Vijana tujiari Serikalini hakuna ajira

thomas_360

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
1,459
1,428
Habarini wakuu.

Najua watakaopitia huu Uzi ni Watu wa Rika mbali mbali kuna waliofanikiwa, kuna wanahangaika mtaani na kuna wale ambao wapo masomoni bado na kuna wale ambao hawaelewi wafanye nini mtaani.

Mtaani kuna kazi za aina mbalimbali ambazo mtu unaweza ukaamua na ukafanya kama una mtaji binafsi au hata kusaidiwa na wazazi au ndugu jamaa na marafiki....Ukweli ni kwamba Ajira serikalini ni mchezo wa bahat nasibu kwa siku hizi so kama kijana hupaswi kuweka malengo 80% kuwa utapata kazi huko.

Binafsi nilihitimu chuo na kupata degree yangu ya kwanza na kuamini kuwa nikimaliza basi ajira ipo na sio serikalini tu hata katika private sector.

Baada ya kuhitimu ilikuwa kama bahati nikapata sehemu ya kujishikiza maana haikuwa ajira rasmi maana mshahara ulikuwa wa kawaida sana...Niliendelea kupiga kazi huku natafuta sehemu kwingine ila mambo hayakuwa kama nilivyotegemea.

Mwisho wa siku nikaamua kutokutafuta kazi sehemu nyingine maana umri unakimbia so nikaamua kutafuta pikipiki ya mkataba maana sikuwa na pesa CASH na kwa kuwa naweza kuendesha chombo basi nikajiingiza kwenye bodaboda na degree yangu.

KUMBUKA KUWA AJIRA yangu sijaiacha yaani nafanya kazi mbili kwa nyakati tofauti....ratiba ni kwamba kuanzia alfajiri mpaka saa mbili kasorobo nafanya boda boda, saa mbili asubuh mpaka saa kumi na moja jioni nakuwa kazini. kuanzia saa kumi na moja na nusu jioni mpaka saa mbili nafanya boda boda.

Wakati wa kuanza kuna kuwa na ugumu lakini kadri siku zinavyoenda mambo yanakuwa kawaida, na nashukuru mungu kwa siku hizo za kazi napambana na huwa napata angalau 15000 kwa siku ili hesabu ya pikipiki niipate nakama siku ikienda vibaya sio mbaya mwisho wa siku nachukua ela kwenye mshahara wangu wa week najazia then napeleka hesabu ya watu.

Siku za Jumamosi na Jumapili nakuwa nipo free maana siingii kazini so boda nafanya full time na katika siku hizi mbili na uwezo wa kutengeneza faida ya sh. 50000 kwa mtaji wa mafuta ya sh. 15000 na sio kwamba yanakuwa yameisha na mengine yanabakia ila hiyo ndo average.

So vijana naomba niwaambie kuwa wanaofanya bodaboda wanadharaulika lakini inalipa ukiwa makini na wala usiangalie watu watakufikiriaje we pambna mwisho wa siku unakula vizuri, unavaa vizuri na unakuwa na malengo basi maneno ya nje yasikutishe wala kukukatisha tamaa.

Malengo ni kuwa nikimaliza mkatab a napAmbana kununua pikipiki ya Pili kisha moja natoa kwa mkataba ambapo pesa itakayo kuwa inakusanywa basi nitanunua pikipiki ya tatu ambayo itakuwa inaleta hesabu pia.

VIJANA USIRIDHIKE HAPO ULIPO PAMBANA NA USICHAGUE KAZI PESA INATAFUTWA POPOTE IMRADI IWE YA HALALI....NASHUKURU NA NAWASALIMIA KWA JINA LA MUUNGANO WA TANZANIA.....NA KAZI IENDELEEEEEEEEE...HAKUNA KUFELI
 
Wasomi wetu tunaowategemea mnatuangusha sana. Ungesema kuna jambo unalitafuta pesa kulifanya kulingana na madarasa uliyonayo, ungenitia moyo kuona siku za usoni tutaanza kufaidi fikra za kisomi.

Akili ni kile unachobakiwa nacho baada ya kutoa elimu ya darasani. Kama sisi wa la nne B tunawaza kujikwamua kupitia bodaboda na wewe pia mwenye AKILI + Madarasa uwaze kama sisi?

Mbona hili li-nchi ni li kubwa sana na lina matatizo kibao! Nyie wasomi hamuwezi kutusaidia hata kurahisisha maisha kwa kutatua vikero hivyi vya kimazingira kutokana na elimu zenu?

Piga bodaboda, kusanya pesa, fanya tatuzi moja kwa level ya elimu yako, geuza changamoto moja kuwa fursa yako....unamkuta mtu amesomea vyuma huko, naye analalamika hakuna ajira kama sisi, dokta naye anatafuta kazi kama mwanasheria au mwalimu.
 
upo sawa ila kila mtu anaplaNi na malengo yake...Kikubwa mwisho wa siku ugali unafika mdomoni na maendeleo mengine. kama nikiwa nauwezo wa kumiliki pikipiki 10 huoni nitakuwa nimesaidia jamii kwa kuajiri vijana 10 ??
 
Elimu ya Tanzania haiendani kabisa na maisha khalisi ya mtaa. Sasa msomi umemaliza degree unaennda kuwa boda boda. Yani hata Ile elimu yako haina maana. Tena ivyo hukupaswa kwenda level za mbali ivyo halafu uje kuwa bodaboda. Tafuta dhumuni la kwanini wewe umesoma Hadi degree japo unaendelea kutafuta pesa kupitia bodaboda.
 
Mnaongea hivi kwa kuwa mnamaisha tayari....
 
Elimu ya Tanzania haiendani kabisa na maisha khalisi ya mtaa. Sasa msomi umemaliza degree unaennda kuwa boda boda. Yani hata Ile elimu yako haina maana. Tena ivyo hukupaswa kwenda level za mbali ivyo halafu uje kuwa bodaboda. Tafuta dhumuni la kwanini wewe umesoma Hadi degree japo unaendelea kutafuta pesa kupitia bodaboda.
Ulitaka afanyaje na usomi wake?

Alafu lazima ujue , kila mtu anakuwa na plans zake, kuna long plan na short plan, siku zote Short plans ndio zina facilitate achievement of long plans.

Mfn, long plans zako ni kumiliki kiwanda, sasa unataka kumiliki kiwanda na hauna mtaji, utafanyaje?

Sasa lazima uwe na short plan, ambayo itakupata capital kuja Ku facilitate hiyo long plan ya kuwa na kiwanda,

Sasa Short plan, ya mtoa mada, ni kama hivyo, kuendesha boda , kuajiriwa, etc, lengo apate capital ili long plans zake zitimie kupitia Short plans.

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
well said mkuu....
 
Hongera mleta mada. Usikatishwe tamaa na wapinzani. Halafu hawa wanaokuponda wanajisahaulisha kuwa hata hiyo kozi uliosomea imebesi sana kwenye theory badala ya practical.
maneno ya watu kama hao huwa kwangu yanaingia sikio la kulia yanatokea sikio la kushoto....kama nauwezo wa kuingiza faida ya sh. 60000 kwa mtaji wa mafuta ya sh. 15000 na hapo nafunga hesabu saa moja jioni. kwann nibabaishwe na maneno ya wakosa maarifa?? au wanataka watu wakakabe huko mtaani??
 
Uko sahihi mkuu
Wasomi wetu tunaowategemea mnatuangusha sana. Ungesema kuna jambo unalitafuta pesa kulifanya kulingana na madarasa uliyonayo, ungenitia moyo kuona siku za usoni tutaanza kufaidi fikra za kisomi.

Akili ni kile unachobakiwa nacho baada ya kutoa elimu ya darasani. Kama sisi wa la nne B tunawaza kujikwamua kupitia bodaboda na wewe pia mwenye AKILI + Madarasa uwaze kama sisi?

Mbona hili li-nchi ni li kubwa sana na lina matatizo kibao! Nyie wasomi hamuwezi kutusaidia hata kurahisisha maisha kwa kutatua vikero hivyi vya kimazingira kutokana na elimu zenu?

Piga bodaboda, kusanya pesa, fanya tatuzi moja kwa level ya elimu yako, geuza changamoto moja kuwa fursa yako....unamkuta mtu amesomea vyuma huko, naye analalamika hakuna ajira kama sisi, dokta naye anatafuta kazi kama mwanasheria au mwalimu.
 
Wasomi wetu tunaowategemea mnatuangusha sana. Ungesema kuna jambo unalitafuta pesa kulifanya kulingana na madarasa uliyonayo, ungenitia moyo kuona siku za usoni tutaanza kufaidi fikra za kisomi.

Akili ni kile unachobakiwa nacho baada ya kutoa elimu ya darasani. Kama sisi wa la nne B tunawaza kujikwamua kupitia bodaboda na wewe pia mwenye AKILI + Madarasa uwaze kama sisi?

Mbona hili li-nchi ni li kubwa sana na lina matatizo kibao! Nyie wasomi hamuwezi kutusaidia hata kurahisisha maisha kwa kutatua vikero hivyi vya kimazingira kutokana na elimu zenu?

Piga bodaboda, kusanya pesa, fanya tatuzi moja kwa level ya elimu yako, geuza changamoto moja kuwa fursa yako....unamkuta mtu amesomea vyuma huko, naye analalamika hakuna ajira kama sisi, dokta naye anatafuta kazi kama mwanasheria au mwalimu.
Aisee yaaani wewe unamshangaa kijana kapambana kasoma kwa mkopo wa bodi mpk kamaliza chuo unaacha kushangaa watu walishakua wabunge miaka,walipokosa ubunge hawajui cha kufanya tena wamekaaaa tu mpk waje kujipendekeza wateuliwe.
Wengine wananunuliwa mpk wanahama vyama vyao na kupewa ubunge kwa lazima kwingine.
Joshua nassari kawa mbunge kasoma mpk marekani karudi kupigania apewe udc,

Akina halima mdee walikosa ubunge wakasaliti mpk vyama vyao mtaani hakuna la kufanya nje ya ubunge,ikabidi wabadili gia,mtaani ni kugumu

Tatizo mkishakula mkishiba mnaanza kukejeli vijana wanaotafuta maisha.
Nchi ina watu wa ajabu ajabu tu
Kujiajiri sio lelemama
Ukishakua umeajiriwa ni rahisi kuwaambia wenzako
MKAJIAJIRI SERIKALINI HAKUNA NAFASI,ELIMU YA SIKU HIZI HAINA SKILLS UTADHANI KUNA LA MAANA MLILOFANYA ZAIDI YA KUJIKOMBA ILI MTEULIWE NA KULINDA NAFASI ZENU
 
Aisee yaaani wewe unamshangaa kijana kapambana kasoma kwa mkopo wa bodi mpk kamaliza chuo unaacha kushangaa watu walishakua wabunge miaka,walipokosa ubunge hawajui cha kufanya tena wamekaaaa tu mpk waje kujipendekeza wateuliwe.
Wengine wananunulia kuhama vyama vyao na kupewa ubunge kwa lazima kwingine
Kujiajiri sio lelemama
Ukishakua umeajiriwa ni rahisi kuwaambia wenzako
MKAJIAJIRI SERIKALINI HAKUNA NAFASI
hawa ndo wale wa kilimo cha mdomoni ili kwenye field hawajui changamoto zake
 
chombo hicho
02440077b23e95aa3bcfa3ccf284cbcb.jpg
 
Back
Top Bottom