thomas_360
JF-Expert Member
- Oct 11, 2015
- 1,459
- 1,428
Habarini wakuu.
Najua watakaopitia huu Uzi ni Watu wa Rika mbali mbali kuna waliofanikiwa, kuna wanahangaika mtaani na kuna wale ambao wapo masomoni bado na kuna wale ambao hawaelewi wafanye nini mtaani.
Mtaani kuna kazi za aina mbalimbali ambazo mtu unaweza ukaamua na ukafanya kama una mtaji binafsi au hata kusaidiwa na wazazi au ndugu jamaa na marafiki....Ukweli ni kwamba Ajira serikalini ni mchezo wa bahat nasibu kwa siku hizi so kama kijana hupaswi kuweka malengo 80% kuwa utapata kazi huko.
Binafsi nilihitimu chuo na kupata degree yangu ya kwanza na kuamini kuwa nikimaliza basi ajira ipo na sio serikalini tu hata katika private sector.
Baada ya kuhitimu ilikuwa kama bahati nikapata sehemu ya kujishikiza maana haikuwa ajira rasmi maana mshahara ulikuwa wa kawaida sana...Niliendelea kupiga kazi huku natafuta sehemu kwingine ila mambo hayakuwa kama nilivyotegemea.
Mwisho wa siku nikaamua kutokutafuta kazi sehemu nyingine maana umri unakimbia so nikaamua kutafuta pikipiki ya mkataba maana sikuwa na pesa CASH na kwa kuwa naweza kuendesha chombo basi nikajiingiza kwenye bodaboda na degree yangu.
KUMBUKA KUWA AJIRA yangu sijaiacha yaani nafanya kazi mbili kwa nyakati tofauti....ratiba ni kwamba kuanzia alfajiri mpaka saa mbili kasorobo nafanya boda boda, saa mbili asubuh mpaka saa kumi na moja jioni nakuwa kazini. kuanzia saa kumi na moja na nusu jioni mpaka saa mbili nafanya boda boda.
Wakati wa kuanza kuna kuwa na ugumu lakini kadri siku zinavyoenda mambo yanakuwa kawaida, na nashukuru mungu kwa siku hizo za kazi napambana na huwa napata angalau 15000 kwa siku ili hesabu ya pikipiki niipate nakama siku ikienda vibaya sio mbaya mwisho wa siku nachukua ela kwenye mshahara wangu wa week najazia then napeleka hesabu ya watu.
Siku za Jumamosi na Jumapili nakuwa nipo free maana siingii kazini so boda nafanya full time na katika siku hizi mbili na uwezo wa kutengeneza faida ya sh. 50000 kwa mtaji wa mafuta ya sh. 15000 na sio kwamba yanakuwa yameisha na mengine yanabakia ila hiyo ndo average.
So vijana naomba niwaambie kuwa wanaofanya bodaboda wanadharaulika lakini inalipa ukiwa makini na wala usiangalie watu watakufikiriaje we pambna mwisho wa siku unakula vizuri, unavaa vizuri na unakuwa na malengo basi maneno ya nje yasikutishe wala kukukatisha tamaa.
Malengo ni kuwa nikimaliza mkatab a napAmbana kununua pikipiki ya Pili kisha moja natoa kwa mkataba ambapo pesa itakayo kuwa inakusanywa basi nitanunua pikipiki ya tatu ambayo itakuwa inaleta hesabu pia.
VIJANA USIRIDHIKE HAPO ULIPO PAMBANA NA USICHAGUE KAZI PESA INATAFUTWA POPOTE IMRADI IWE YA HALALI....NASHUKURU NA NAWASALIMIA KWA JINA LA MUUNGANO WA TANZANIA.....NA KAZI IENDELEEEEEEEEE...HAKUNA KUFELI