai rejesho usipotoa litaondoka na wewe au litaondoka na kile ulichopewa kutoka Gizani

Sasa hapo ni wewe kuamua utoe rejesho, uondoke na Giza au upoteze kile ulichokichukua Gizani
 
Nipo hapa kwa kitanda usiku huu wa manane nikiwa na msongamano wa mawazo na kutafakari mambo mbalimbali kuhusu haya maisha hasa kwa sisi vijana ambao tunajitafuta na bado hatujajipata.

Haya maisha ya utafutaji yamejaa vitu vigumu na vizito ambavyo siyo rahisi mtu kukuelezea ni namna gani aliweza kufanikiwa katika maisha na kufikia level aliyopo.

Tukubali ama tukatae ila ukweli ni kwamba kila mmoja wetu katika maisha ya utafutaji ana LIGHT SIDE na DARK SIDE yake lakini upande unaomtambulisha mtu hadi akawa midomoni mwa walimwengu kwa kile anachokifanya ni DARK SIDE ambayo inakuwa ni SIRI ya mhusika na tusije danganyana. LIGHT SIDE huwa inatumika kama mfuniko na ngozi ya kuficha nyama ya ndani ambayo ni DARK SIDE.

Muda mwingine unaweza kuamini hiki kumbe sicho na kile usichokiamini ndo ndicho, kinachopaswa kuzingatiwa ni kujua na kuelewa namna ya kutofautisha kipi ni sawa na kipi siyo sawa.

Ilikuwa mwaka 2019 nilijichangachanga nikapata kama 2.5 Milion nikafungua biashara ya duka la chakula(duka la mangi) maeneo fulani hapa jijini Dar es Slaam. Baada ya kufanya biashara kwa takribani miezi 2, nilianza kutotamani kwenda kufungua hii biashara yangu yaani ilikuwa kila nikitaka kwenda kazini kunakuwa na kaubaridi jumlisha uoga, miguu kuwaka moto nikiwa maeneo ya biahara, kuchoka na kuumwa ghafla ambao hadi leo hii sijawahi kuelewa shida ilikuwa nini japo mm huwa ni muoga na kutoamini sana mambo ya nguvu za giza.

Motokeo yake niliamua kufunga ile biashara kwa kuuza vitu kwa bei ya jumla kwa hasara kubwa mno na baada ya hapo niliamua kuachana na masuala ya biashara nikajikita kwenye mishe zangu zingine.

Mwaka jana baada ya zoezi la sensa(2022), wazo la biashara lilinijia nikajichangachanga nikafungua biashara ya kuuza mabegi ya mtumba hasa haya ya watoto wa shule na watu wazima hasa wale wa kwenda site i.e kubebea vitu vya mafundi. Niliamua liwalo na liwe hata iweje ile hali ya kukatia tamaa biashara yangu kama ingenijia, ningekaza na nisingejaribu kukata tamaa.

Nilipambana na hiyo biashara wee japokuwa kuna muda ile hali ilikuwa inanijia lakini nilijikaza kiume. Kuna kipindi mwanzoni mwanzoni km February mwaka huu(2023) biashara ikawa ngumu kiasi hivyo nikaona nihamishe location ya biashara. Nilihamia sehemu yenye mzunguko wa watu na biashara ilichangamka sana hadi nikawa nauza hadi 20 bags per day.

Baada ya muda km miezi 3 toka nihamie hii location mpya, biashara ilianza kuwa ngumu ghafla kwangu ikawa hata kwa siku naweza uza 1 bag au nisiuze kabisa na mzigo upo wa kutosha. Uvumilivu ulinishinda nikamshirikisha mwanangu mmoja hivi akanielekeza kwa mtaalamu(Sangoma)mmoja huko mbagala chamazi ndani ndani. Ni kweli baada ya mtaalamu mambo yakawa mwororo kama kwa muda wa mwezi mmoja hivi na ghafla mambo yakawa magumu tena balaa. Niliona hata kama uvumilivu wa kibiashara si kwa mtindo huu, yaani majumuisho ya mauzo kwa mwezi ni 10 bags.
Niliamua kufunga hii biashara maana sikutaka kuwa mtumwa tena wa kwenda kwa mtaalamu.

Enyi motivation speakers hasa wa masuala ya biashara, mkiwa mnawaponda watu wanaofunga biashara kwa falsafa zenu eti kukosa mitaji, ubunifu na usimamizi mbaya, basi muwe mnakumbuka kuwa kuna masuala ya nguvu za giza na mnapaswa kuyajumlisha km mojawapo ya changamoto zinazosababisha biashara kufungwa.

Wako katika ujenzi wa Taifa,
DON YRN.
Young rich niggars
 
Usifanye biashara uswahilini.. eneo lenye watu wa pwani wengi hasa wamakonde achana nalo utafeli
 
Ulikuwa unauzia wap
 
Back
Top Bottom