Vijana takriban 40 wauawa baada ya 'kumzodoa' Mtumishi wa Mungu!

Vijana takriban 40 wauawa baada ya 'kumzodoa' Mtumishi wa Mungu!

Duh, KERATO MOMBAA
Inaonekana unapenda konyagi. Jiepushe na ulevi ndugu.
Walevi hawataurithi ufalme wa Mungu(Wakorintho 6:9-10)
Mkuu, mm siyo mlevi hata kidogo!
Nikumbushe kdogo kwenye biblia kitabu cha mithali kuna sehemu kinasema "mpe masikini kilevi asahau shida zake" HII UNAIZUNGUMZIAJE MKUU!
 
Asante mkuu, kwa comment yako. Ni kweli habari hiyo ipo katika kitabu cha 2 Wafalme 2:23–24.

Ngoja nikufafanulie kwa kina, maana umesema tafsiri za Kiswahili zimechakachuliwa! Neno la Kiebrania lililotafsiriwa kama "watoto" (na'ar) halimaanishi watoto wadogo tu. Linaweza kumaanisha pia kijana mdogo hadi kijana mkubwa (kama Daudi alipomwua Goliathi bado aliitwa "na'ar"). Kwa muktadha wa tamaduni za Kiebrania, walikuwa watu wazima kiakili waliostahili kuwajibika kwa maneno yao.

Hii haikuwa dhihaka ya kawaida – ilikuwa dhihaka ya kiroho. Kumbuka, Elisha alikuwa amechukua nafasi ya Eliya, na watu wengi walikuwa wakikataa manabii wa kweli na kumgeukia Baali na ibada potovu. Hawa vijana walimtania kwa makusudi – "Paa wewe!" – kama kejeli kwa Eliya aliyepaa mbinguni. Walikuwa wakidharau kazi ya Mungu hadharani. Huu haukuwa mzaha tu; ulikuwa uasi wa wazi dhidi ya Mungu kupitia mtumishi wake. Hawakuwa watoto hao. Walikuwa vijana wenye ufahamu kuhusu Eliya. Watoto wangejuaje kwamba Eliya alipaa na kujua kuwa Elisha alikuwa successor wa Eliya?

Halafu, haikuwa Elisha aliyeleta dubu – bali Mungu. Elisha aliwalaani tu kwa jina la Bwana kisha Mungu akaamua kushughulikia dhihaka hiyo kwa njia ile. Hii inaonyesha kuwa lilikuwa somo la kiroho – si chuki binafsi ya mtumishi huyo. Mungu ndiye aliyehukumu, si Elisha kama mtu.

Kuhusu Elisha kumchinja mfalme, hakuna sehemu iliyo wazi inayoonyesha kuwa Elisha mwenyewe alimchinja mfalme kwa mkono wake. Mara nyingi alikuwa anatoa maagizo ya kinabii, na hukumu ya Mungu ilikuwa inatekelezwa na wafalme au jeshi. Kama una andiko la moja kwa moja linalosema Elisha alichinja mtu kwa mkono wake, liweke hapa na mimi nijifunze.

Kwa mtazamo wako, unaona ule ulikuwa ukatili wa hali ya juu. Lakini tunapotafsiri matukio ya kihistoria ya Biblia, ni muhimu kuelewa muktadha wa kiroho, kisiasa, na kijamii wa wakati ule. Kulingana na Mungu, dhihaka ya makusudi dhidi ya mamlaka yake ya kiroho ni kosa kubwa sana.

Niseme tu kwamba habari hii inafunua jinsi ambavyo Mungu anachukulia kwa uzito dhihaka, dharau kwa watumishi wake, na uasi wa kizazi dhidi ya mamlaka ya kiroho. Mungu akusaidie kuyajua mapenzi yake hata kupitia habari hii.

Kumbuka Paulo(Sauli) alivyopigwa upofu baada ya kuwatesa wafuasi wa Yesu. Kwa neema tu alipona na kuwa Mtume. Kumbuka Anania na Safira jinsi walivyokufa baada ya kumwambia uongo Mtumishi wa Mungu, Petro. Mungu ni wa upendo lakini pia ni wa haki. Ndio sababu wanaokataa wokovu sasa, watachomwa moto milele na milele.

AMINA. Ubarikiwe mtumishi, kuna kitu kipya nimekipata hapa!
 
Mji fulani ni upi?umesema ni story ya ukweli tutajie mji na sisi tuofuatile habari kwa kina
 
Habari hii ni ya kweli kabisa. Sio chai wala udaku.

Taharuki imetanda katika mji mmoja baada ya tukio la kutisha lililowahusisha vijana zaidi ya 40 walioshambuliwa na wanyama wakali wa porini.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo karibu na eneo la tukio, kundi la vijana zaidi ya 40 lilijikuta katika hali ya hatari baada ya kumcheka na kumdhihaki Mtumishi wa Mungu aliyekuwa akipita njiani. Walimzodoa kwa maneno ya dhihaka kuhusu kichwa chake chenye upara. Vijana hao walimzomea kwa sauti na kejeli na kumwambia: "Paa wewe, mzee Kipara!"

Muda mfupi baada ya dhihaka hizo, dubu wawili wa porini(wild bears) walitokea ghafla na kuanza kuwashambulia vijana hao bila huruma, wakasababisha vifo vya vijana 42!

Tukio hili limechochea mjadala mkubwa, wengi wakisema ni somo kali kwa kizazi kinachopenda mzaha na kukosa heshima kwa wakubwa. Na wengine wakihusisha tukio hilo na laana.

Endelea kufuatilia uzi huu kwa taarifa/ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hili la kushangaza.
Hilo eneo halina jina? Huyo mtumishi hana jina?
 
Hilo eneo halina jina? Huyo mtumishi hana jina?
Mwaka ni 2025.

Mtu analeta habari anasema habari hii ni ya kweli kabisa!
- hataji jina la eneo tukio lilipotokea
  • hakuna jina la mtumishi
  • hakuna source ya taarifa
  • hakuna picha/video/ushahidi wowote ule!
 
Back
Top Bottom