Hii ni kwa wahasibu na wafanyabiashara

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
174
618
Nitaongelea zaidi uhasibu, kwa sababu ndo fani Ninayoizungumzia zaidi, katika kazi ya uhasibu ina changamoto mbalimbali, kama kulipa loss etc. Mfano siku umefanya mauzo ya sh milioni moja, lakini baada ya kufunga hesabu zako ukapata laki tisa lazima ulipe laki moja ili hesabu ifunge, ndo hivyo kazi zetu hizi.

Sasa nauliza je ukipata mteja amekupa kiwango zaidi tofauti na anachotamka utamrudishia pesa yake au utaichikichia (kufanyia matumizi yako binafsi) anasema kakupa laki mbili lakini kila ukihesabu unakuta imezidi elfu ishirini unamuuliza Mara mbili mbili anataja hiyo hiyo laki mbili lakini kila ukirudia kuhesabu imezidi!!!..

Halafu kingine nauliza mnatumia njia gani kuhakikisha hupati loss maana sio kila sehemu kuna machine za kuhesabia pesa nauliza kwa sisi ambao tunapokea hela by hand.

Msaada tafadhali maana kuna ile ukidhani mteja amekupa pesa kumbe hajakupa utajikuta umemwandikia risiti na hakushtui kama hajalipa badae ukifunga hesabu unapata loss, utakuta una kazi ya kulipa loss tu
 
Back
Top Bottom