Vijana acheni kuwekeza sana kwenye decorations za duka badala ya stock

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
619
1,517
Mojawapo ya kosa kubwa sana la kiufundi kwa vijana wengi wadogo wanaoanza biashara ni kuwekeza pesa nyingi kwenye vitu ambavyo havirudishi pesa kwa haraka au pengine havirudishi kabisa. Vijana wanafungua maduka ila wengie hawafikishi mwaka mmoja wamefunga baada ya kushindwa biashara.

Vijana wanafanya makosa mbalimbali ya kiufundi ila kosa lililoshika kasi zaidi ni kutumia pesa nyingi sana kufanya decorations ya duka badala ya kununua mzigo wa kutosha. Imekuwa kawaida kuona bajeti ya decorations milioni 5 halafu mzigo wa dukani milioni 3. Ukiliona duka kwa nje ni zuri balaa hadi ndani ila mzigo ni mdogo usioendana na hadhi ya duka. Wengine hufanga kosa zaidi kwa kuteketeza pesa kufanya sherehe ya uzinduzi wa duka (launching party).

Ninawashauri vijana wakiwa wanafungua duka wafanye decorations za kiasi kidogo sana ila baadae wakijaliwa watafanya decorations kali kwa kutumia sehemu ya faida iliyopatikana kwenye biashara. Vijana acheni kushangilia ushindi wakati hata mechi bado. Hakikisheni mnanunua stock ya kutosha. Huo ndo usalama wa biashara.
 
Hizo decoration wakati fulani zinaweza kuwakimbiza wateja wakihisi kwa uwezo wao hawawezi kununua bidhaa zilizomo kwa kudhani bei itakuwa ghali sana, kuna bucha fulani lilifunguliwa limefanyiwa decorations za kufa mtu mpk unahisi humu kweli nikitaka nyama robo wanapima kweli!! Au bei yake ndiyo hii sawa na bucha za kawaida

Basi inabidi ulipite tu uende bucha za kawaida hizi mpk walipobandika bei ndiyo mtu anafahamu kumbe bei sawa tu ni mbwembwe tu decorations hata wanyonge wanaweza kuingia
 
Back
Top Bottom